Misingi Ya BIBLIA
Somo La 5: Ufalme wa Mungu
Kuelezea wazi kabisa Kuhusu Ufalme | Kwa Sasa Ufalme Haujasimikwa | Ufalme wa Mungu uliopita | Ufalme wa Mungu kwa Wakati Ujao | Miaka Elfu - Kikwi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Ufalme wenyewe, Maelezo mafupi ya Historia ya Israeli) | Maswali

5.1 Kuelezea wazi kabisa Kuhusu Ufalme

Masomo yetu yaliyotangulia yameonyesha kuwa ni kusudi la Mungu kuwapa tuzo watu wake waaminifu kwa uzima wa milele Kristo akirudi. Uzima huu wa milele utatumiwa duniani; Ahadi za Mungu zilizorudiwa kuhusu hii kamwe haidokezi kuwa waaminifu watakwenda mbinguni."Injili (habari njema) ya ufalme wa Mungu"(Math. 4:23) ilihubiriwa kwa Abrahamu kwa namna ya ahadi za Mungu kuhusu uzima wa milele duniani (Gal. 3:8) Kwa hiyo"Ufalme wa Mungu utakuwa wakati baada ya Kristo kurudi ndipo hizi ahadi zitatimizwa. Wakati Mungu ni mfalme wa Mwisho juu ya viumbe vyote vya sasa, amempa binadamu hiari ya kufanya apendavyo kutawala ulimwengu na maisha yake mwenyewe kama atakavyo. hivyo kwa sasa ulimwengu umekuwa ni "Ufalme wa mwanadamu" (Dan. 4:17).

Kristo akirudi,"ufalme wa dunia hii utakuwa ufalme wa Bwana wetu, na Kristo wake naye atamiliki hata milele na milele"(uf. 11:15) Ndipo mapenzi ya Mungu na nia itatimizwa wazi wazi na kufanywa katika dunia hii. Basi, Yesu ametuamuru tuombe;"Ufalme wako uje (ili) mapenzi yatimizwe hapa duniani kama (sasa) yanavyotimizwa huko mbinguni"(Math. 6:10). Kwa sababu hii fungu la maneno "Ufalme wa Mungu"limebadilishana na "Ufalme wa mbinguni"(Math 13:11; Marko.4:11). kumbuka kuwa hatusomi'Ufalme katika mbingu’; ni ufalme wa mbinguni ambao utawekwa na Kristo duniani akirudi kama malaika wanavyotii kwa ukamilifu mapenzi ya Mungu (Zab. 103: 19 -21), ndivyo itakavyokuwa kwenye ufalme ujao wa Mungu, dunia itakapo kaliwa na wenye haki pekee, ambao wakati huo watakuwa "Sawa na Malaika" (Luk. 20:36) .

Kuingia Ufalme wa Mungu Kristo akirudi basi ni mwisho wa matokeo ya juhudi yetu yote ya Ukristo wa maisha haya (Math. 25: 34; Mdo. 14: 22); kama hivi; ni muhimu kuelewa kwa usahihi. Filipo akihubiri habari za "Kristo"imefafanuliwa akifundisha "Mambo yanayohusu Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo (Mdo 8:5,12). Mafungu ya maneno juu ya mafungu ya maneno yanatukumbusha jinsi ufalme wa Mungu ulikuwa ni mzigo mkubwa wa mahubiri ya Paulo (Mdo. 19: 8; 20:25; 28:23, 31). Kwa hiyo ni wenye maana kuu muhimu kuwa tunaelewa vya kutosha fundisho la ufalme wa Mungu, kwa kuwa ni sehemu ya muhimu kwa ujumbe wa Injili"Imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi"(Mdo. 14:22); ni nuru mwishoni mwa shimo la kupita chini ya maisha haya, na kwa hiyo kusudi la kutengeneza dhabihu ambayo maisha ya kweli ya Kristo imo.

Nebukadneza , Mfalme wa Babeli, akataka kujua mambo ya ulimwengu ujao (ona Dan. 2). Alipewa ndoto ya sanamu kubwa ya mtu, ameundwa kwa vyuma tofauti. Danieli alitoa tafsiri ya kichwa cha dhahabu kuonyesha mfalme wa Babeli (Dan. 2:38). baada yake yalikuja madola yaliyofuatana katika eneo karibu na Israeli na kumalizika na hali ambayo "Kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu na nusu yake umevunjika" (Dan. 2:42).

Uwiano wa nguvu uliopo katika ulimwengu umegawanyika kati ya mataifa mengi, mengine ni yenye nguvu na mengine ni dhaifu. ndipo Danieli aliona jiwe dogo likiipiga sanamu kwenye nyayo, likahiaribu, nalo likakua na kuwa mlima mkubwa uliojaa dunia nzima (Dan 2: 34,35). Hili jiwe lina maana Yesu u (Math. 21:42; Mdo.4:11; Ef. 2:20; 1Pet. 2:4 -8)."Mlima" atakao ufanya uwe juu ya dunia yote ni ufalme usio na mwisho wa Mungu, utakao wekwa atakapo kuja mara ya pili.Unabii huu ni ushahidi Kuwait ufalme utakuwa duniani, sio mbinguni.

Kama ufalme utasimamishwa tu katika kweli kabisa Kristo akirudi ni msemo wa mafungu mengine.Paulo anasema Yesu akihukumu walio hai na wafu "atakapofunuliwa na ufalme wake" (2Tim. 4:1). Mika 4:1 anachukua wazo la ufalme wa Mungu kuwa kama mlima mkubwa; "Lakini itakuwa katika siku za Mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya mlima, nao utainuliwa juu"; Kisha hapo yanafuata maelezo jinsi huu ufalme utakavyokuwa Duniani (Mika. 4:1 -4). Mungu atampa Yesu kiti cha enzi cha Daudi kilichokuwa Yerusalemu:"Atamiliki ……. Hata milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho"(Luk. 1:32,33). Hii inawezesha maana yakini ambayo Yesu anaanza kutawala kiti cha enzi cha Daudi, na ufalme unaanza. Huu utakuwa Yesu akirudi."Ufalme wake hautakuwa na mwisho"imeunganika na Danieli 2: 44: "Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaharibiwa kamwe: hautaachwa kwa watu wengine" Uf. 11:15 imetumika Lugha kama hii ikielezea jinsi akirudi mara ya pili,"Falme za ulimwengu zinakuwa falme za Bwana wetu na za Kristo wake, naye atamiliki milele na hata milele"Tena, inabidi uwepo wakati dhahiri hapo ufalme wa Kristo na utawala unapoanza duniani; huu utakuwa akirudi .


  Back
Home
Next