Misingi Ya BIBLIA
Somo La 5: Ufalme wa Mungu
Kuelezea wazi kabisa Kuhusu Ufalme | Kwa Sasa Ufalme Haujasimikwa | Ufalme wa Mungu uliopita | Ufalme wa Mungu kwa Wakati Ujao | Miaka Elfu - Kikwi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Ufalme wenyewe, Maelezo mafupi ya Historia ya Israeli) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 15: Ufalme wenyewe

Maelezo yenyewe kabisa ya ufalme yanayopatikana katika manabii wa Agano la Kale mara nyingi wameyakejeli wanatheologia na washirika wengi wa madhehebu. Imedaiwa kwamba Lugha ni ya mifano ya maeneo mengine ya kupewa dhawabu kuliko duniani, kwa kuwa sayari hii yaelekea kuchomwa moto.

Kwa kujibu hili, inabidi ieleweke kwamba kanuni ya kufundisha somo la Biblia ni kuwa siku zote tuichukulie Biblia ilivyoandikwa isipokuwa ikiwepo sababu nzuri ya kuweka tafsiri ya kiroho. Mathalani, mstari wa kwanza wa kitabu cha ufunuo unatujulisha ya kuwa maono kwa upana yameandikwa kwa ishara - Lakini sio katika Biblia ya kiswahili, Huu mstari haujaandikwa kama ni kwa ishara ila Biblia ya kiingereza ya K.J.V (Uf. 1:1), huu unaweza kutuongoza kwa mtazamo wetu. Pia ipo maana moja nzuri na ya kuwa kweli kwa kutumia Lugha ambayo inaweza kuonyesha ikiwa au hapana maneno yasisomwe kwa ishara. Hivyo tunaposoma dunia inalewa -lewa kama mlevi (Isa. 24: 20), Kutokana na kuonekana wazi aina ya lugha iliyotumika hiyo tunakusudia kuisoma kimfano. Kwa utofauti, Lugha iliyotumika kuelezea ufalme ujao ni rahisi sana kufahamu kwa maneno halisi; hakuna fununu kwamba tusome mfano.

Inaonekana kwamba kwa ajili ya watu kutoweza kuipata imani ya kutosha kuamini kwamba muda huu kwa kweli utakuja hapa duniani, wamevumbua nadharia zinazoelezea mbali. Uchaguzi wao wa kiroho, au ufalme ambao upo mbinguni, si dhahiri na unakosa maelezo, kwa hiyo ni kidogo kuamini, na imani kidogo aidha inatakiwa au kutumainishwa. Kama kweli maelezo ya watu walemavu wataponywa au nyika zitafanywa kuwa na rutuba , ni mifano ya ishara tu, basi swali hili inabidi kwa namna yake maalum na kwa kusadikika lijibiwe: Ishara za kitu gani ? Mafungu haya ya maneno yanaelezea ufalme wa Mungu. ikiwa hatuna uhakika hasa Ishara ni za nini, basi hatuijui Injili ('habari njema’) kuhusu ufalme wa Mungu, na kwa hiyo hatuwezi kuwa na tumaini lolote ndani yake.

Juu ya hayo, itakuwa wazi kabisa toka ushahidi wote ulioonyeshwa mpaka hapa, ya kwamba Mungu analo kusudi la milele na wanadamu juu ya dunia hii. Haitaangamizwa sayari ambayo alimwahidi Abrahamu na uzao wake milele. Kwa hiyo tunangoja hapo kuwa maelezo halisi yaliyomo ndani ya Biblia ya ufalme unaokuja juu ya dunia.

Mafungu ya maneno yafuatayo yanathibitisha hili: -

  • "Yeye ni Mungu aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba (ya bure) ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu" (Isa. 45:18). kuumbwa kwa dunia kungekuwa hakufai ikiwa Mungu ataiharibu; bali, ni namna nyingine, kwani kusudi la Mungu ni kuwa ikaliwe na watu wasioharibika.

  • "Dunia hudumu daima" (Muhubiri 1: 4).

  • "Amevithibitisha (mpangilio wa asili wa sayari zote kulizunguka jua) hata milele na milele: Ametoa amri wala haitapita" (Zab. 148:6).

Muda wa Kikwi kwa miaka 1000, kama ilivyoandikwa katika Uf. 20:4, ikubalike kwa maneno yalivyo, ili kuoanisha na maneno mengine katika manabii kuhusu kawaida ya kipindi hiki. Hata katika ufunuo, sio kila tarakimu ipasayo ichukuliwe kimfano. Ushahidi mwingi ndani yake kwa"theluthi" ni mifano iliyo wazi. Kwa maana zaidi Kikwi imeelezewa katika Waebrania 4: 4-9 kuwa ni siku ya sabato ya kupumzika. Kwa Mungu "siku ni sawa na miaka elfu" (2Pet. 3:8).Baada ya 'Siku’ sita za miaka elfu katika mpango wa Mungu na dunia, itafika'Siku’ ya sabato ya Kikwi.

Kulingana na kalenda ya Biblia ya uumbaji, miaka 6000 (yaani,'Siku’ 6) toka uumbaji tunafikishwa 2000 B.K (yaani - uumbaji ulikuwa karibu 4000 K.K.). Hapa panaweza kuwa na maana kwamba mwanzo wa Kikwi itakuwa karibu na 2000 B.K. Kwetu sote, muda umefika upeo. Tukiwa tunakabiliwa na matumaini ya Kristo kurejea mapema, twahitajika tutumie kila nafasi inayowezekana katika maisha haya mafupi kujiweka tayari kwa ujio wake.


  Back
Home
Next