Misingi Ya BIBLIA
Somo La 5: Ufalme wa Mungu
Kuelezea wazi kabisa Kuhusu Ufalme | Kwa Sasa Ufalme Haujasimikwa | Ufalme wa Mungu uliopita | Ufalme wa Mungu kwa Wakati Ujao | Miaka Elfu - Kikwi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Ufalme wenyewe, Maelezo mafupi ya Historia ya Israeli) | Maswali

5.5 Miaka Elfu - Kikwi

Kwa kipengele hiki cha somo letu la maisha katika ufalme, msomaji mwenye kuwaza kwanza atauliza, 'Picha hii yote ya ufalme wa Mungu, Je ! haionekani kuwa ni ya mwanadamu ?’ watu katika ufalme watakuwa bado wanazaa watoto (Isa. 65: 23) na hata kufa (Isa. 65:20). Bado watu hawa watakaidi kile Kristo atakachokalisha - yaani ufalme (Isa.2:4) na bado watahitajika kufanya kazi ya kulima ili waishi, ingawa kazi hii itakuwa ya raha sana kuliko wakati uliopo. Haya yote yanaonekana kuwa kilio cha mbali toka ahadi za kwamba watu wenye haki watapata uzima wa milele, na mwili wa Uungu, kufanywa sawa na malaika, wasiooa na kuzaa (Luk. 20: 35,36). Jibu lipo katika ukweli kwamba sehemu ya kwanza ya ufalme wa Mungu itadumu kwa miaka 1000 -'Kikwi’ (ona Uf. 20: 2-7). Kipindi hiki cha kikwi kutakuwapo makundi ya watu aina mbili duniani: -

  1. Watakatifu - ni sisi hao tuliomfuata Kristo inavyokubalika katika maisha, ambao watakuwa wamepewa uzima wa milele kwenye kiti cha hukumu, Elewa:'Mtakatifu’ maana yake mtu 'aliyeitwa atoke’ anatajwa mwamini yeyote wa kweli.

  2. Watu wa kawaida wanaopatwa na mauti ambao hawakuijua Injili Kristo anaporudi - yaani hawakuwa na la kusema mbele ya kiti cha hukumu.

Kristo atakapokuja , watu wawili watakuwa kondeni, mmoja atwaliwa (kwenda mbele ya hukumu) na mmoja aachwa (Luk. 17: 36); hao wanao"achwa" watakuwa katika hili kundi la pili.

Wakiisha pata mwili wa Mungu mbele ya kiti cha hukumu, watakatifu hawataweza kufa au kuzaa watoto. Maelezo ya watu kupata vitu katika ufalme basi inabidi iwe ni kwa kundi la pili - hao walio hai Kristo anaporejea, Lakini hawakujua matakwa ya Mungu.Thawabu ya watu wenye haki ni kuwa "Wafalme na Makuhani: na kumiliki nchi"(Uf. 5:10). Wafalme inabidi wawatawale watu wengine; hao watu ambao walikuwa hawajui Injili wakati wa kuja mara ya pili wataachwa wawe hai, ili wamilikiwe. kwa njia ya kuwamo "ndani ya Kristo"tutashiriki thawabu yake - ambayo ni kuwa mfalme wa ulimwengu: "Na yeye ashindaye ….. nitampa mamlaka juu ya mataifa: naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.. kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu" (Uf. 2: 26,27).

Kristo na mahubiri yake ya mfano wa fedha sasa unaingia mahala - watumwa waaminifu walipewa zawadi ya kutawala miji kumi au mitano katika ufalme (Luk. 19: 12 -19). Maarifa ya njia za Mungu hayataenea haraka Kristo akisemwa kuwa ni mfalme mjini Yerusalemu; Watu watasafiri kwenda Yerusalemu kwa ajili ya kujipatia elimu kuhusu Mungu (Isa. 2: 2,3). kumbuka,pia, mlima uliotajwa katika Dan. 2: 35, 44 (maana yake ufalme wa Mungu) pole pole unaenea juu ya dunia. Litakuwa ni jukumu la watakatifu kueneza maarifa ya Mungu na kwa hiyo ufalme wake. Israeli ulipokuwa ni ufalme wa Mungu awali, jukumu la makuhani lilikuwa ni kufunza watu wapate kumjua Mungu (Malaki 2:5 -7). kwa kusudi hili waliwekwa katika miji mbali mbali ya Israeli yote. Utakapowekwa tena ufalme wa Mungu wenye utukufu zaidi, watakatifu wataingia mahali pa kazi ya makuhani (Uf. 5:10).

Kristo akija Leo:

  1. Wafu wanaotakiwa kutoa habari watafufuliwa, pamoja na watu walio hai, watachukuliwa kwenda mbele ya kiti cha hukumu .

  2. Wawajibikaji wabaya wataadhibiwa kwa mauti, na wenye haki watapewa uzima wa milele. Hukumu pia itatolewa kwa mataifa yanayo mpinga Kristo .

  3. Watu wenye haki wakati huo watawatawala watu ambao wakati huo watakuwa hai, Lakini ambao hawawajibiki kwa Mungu sivyo; Watafundishwa Injili wao wakiwa ni "Wafalme na Makuhani"(Uf. 5:10)

  4. Ufalme utadumu kwa miaka 1000. Wakati wa kipindi hiki watu wote wenye kupatwa na mauti wataisikia injili na kwa hiyo kuwa na wajibu kwa Mungu. Watu hawa wataishi kwa muda mrefu zaidi kwa maisha ya furaha .

  5. Mwisho wa Kikwi kutatokea uasi juu ya Kristo na watakatifu, Uasi huo Mungu atauweka chini (Uf. 20: 8,9).

  6. Mwisho wa miaka 1000, wote waliokufa wakati wa kipindi hicho watafufuliwa na kuhukumiwa (Uf. 20: 5,11 -15).

  7. Wabaya miongoni mwao wataharibiwa, na watu wenye haki wataungana nasi kuwa na uzima wa milele.

Kusudi la Mungu kwa dunia wakati huo litakamilika. Itajawa na watu wenye haki wasiokufa. Jina la Mungu 'Yahweh Elohim’ - Hili jina katika kiswahili limeandikwa YAHU ELOI (lina maana'Yeye atakayedhihirika katika kundi la wenye nguvu’) wakati huo litatimia. Dhambi na mauti havitaonekana tena duniani; ahadi ya kwmba uzao wa nyoka utaharibiwa kabisa kwa kupondwa kichwa, wakati itatimia kwa ukamilifu (Mwa. 3:15). Wakati wa Kikwi Kristo yampasa amiliki "hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayeondoshwa ni mauti ….. Basi , vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake (Mungu) aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote" (1 Kor. 15: 25 -28).

Hapo ndipo"Mwisho, (Kristo) atakapompa Mungu Baba ufalme wake"(1Kor. 15:24) Kitakachofuata kwa kipindi hiki Mungu atakapokuwa"yote katika wote" hatujaambiwa; yote tunayojua ni kuwa kutakuwa na uzima wa milele, mwili wa Uungu, na kuishi kwa kumtukuza na kumpendeza Mungu. Ni ufedhuli kuuliza zaidi hali ya baada ya Kikwi itakuwaje.

Kufahamu "Injli ya ufalme wa Mungu" ni muhimu kwa wokovu wa kila msomaji wa maneno haya. Tunakuomba usome tena somo hili kisha utazame mafungu ya maneno yaliyonukuliwa.

Mungu anatutaka tuwemo katika ufalme wake. Kusudi lake lote lilipangwa kwa ajili yetu kuwa na sehemu ya kweli , kuliko kueleza tu, uweza wake wa uumbaji. Ubatizo unatuhusisha na ahadi zinazohusu ufalme huu. Ni shida kuamini kwamba ubatizo, unaofuatiwa na miaka michache ya kunyenyekea kumtii Mungu na neno lake, kunaweza kutupatia kuingia kwenye enzi zenye utukufu huo. Lakini imani yetu kwa upendo mpana wa Mungu inatakiwa iwe thabiti. Matatizo yetu yoyote ya muda mfupi, hakika hatuna sababu za kupinga mwito wa Injili .

"Mungu akiwapos upande wetu, nani aliye juu yetu ?"(Rum. 8:31).

"Mateso ya wakati huu wa sasa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu" (Rum. 8:18).

"Dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi"(2 Kor. 4:17).


  Back
Home
Next