Misingi Ya BIBLIA
Somo La 5: Ufalme wa Mungu
Kuelezea wazi kabisa Kuhusu Ufalme | Kwa Sasa Ufalme Haujasimikwa | Ufalme wa Mungu uliopita | Ufalme wa Mungu kwa Wakati Ujao | Miaka Elfu - Kikwi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Ufalme wenyewe, Maelezo mafupi ya Historia ya Israeli) | Maswali

5.4 Ufalme wa Mungu kwa Wakati Ujao

Sehemu ya 1 na 3 ya somo hili zimetoa habari kiasi cha kutosha kuhusu jinsi huu ufalme utakavyokuwa. Tumeona kuwa Abrahamu aliahidiwa kwamba kwa njia ya mzao wake watu toka maeneo yote ya ulimwengu watabarikiwa; Rum.4: 13 inapanua suala hili kuwa na maana ya kuwa Dunia yote itakaliwa na hao watu ambao wamo'Katika’ Uzao wa Abrahamu, yaani Kristo. Unabii ulio katika sanamu ya Dan. 2 waeleza Kristo atakavyorudi kama jiwe dogo, na kisha pole pole ufalme utapanuka na kuwa wa ulimwengu wote (Zab.72:8). Hii inamaana ya kwamba ufalme wa Mungu hautakuwa eneo la Yerusalemu pekee au katika nchi ya Israeli , kama wengine wanavyosema, kama maeneo haya hakika yatakuwa maeneo yake makuu. Wanaomfuata Kristo katika maeneo haya watakuwa"Wafalme na makuhani; tutatawala dunia"(Uf. 5:10). Tutakuwa wasimamizi juu ya makazi ya watu ya ukubwa mbali mbali na idadi; mmoja atakuwa juu ya miji kumi, na mwingine juu ya mitano (Luk. 19:17). Kristo atashiriki utawala wake pamoja nasi (uf. 2:27; 2 Tim 2:12)."Mfalme (Yesu) atamiliki kwa haki, na wakuu (Waaminio) wake watatawala kwa hukumu" (Isa. 32:1; Zab. 45: 16).

Kristo atamiliki milele katika kiti cha enzi cha Daudi kitakachokuwa kimewekwa tena (Luk. 1: 32, 33), yaani, atakuwa na mahali pa Daudi na cheo cha utawala, kilichokuwa Yerusalemu. Ikiwa Kristo atamiliki tokea Yerusalmeu, Huu utakuwa ni mji mkuu wa ufalme ujao. ni kwenye eneo hili ambapo hekalu litajengwa (Ezek. 40 -48). Wakati watu watamtukuza Mungu sehemu mbali mbali za ulimwengu wote (Malaki. 1:11), Hekalu hili litakuwa kitovu cha ibada walimwengu. Mataifa"watakwea mwaka baada ya mwaka ili kumwabudu mfalme, Bwana wa majeshi, na k ushika sikukuu ya vibanda"kuzunguka hekalu katika mji wa Yerusalemu (Zekaria 14:16). Hii hija ya mwaka kwenda Yerusalemu pia imetabiriwa kwa Isa. 2: 2,3) "Katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana (Ufalme- Dan.2:35,44) wa nyumba ya Bwana (Hekalu) utawekwa imara juu ya mlima (yaani, ufalme wa Mungu na hekalu vitawekwa juu ya falme zetu) ….. na mataifa yote watauendea makundi makundi Na mataifa wengi watakwenda na kusema, Njooni twendeni juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atafundisha njia zake, ….. maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu" Hii inaonekana kuwa picha ya siku za kwanza za ufalme, watu walipotangaza maarifa ya miliki ya Kristo kwa wengine, na watu wanakwenda juu "Mlimani"wenye ufalme wa Mungu, ambao utaene taratibu ulimwenguni pote. Hapa tuna picha ya shauku ya kweli katika ibada ya dini .

Moja ya mambo makubwa yaletayo huzuni kwa mwanadamu wa siku zetu ni kwamba watu'humwbudu’ Mungu kwa siasa, kwa makundi kukaa pamoja , kwa mazoea au kwa hangaiko la moyo, kuliko juu ya msingi wa ufahamu wa kweli kwake akiwa ni Baba yao na muumba. Katika Ufalme kutakuwepo shauku ulimwenguni pote ya kujifunza njia za Mungu; watu watakuwa na nia ya kusudi sana kusafiri toka miisho yote ya Dunia kwenda Yerusalemu ili kupata elimu ya Mungu zaidi. Badala ya chafuko na utaratibu wa kuhusiana na binadamu usio na haki na utawala wa haki, kutakuwa na kanuni moja ya sheria"Sheria na neno la Bwana"Vitatamkwa na Kristo toka Yerusalemu."Mataifa yote yatakwenda makundi makundi"kwenye vipindi vya mafunzo haya, yanadokeza kuwa hii nia ya watu wote kutafuta elimu ya kweli juu ya Mungu itapunguza mabishano yaliyozaliwa nayo kati ya mataifa, kama yafanyavyo kati ya mtu na mmoja mmoja wanaojitoa wenyewe kujipatia elimu kama hii katika maisha haya.

Namna hii ya mataifa kufurika katika mji wa Yerusalemu ni moja na picha inayoonyesha katika Isa. 60: 5, ambapo Wayahudi "Wanakwenda pamoja"na watu wa mataifa (wasio wayahudi) kumwabudu Mungu katika mji wa Yerusalemu. Habari hii inaungana kikamilifu na unabii ulio katika Zekaria. 8: 20 -23: -

"Itatokea halafu ya kwamba watakuja mataifa na wenyeji wa miji mingi; wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya ! twendeni zetu kwa haraka (Zek. 14: 16 mwaka kwa mwaka) tuombe fadhili za Bwana , na kumtafuta Bwana wa majeshi; mimi nami nitakwenda. Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta Bwana ….. watu kumi, wa Lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; Naam, wataushika wakisema, tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi"

Hii inaumba picha ya watu wa Uyahudi kufanywa"Kichwa na sio mkia" wa mataifa, kwa ajili ya kutubu kwao na utiifu (K/Torati 28:13);Mpango wa Mungu kwa Wayahudi wa wokovu wakati huo utakubalika na kila mtu. Kutokujua huku miongoni mwa Wakristo wa wakati ule ule basi utafikia mwisho mara moja. Wakati huo watu kwa shauku watajadili mambo haya. Kwa kusudi kwamba waweze kuwaambia wayahudi,"tumesikia ya kwamba Mungu yu pamoja nanyi". Mazungumzo yatakuwa mambo ya kiroho wakati huo, kuliko mizuka inayojaa fikira za ulimwengu uliopo.

Kutolewa sharti kubwa kwa utauwa, halishangazi kuwa Kristo "atafanya hukumu katika mataifa mengi, ….Nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe minundu: Taifa halitainua upanga juu ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe"(Isa. 2:4).

Mamlaka kamili ya Kristo na haki kabisa ya ushupavu wake katika mabishano utasababisha mataifa kwa hiari kubadili zana za kijeshi na kuwa vyombo vya kilimo na kuacha mafundisho yote ya kijeshi. "Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi" (Zab. 72:7). Kwa kiroho wakati huo atakuwa na hali ya juu, na heshima watapewa walio na sifa ya upendo wa Mungu, huruma na haki. Ni tofauti na wakati uliopo wa kuwa juu wenye kiburi, wenye kujidai na wachoyo wenye tamaa ya kuwa maarufu.

Hiari ya kufua"Mapanga kuwa majembe"itakuwa sana sehemu kubwa ya mabadiliko kwa kilimo kitakachokuja duniani, kwa toleo la dhambi ya Adamu, ardhi ililaaniwa kwa ajili yake (Mwa. 3: 17 -19), pamoja na matokeo ya jitihada kubwa inatakiwa kwa sasa ili kupata chakula. Katika ufalme wa Mungu"utakuwepo wingi wa nafaka katika ardhi juu ya milima - yaani sehemu kame; na matunda yake yatawaya -waya kama (mazao) Lebanoni"(Zab. 72:16)."Alimaye atamfikilia avunae,naye akanyagae zabibu atamfikilia apandae mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu"(Amosi. 9:13), ndivyo ardhi itakuza hali ya uzaaji, na kupunguza laana iliyotamkwa Edeni juu ya ardhi

Bidii hii kubwa kwa kilimo itahusisha watu wengi. Unabii na ufalme unatoa fikira ya kuwa watu watarejea kujitosheleza, kwa mtindo wa maisha ya kulima: -

"Wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, chini ya mtini wake; wala hakuna mtu atakayewatia hofu" (Mika. 4:4)

Huku kujitosheleza kutashinda matumizi mabaya yaliyo ndani ya mfumo wowote wa ajira ya kazi kwa ajili ya kupata pesa. Kutumia maisha yote kufanya kazi ya kuwafanya watu wengine watajirike wakati huo itakuwa ni jambo lililopita.

"Watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu na kula matunda yake. Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine …. Wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi. Hawatajitaabisha kwa kazi bure ……"(Isa. 65: 21 -23).

Isaya 35: 1 -7 ina unabii usio na kifani jinsi nchi kame itakavyobadilika, ikisababisha kuwa katika hali ya shangwe na kufurahisha karibu ikitiririka toka kwenye nchi, kwa sababu ya kuwa na raha na zaidi maisha ya kiroho kwa wale watendaji : "Nyika …. Pata furahi ….. jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. Litachanua … na kufurahi , naam, kwa shangwe na kuimba …….. maana katika nyika maji yatabubujika, na vijito jangwani. Na mchanga ung’aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji na nchi yenye kiu itakuwa chemi chemi za maji". Hata tendo la asili la kushambuliana kati ya wanyama litaondolewa:"mbwa mwitu na mwana kondoo watalisha pamoja", na watoto wataweza kucheza na nyoka (Isa. 65:25; 11: 6 - 8).

Kwa njia hiyo hiyo Laana iliyowekwa juu ya wanyama kwa ukubwa itapunguzwa, Hivyo na tokeo lililowekwa juu ya wanadamu nalo pia litapunguka.Ufu. 20: 2,3 inasema hivi kwa lugha ya ishara ya Ibilisi (dhambi na matokeo yake) "Kufungwa"au kuzuiwa, kwa kipindi cha millenia yaani miaka elfu. Maisha ya kuishi yataongezeka, hivyo basi mtu akifa mwenye miaka 100, atadhaniwa bali kuwa ni mtoto (Isa. 65:20) Wanawake watapata uchungu mdogo wakati wa kujifungua mtoto (mst. 23). "Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na viziwi masikio yao yatazibuliwa. Mtu aliye kilema ataruka -ruka kama ndama, na ulimi wake aliye bubu utaimba" (Isa. 35: 5,6). Hii itakuwa kwa sababu ya kuwepo vipawa vya Roho (Ebra. 6:5).

Ufalme waMungu kwa nguvu hauwezi kukaziwa mno kama kuonekana kama kisiwa chenye joto jingi peponi, ambacho watu wenye haki watafurahia kwa namna hii watu wanavyofurahia kuota jua baada ya kuogelea katikati ya kujivunia maumbile. Kusudi la msingi wa Ufalme wa Mungu ni kutoa utukufu kwa Mungu, hata dunia itajawa na utukufu wake"Kama maji yaifunikavyo bahari" (Habakuki 2:14). Hii ni shabaha aliyokuwa nayo Mungu tangu asili:"Kama niishivyo, dunia nzima itajaa utukufu wa Bwana" (Hes. 14: 21). Utukufu kwa Mungu maana yake ni kwamba wakaazi wa dunia watatoa shukrani, Sifa na mfano ulio kiini cha tabia yake; kwa kuwa ulimwengu utakuwa katika hali hii, Mungu atafanya nayo dunia inayoonekana itoe utukufu pia. Hivyo"Wapole watairithi nchi (Katika ufalme wa Mungu) Watajifurahisha kwa wingi wa amani (ya kiroho)" (Zaburi 37:11), kuliko kufurahia maisha ya starehe. Hao"Walio na njaa na kiu ya haki …. Watashibishwa" (Math.5:6).

Wazo tu la kuwa na uzima wa milele katika ufalme mara nyingi limetumika kama 'kuwavuta kuwapa zawadi’ ya kuwashawishi watu kwenye mapenzi ya Ukristo. Ingawa hivyo, wakati huu wa kuwa nalo sisi, karibu ni la kufuata kama matokeo kwa sababu yetu ya kweli kuwamo katika ufalme ambao ni kwa kumtukuza Mungu. Ni kwa muda gani litasalia nasi baada ya sisi kubatizwa, ufahamu wetu kwa hili daima utakua. Kwa maandishi, kuishi miaka kumi tu kwa furaha ya utimilifu kabisa na dhamiri njema na Mungu lngekuwa bora kuliko maisha haya ya shida. kama hali hii yenye utukufu itadumu mielele akili peke yake inapanuka mno, na kuchukuliwa kupita upeo wa fahamu ya mwanadamu.

Hataitazamwapo kidogo zaidi kwa maneno ya kimwili, kuwa katika ufalme wa Mungu kuwe ni kusudi kuu letu kudharau faida za ulimwengu na kujikusanyia vitu vya mwilini. Badala ya kuwaza mno u karibu wa wakati ujao Yesu alishauri,"Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na haya yote mtazidishiwa"(math. 6:30 -34) Kila kitu ambacho sasa tunaweza kufikiri na kujitahidi hakilinganishwi na utimilifu wa mwisho wa kuwamo katika ufalme wa Mungu.

Tunatakiwa kutafuta "haki (ya Mungu)", yaani kujaribu kukuza upendo wa tabia ya Mungu, ambayo maana yake ni kwamba tunataka kuwa katika Ufalme wa Mungu kwa sababu haki itatukuzwa humo, kwa sababu tunataka kwa uadilifu tuwe kamili kabisa kuliko tu kwa sababu sisi wenyewe’ tunataka kuepuka mauti na kuishi maisha ya raha milele.

Tumaini la Injili lote pia mara nyingi limeonyeshwa kwa njia ambayo inatazamisha ubinafsi wa mwanadamu. Ni dhahiri kusudi letu la kuwamo kwenye ufalme wa Mungu kwa ukubwa linahitilafiana toka siku hadi siku. Tunachodokeza hapa ni wazo la ukamilifu; kipaumbele chetu ni

kujifunza injili na kuonyesha kuwa tunaitii kwa ubatizo kutokana na wazo lenye upendo wa kumtii Mungu. Kuthamini kwetu tumaini ambalo Mungu anatoa, na sababu zetu hasa za kutosha kuamo katika Ufalme, zitakua na kukomaa baada ya ubatizo wetu.


  Back
Home
Next