Misingi Ya BIBLIA
Somo La 5: Ufalme wa Mungu
Kuelezea wazi kabisa Kuhusu Ufalme | Kwa Sasa Ufalme Haujasimikwa | Ufalme wa Mungu uliopita | Ufalme wa Mungu kwa Wakati Ujao | Miaka Elfu - Kikwi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Ufalme wenyewe, Maelezo mafupi ya Historia ya Israeli) | Maswali

5.3 Ufalme wa Mungu uliopita

Ufalme wa Mungu ujao ni thawabu ya waaminio, Ikiwa hii , ni kusudi lao kuishi maisha ya kujitoa kuiga mfano wa Kristo - jambo fulani linalohusishwa maumivu ya muhula mfupi pamoja na kutokuwa na faraja. kwa hiyo inategemewa kuwa siku zao zote zitatumiwa na nia kubwa inayoongezeka kushukuru na kuelewa ajabu za enzi ijayo. Itakuwa ni nyongeza ya jitihada zao zote kiroho, na azimio kamili kwa Mungu ambaye wamependa akiwa ni Baba yao.

Maandiko yamejaa tele na maelezo jinsi ufalme utakavyokuwa, na utakuta ni kazi ya muda ya maisha kuvumbua baadhi yake. Njia moja inayoweza kutuletea kuelewa mambo mengine makuu ya msingi ya ufalme huu ujao ni kukubali kuwa ufalme wa Mungu uliwahi kuwepo zamani kwa namna ya taifa la Israeli. Ufalme huu utaanzishwa tena Kristo akirudi. Mengi ya Biblia yanatupatia habari kuhusu taifa la Israeli, ili tuelewe kwa maelezo marefu, jinsi ufalme wa Mungu ujao utakavyotengenezwa. Mara nyingi Mungu amejieleza kuwa Yeye ni "Mfalme wa Israeli" (Isa. 44: 6 ml. Isa. 41: 27; 43: 15; Zab.48:2; 89:18; 149:2); kinachofuata ni kwamba watu wa Israeli walikuwa ni ufalme wake, walianza kuwa ufalme wa Mungu kwa kuingia katika Agano naye chini ya mlima Sinai, muda mfupi walipotoka Misri kwa kupitia Bahari ya Shamu.

Kwa kuitikia kwa hiari yao kutunza Agano hili, watakuwa "Kwa (Mungu) ufalme …… na taifa takatifu"(Kut. 19:5,6). Hivyo,"Israeli alipotoka Misri …. Israeli (alikuwa) miliki yake" au ufalme (Zab. 114:1,2).Baada ya kuingia katika mkataba huu, Israeli akasafiri kupitia jangwa la Sinai na akaja kuweka makao katika nchi ya Ahadi -Kanaani. Mungu akiwa ni mfalme wao, mambo yao yaliamliwa na"Waamuzi"(K.m Gideon na Samsoni) sio wafalme. Hawa waamuzi hawakuwa wafalme, bali waliongozwa na wasimamizi wa Mungu wakiwa magavana wa sehemu moja ya nchi sio kutawala nchi yote. Mara nyingi waliinuliwa na Mungu kwa dhumni maalumu. k.m kuongoza wana - Israeli kutubu na kuwaokoa toka maadui wao. Wana Israeli walipomwuliza mwamuzi Gideoni ili awe mfalme wao, aliwajibu,"Mimi sitatawala juu yenu …. Yeye Bwana atatawala juu yenu" (Amosi 8:23).

Mwamuzi wa mwisho alikuwa Samweli . Katika kipindi chake wana - Israeli waliomba wawe na mfalme binadamu ili wawe kama mataifa mengine yanayozunguka (Sam.8: 5, 6). Katikati ya historia nzima, watu wa kweli wa Mungu wamejaribu kupima kidogo sana ukaribu na uhusiano wao kwa Mungu, na kutoa dhabihu hii kwa sura yenye mfano mmoja na ulimwengu uliowazunguka. Majaribu haya ni makali zaidi ulimwengu huu wetu uliopo . Mungu alisikitika kwa Samweli:"Wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao"(1Sam. 8:7). Ingawa hivyo, Mungu aliwapa Wafalme, wakaanza na kuwa na Sauli mbaya, Baada yake akafuata Daudi mwenye haki, mstari mzima wa ufalme umeshuka toka kwake. Wafalme wenye nia ya roho zaidi walitambua kuwa Israeli bado walikuwa ni ufalme wa Mungu hata kama walimkataa kuwa mfalme. Kwa sababu hii waligundua kwamba walikuwa watawala juu ya Israeli kwa niaba ya Mungu sio kwa Haki yao.

Tunapolielewa jambo hili linatuwezesha kutafakari maelezo ya Suleimani, mwana wa Daudi, alipotawala juu ya "Kiti cha enzi cha Mungu, kuwa mfalme wake Bwana, Mungu wako" (2 M/Nyak. 9: 8; 1 M/nyak. 28:5; 29:23). Utawala wa Suleimani wa amani na ustawi ulionyesha mbele (au ulikuwa ni 'mfano’ wa) Ufalme ujao wa Mungu. Hii ndio sababu imetiwa mkazo kwamba akawa mfalme juu ya Israeli badala ya Mungu, Kama Yesu naye atakavyoketi juu ya kiti cha enzi cha Mungu akiwa mfalme wa Israeli kwa ajili ya Mungu (Mat 27: 37, 42; Yn. 1:49; 12:13).

Wengi wa wafalme wenye haki walioorodheshwa kwenye Agano la Kale walifurahia tawala zilizokuwa ni mfano wa ufalme ujao wa Kristo. Hivyo kama Suleimani alivyojenga hekalu la Mugnu Yerusalemu, basi pia, Kristo atafanya hivyo katika ufalme ujao (ona Ezek. 40 -48). Kama Ezekia na Suleimani walivyopokea kodi na vipawa toka mataifa yaliyowazunguka. (1Fal.10: 1-4; 2 Fal. 20: 12). na kuona nchi ya Israeli ikibarikiwa kwa rutuba ya kushangaza na ustawi (1Fal. 10: 5-15; Isa. 37: 30), hivyo katika ufalme wa Kristo utakaokuwa wa ulimwengu wote mambo hayo hayo yataonekana kwa kipimo chenye mapana zaidi.

NDOA

Mbali na Suleimani kuanza vyema, wakati bado kabisa akingali kijana alifanya makosa ya mintarafu ya ndoa ambayo kwa kuyaendekeza yalinyonya nguvu zake za kiroho alipozeeka. "Mfalme Suleimani akawapenda wanawake wengi wageni …… wanawake wa moabu, na wa Waamoni, na Waedomi …. Na wa mataifa Bwana alivyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu: kwa kuwa hakika watageuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Suleimani akaambatana nao kwa kuwapenda …. Wake zake wakamgeuza moyo wake. maana ikawa Suleimani alipokuwa mzee, Wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, ….. Suleimani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana,wala hakumfuata Bwana akamghadhibikia Suleimani …. Kwa hiyo Bwana akamwambia …. Hakika nitaurarua ufalme usiwe wako" (1Fal. 11: 1 -11).

Kuteleza na kuiacha imani Suleimani kulidumu maisha . Uhusiano wake na wanawake ambao hawakushiriki maarifa yake kwa Mungu wa Israeli kulimwongoza kuwa na uhusiano wa kuielekea miungu yao ya uongo. Upendo wake kwa wake zake ilimaanisha hakuona tena miungu hii inamkengeusha kiroho toka kwa Mungu wa kweli ambapo ndivyo ilikuwa. Kadri muda ulivyosonga mbele , moyo wake haukumwabudu tena Mungu wa Israeli."Moyo wake haukutimilika"yaani, dhamira yake haikumchoma tena kuabudu miungu inayodanganya. kukosa moyo wake wote kujitoa kwa Mungu wa kweli "ukawa ni uovu machoni pa Bwana"ikasababisha Mungu kuvunja uhusiano na Suleimani. Israeli waliambiwa mara kwa mara wasioane na wanawake wa mataifa yanayowazunguka (Kut. 34: 12 -16; Yoshua. 23: 12, 13; K/Torati 7:3).

Kwa kubatizwa katika Kristo kiroho tunakuwa Israeli, kama hatujaoa, tuoe tu ndani ya Israeli kiroho,"Katika Bwana" (1Kor. 7:39) - yaani, mwamini mwingine aliyebatizwa 'Katika Kristo’ Ikiwa tayari tumeoa wakati tunabatizwa, tusitengane na wake zetu; uhusiano wetu wa ndoa unatakaswa kwa sababu ya imani yetu (1Kor. 7: 12 -14). Kwa kufahamu, kuchagua kuoa wale ambao hawamjui Mungu wa kweli, kwa muda mrefu, watatuongoza kwenye ukengeufu wetu. Solomoni ni dhahiri alishindwa kukubali onyo la nguvu za Mungu kuhusu wanawake hawa:"Hakika wataugeuza moyo wako"(1Fal. 11: 2; Kut. 34: 16). Usawa pekee wa ajabu wa kujiweza na nguvu ya mawazo ya toba inaweza kutufanya tusihesabiwe na amri hii .

Awali tumeonyesha jinsi huo Ukristo wa orthodox haukubali msingi wa Wayahudi ambao ni tumaini la mkristo; hawamjui Mungu wa kweli wa Israeli. Kuoana na watu hawa wasiomjua Mungu kutatupeleka pole pole kutofautiana na utukufu wenye kweli ya mafunzo ambayo ni msingi wa wokovu wetu. Kwa sababu hii Isaka na Yakobo walikwenda umbali wa ajabu kuoa wanawake ambao waliishika imani ya kweili vema, Isaka akasubiri mpaka alipofikia umri wa miaka 40 ili kupata mke anayefaa (Mwa. 24: 3, 4; 28: 1). Sababu iliyoleta huzuni kwa Ezra na Nehemia waliposikia ya kuwa Wayahudi wengine walioa wasio wayahudi zaidi inaonyesha ukubwa wa toleo hili (Ezra. 9:12; Nehemia 10: 29, 30).Tumeleta jambo hili kwenye hatua hii ili kusaidia kufikiri kwa kuangalia; ndoa imejadiliwa kwa maelezo zaidi katika somo la 11.4.

HUKUMU YA MUNGU

Yakiwa ni matokeo ya kukengeuka Suleimani, Ufalme wa Israeli ukagawanyika na kuwa falme mbili; mwanae Suleimani,Rehoboamu, akatawala juu ya kabila ya Yuda, Benjamini na nusu ya kabila la Manase, wakati Yeroboamu akatawala juu ya kabila zingine kumi. Huu ufalme wa kabila kumi uliitwa Isrraeli,au Efraimu, ambapo makabila mawili yaliitwa Yuda. Watu wote wa kabila hizi kwa sehemu kubwa walifuata mfano mbaya wa Suleimani - walidai kumwamini Mungu wa kweli, wakati huo huo wakiendelea kuziabudu sanamu za mataifa waliowazunguka. Mara kwa mara Mungu aliwasihi, kwa njia ya manabii, ili watubu, bali haikufaa. Kwa sababu hii akawaadhibu kwa kuwatoa kwenda nje ya ufalme wa Israeli waingie nchi za adui zao. Hii ilikuwa kwa waashuri na wakaldayo wakiihusuru Israeli na kutwaa mateka. "Miaka mingi (Mungu) akachukuliana nao, nawe ukawashuhudia kwa roho yako (neno) kwa vinywa vya manabii wako: (bali) wao wasitake kusikiliza; kwa hiyo ukawatia katika mikono ya watu wa nchi (zilizowazunguka)"Nehemia 9:30.

Kabila kumi, ufalme wa Israeli, haukuwa na wafalme wazuri hata kidogo. Yeroboam, Ahazi, Yehoahazi n.k wote wameandikwa taarifa zao katika kitabu cha wafalme wakiwa ni waabuduo sanamu. Mfalme wao alikuwa Hoshea, kipindi cha utawala wake Israeli walipopigwa na waashuri, nao kabila kumi wakachukuliwa utumwani (2 Fal. 17). kutokana na hii hawakurudi kamwe .

Ufalme wa Yuda wenye kabila mbili ulikuwa na baadhi ya wafalme wazuri (k.m Hezekia na Yosia), ingawa walio wengi walikuwa waovu. Kwa ajili ya watu kurudia -rudia kutenda dhambi, Mungu akaupindua ufalme wa Yuda katika kipindi cha utawala wa mfalme wao wa mwisho, Sedekia. Hsii ilitokana na wao kuvamiwa na wakaldayo , waliowachukua kwenda utumwani Babeli (2 Fal. 25) Walibakia Babeli kwa miaka 70, Wengine wakarudi baadae Israeli chini ya uongozi wa Ezra na Nehemia. hawakuwa tena na mfalme wao, walipokuja tawaliwa na wakaldayo, wayunani na warumi. Yesu alizaliwa wakati wa kipindi cha utawala wa Warumi. Kwa sababu ya Israeli kumkataa Yesu, Waroma wakawavamia mwaka 70 B.K na kuwatawanya ulimwenguni pote. Ni miaka 100 tu iliyopita walianza kurudi, hii ni ishara inaonya kurudi kwa Kristo

{ Ona kilichotiwa mwishoni mwa kitabu sehemu ya 3 }

{ nyongeza iliyotiwa mwishoni mwa kitabu}.

Ezekieli 21: 25 -27 mistari hii ilitabiri mwisho wa ufalme huu wa Mungu kama ulivyoonekana katika taifa la Israeli: "Na wewe, Ewe mtu mwovu, uliyetiwa jeraha kiasi cha kuwa , Mkuu wa Israeli (yaani, Sedekia), ambayo siku yako imekuja ….. Bwana MUNGU asema hivi; Kiondoe kilemba, ivue taji; (yaani Sedekia atakoma kuwa mfalme) haya hayatakuwa tena kama yalivyo; …… Nitakipindua, hiki nacho Nitakipindua, Nitakipindua, hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa"Maneno baada ya maneno kwa manabii wanaohuzunikia kukomeshwa kwa ufalme wa Mungu (Hos.10: 3; Omb. 5:16; Yer. 14:12; Dan. 8: 12 -14).

‘Kupindua’ mara tatu iliyo katika Ezekiel 21: 25 -27 unatajwa uvamizi uliofanywa mara tatu na Nebukadneza, mfalme wa Babeli. Mwanafunzi anayekesha ataona katika mistari hii mfano mwingine wa jinsi ufalme wa Mungu na mfalme wake anaweza kutendwa sawa; Kuangushwa kwa Sedekia ulikuwa huo ufalme wa Mungu (ona sehemu ya 5:2). Hivyo ufalme wa Mungu kama ulivyokuwa katika taifa la Israeli ulifika mwisho: "….. na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli"(Hos. 1:4), "Hiki nacho hakitakuwa tena , hata …."Inaleta kidokezo kwamba ufalme utaanza tena hapo"atakapokuja ambaye ni haki yake; naye (Mungu) atampa". Mungu atampa (Yesu) kiti cha enzi cha Daudi Baba yake ….. na ufalme wake hautakuwa na mwisho"(Luk. 1: 32, 33) -Kristo akirudi. Basi, hii ni hapo ahadi ya kurudishwa ufalme itakapotimizwa.

KUTENGENEZWA KWA ISRAELI

Lipo jambo kubwa lililoandikwa katika Agano la Kale lote na manabii la kurudishwa ufalme wa Mungu akirudi masihi.Wafuasi wa Kristo walielewa vema hili:"Basi walipokutanika, wakamuuliza, wakisema, Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme ?"yaani, 'Unabii wa Ezekieli 21:27 utatimia sasa ?’ Yesu alijibu kwa kusema kuwa muda hasa wa yeye kuja mara ya pili hawata ujua, Ingawa malaika haraka baadaye waliwahakikishia kuwa atarudi wakati fulani (Matendo. 1: 6 -11).

Kutengenezwa ufalme wa Mungu / Israeli kutakuwa basi akirudi mara ya pili. Hivi Petro alihubiri ya kuwa Mungu atamtuma "Yesu Kristo …….. ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni (yaani, asalie kule) hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu"(mdo. 3:20,12). Kuja mara ya pili kutafanya uanzishwe tena ufalme wa Mungu kama kutengeneza tena ufalme wa Israeli wa zamani.

Kwa kweli kutengeneza tena ufalme wa Mungu ni msemo wa"Manabii wote watakatifu wa (Mungu)":-

  • "Kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema: na mmoja (Yesu) ataketi juu yake katika kweli, katika hema ya Daudi (akija mara ya pili - Luk. 32,33), akifanya hukumu …… mwepesi wa kutenda haki"(Isa. 16:5).

  • "Siku hiyo nitainua tena masikani ya Daudi yaliyoanguka (yaani, kiti cha enzi cha Daudi kilichosemwa na Luk.1: 32,33), na kuziba mahala palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale"(Amosi. 9:11 . Fungu la mwisho la maneno ni Lugha iliyowazi ya kutengeneza tena.

  • "Watoto (Israeli) wao nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu" (Yer. 30:20) .

  • "Bwana atachagua Yerusalemu tena"(Ezek. 2:12), atafanya mji mkuu kwa ufalme wake wa ulimwengu wote (Zab. 48:2; Isa. 2:2 -4).

  • "Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda na wafungwa wa Israeli, na kuwajenga kama kwanza ……. Itasikika tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe ……. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi kama kwanza ….. katika mahali hapa (Yerusalemu) ….. yatakuwepo makao ya wachungaji …. Makundi ya kondoo yatapita"(Yerusalemu 33: 7 -13).

Kurudi kwa Kristo kuanzisha huu ufalme kwa kweli ni "tumaini la Israeli", ambalo yatupasa tujihusishe kwa kubatizwa.


  Back
Home
Next