Misingi Ya BIBLIA
Somo La 5: Ufalme wa Mungu
Kuelezea wazi kabisa Kuhusu Ufalme | Kwa Sasa Ufalme Haujasimikwa | Ufalme wa Mungu uliopita | Ufalme wa Mungu kwa Wakati Ujao | Miaka Elfu - Kikwi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Ufalme wenyewe, Maelezo mafupi ya Historia ya Israeli) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 16: Maelezo mafupi ya Historia ya Israeli

ABRAHAMU aliitwa atoke Uru ya Wakaldayo; Myahudi wa kwanza. Mungu akafanya ahadi naye kuhusu nchi ya Kanaani, na uzao wake. Alikufa asijazipokea hizi ahadi.

ISAKA. Abrahamu alijiweka tayari kumtoa mwanae awe dhabihu. Kwa sababu Abrahamu alikuwa mwaminifu, Mungu akathibitisha ahadi zake kwa Abrahamu kwa kiapo. Hiari ya Isaka kufa kwa kumtii baba yake alichomwamuru ni mfano wa Kristo. Ahadi zilirudiwa kwa Isaka (Mwa. 26: 3-5).

YAKOBO alikuwa mwana wa Isaka. Ahadi zilirudiwa kwake pia . Alikuwa na wana 12 - Reubeni alikuwa mwana mkubwa, Benjamini alikuwa kitinda mimba. Lawi alikuwa ni mmoja ambaye makuhani walizaliwa naye. Yusufu alipendwa mno.

YUSUFU. Akiwa kijana aliota ndoto mbili zilizoonyesha picha kuwa yeye ni mtawala juu ya ndugu zake.Wakamwonea wivu, wakamuuza kama mtumwa katika nchi ya Misri. Huko akawa mtawala, akapanga kukusanya nafaka za kutumia wakati wa miaka saba ya njaa iliyoikumba nchi, wakati wa kipindi hiki, Yakobo na wanawe wakaja kuishi na Yususfu katika nchi ya Misri. Wao na watoto wao wakaishi sehemu ya Gosheni, sehemu ya Misri. Farao aliyekuja baadae akawatesa watu wa Israeli, kwa kuwafanya watumwa.

MUSA akazaliwa wakati huu; akiwa mtoto mchanga alifichwa katika kikapu, na kisha kukutwa na binti wa Farao na akafanywa kuwa wake wakati akiwa kijana, akamuua Mmisri aliyekuwa anampiga mwisraeli. Ndipo Musa akakimbilia Midani, ambako alifanya kazi ya kulisha wanyama kwa miaka 40 kwa Yethro.Ndipo Mungu akamtokea katika kijiti kilichokuwa kinawaka moto. Akaambiwa aende kwa Farao na kutaka ukombozi wa Israeli. Alifanya ishara za miujiza ili kuthibitisha kuwa ametumwa na Mungu. Walakini Farao hakuwafungua Israeli waondoke, basi mapigo kumi yalitumwa juu ya Misri, yaani Vyura, giza, Mvua ya mawe, na mwishowe kuua kila mzaliwa wa kwanza mwanaume. Israeli ilibidi wachinje mwana kondoo na kunyunyiza damu juu ya milango yao. Hii ilionyesha tukio moja mbele jinsi damu ya Yesu inavyoweza kutuokoa toka mauti. Siku kuu hii ilikuja julikana kuwa Pasaka .

KUTOKA. Hatimaye Israeli waliachwa waondoke Misri - walisafiri huku wakiongozwa na malaika wa Mungu katika nguzo ya wingu wakati wa mchana, na nguzo ya moto wakati wa usiku. Jeshi la Farao lilifuata nyuma yao mpaka Bahari ya shamu. Kwa miujiza maji yaligawanyika ili watu wapite, kisha maji yalirudi mahali pake na kuua wamisri. Ndipo wakasafiri kupita jangwani kuelekea nchi ya ahadi ya Kanaani. Mungu aliwapa maji ya kunywa toka kwenye mwamba, na mkate kwa namna ya mana walipewa kila asubuhi. Walipofika mlima Sinai, Mungu akawapa amri kumi na sheria ya Musa. Wakati huo wakawa ni ufalme wa Mungu. Wakaamriwa kufanya hema maalum, waliita hema ya kukutania ambapo Mungu aliabudiwa. Walipewa kuhani mkuu na makuhani ambao wanaweza kutoa dhabihu kwa Mungu. Asili yote ya hiyo masikani na ukuhani vililenga mbele kwa ujio wa Yesu.

NCHI YA AHADI hatimaye waliisogelea, Wapeleezi 12 walitumwa, kumi kati yao walirudi wakisema ni vigumu kuimiliki nchi ya Kanaani. Wapelelezi wengine wawili Yoshua na Kalebu, walisema ukweli - kwamba nchi wataitamalaki, ikiwa wanaamini ahadi za Mungu. Kwa sababu watu walishiriki mwenendo wa wapelelezi kumi, Israeli ikabidi wazunguke jangwani kwa miaka 40 hata wale wote waliokuwa na umri wa miaka 20 na zaidi walipotoka Misri walipokufa.

YOSHUA alimfuata Musa kuongoza wana Israeli kuingia nchi ya Kanaani mji wa kwanza kutawaliwa ulikuwa Yeriko, ambao Rahabu aliishi, kisha Ai. Mara walipowekwa katika nchi, waliongozwa kwa vipindi vya WAAMUZI, ingawa Mungu alikuwa mfalme wao wa kweli. Hawa ni pamoja na watu kama Gideoni, Yefta na Samsoni. Wote waliwakomboa Israeli toka mikononi mwa adui zao, walipotubu kumkosea Mungu.

Historia ya Israeli ina mifano iliyojaa tele ya Israeli kutokumtii Mungu wakaadhibiwa na uvamizi wa Mataifa yaliyo kando kando, wakitubu dhambi zao Mungu aliwaokoa - na kisha wakaendelea kutenda dhambi tena. Mwamuzi wa mwisho alikuwa ni Samweli. Katika kipindi chake, watu wa Israeli walimkataa Mungu kuwa mfalme wao walipoomba wapewe mfalme mwanadamu, kama mataifa yaliyowazunguka.

WAFALME. Mfalme wao wa kwanza aliitwa Sauli ambaye ingawa alianza vema, aligeuka kuwa mtu mbaya, aliasi amri za Mungu, na kumtesa Daudi. Baada ya kifo chake, Daudi akawa mfalme aliyefuata, alikuwa mtu bora wa Israeli. Mungu akafanya ahadi kubwa kwake. Baada yake akaja mwanae Suleimani ambaye baada ya kuanza vizuri aliiacha imani ya kweli kwa sababu ya kuoa wanawake wageni wengi toka mataifa yaliyowazunguka. Baada yake ufalme uligawanyika sehemu mbili - Kabila kumi wakafanywa ufalme wa Israeli, ulianza chini ya Yeroboamu; kabila zingine mbili, Yuda na Benjamini, zikaunda ufalme wa Yuda, ulianza chini ya Rehoboamu, mwana wa Suleimani.

Ufalme wa Israeli (kabila kumi) haukuwa na mfalme yeyote mzuri. Daima walikuwa ni waasi juu ya Mungu. Alitumia manabii wengi kuwasihi watubu, bali hawakutaka.Kwa hiyo Waashuru wakawahusuru, na kuwatwaa kwenda utumwani. Walitawanyika ulimwenguni pote.

Ufalme wa Yuda (kabila Mbili) ulikuwa na wafalme wazuri wachache (yaani, Asa na Hezekia), Lakini, hata wao pi hawakumtiii Mungu. Wakaldayo wakatumwa kuvamia, wakawachukua utumwani Babeli; kwa muda wa miaka 70. Hawakuwa na mfalme tena. Baada ya miaka 70 wengine walirudi nchini Israeli chini ya uongozi wa Ezra, Nehemia, Yoshua (kuhani mkuu wakati ule) na Zurubabeli mtawala. kwanza walitawaliwa na Waajemi, kisha Wayunani na mwishowe Warumi. walikuwa chini ya Waroma Yesu alipozaliwa. Kama tokeo la kumkataa Yesu Wayahudi, Mungu alituma Waroma kuungamiza Yerusalemu mnamo mwaka 70 B.K, na hatimaye Wayahudi wote walitolewa katika nchi ya Israeli.

Kwa miaka ya karibuni , Wayahudi wameanza kurudi katika nchi , ni kutimia nusu kwa unabii wa Agano la Kale. Kufufuka kwa Serikali ya Israeli ni ishara ya kweli kuwa Yesu atarudi tena ufalme wa Israeli ukiwa ni ufalme wa Mungu.


  Back
Home
Next