Misingi Ya BIBLIA
Somo La 4: Mungu Na Mauti
Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 14: Kunyakuliwa

Kuna imani iliyoenea pote miongoni mwa makanisa ya "kiinjili ya kuwa wenye haki'Watanyakuliwa’ kwenda juu mbinguni Kristo akirudi. Hii imani mara nyingi imeungwa na wazo la kuwa s dunia wakati huo itateketea kwa moto. Tumeona katika kitambo tulichokuwa tunaandika sehemu ya 9 kwamba haiwezekani. Tumeonyesha pia katika somo la 4. 7 sehemu ya kupewa thawabu ni hapa duniani, sio mbinguni. Makosa ya imani hizi msingi wake upo kuzunguka tafsiri inayokosewa ya 1 Thes. 4:16, 17; "Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni ….. nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza; kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa na Bwana milele.

Mbali toka hatari dhahiri ya kuweka imani kubwa hii juu ya fungu moja tu la maandiko, ijulikane kuwa hapa hakuna palipotajwa wenye haki kunyakuliwa kwenda mbinguni. Kristo anashuka toka mbinguni kabla ya wakristo kukutana naye. Kristo atamiliki milele juu ya kiti cha enzi cha Daudi katika mji wa Yerusalemu,tutakuwa pamoja naye, hapa duniani, kwa hiyo haiwezekani kwamba tutaishi milele pamoja naye tumening’inia kati kati ya hewa.'Hewa’ imeenea kilomita chache juu ya uso wa dunia. maana yake ni kuwa hapatajwi mbinguni makao ya Mungu.

Fungu la maneno katika sentensi ya Kiyunani lililotafsiriwa "kunyakua" hasa maana yake kukamata upesi ili kutenga; halilengi mwelekeo wowote ulio wazi. Katika Biblia ya Kiyunani Agano la Kale linatokea katika Law. 6:4 na K/Torati 28: 31 (Septugint) kuelezea'kutengana na’ au kupokonya mali kwa nguvu, hivyo ni kunyakua kama mkoba wa mtu kwa nguvu. Vile vile neno hili limetokea katika matendo ya Mituma 8: 39: "Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena ……. Lakini Filipo akaonekana katika Azoto" Hapa taarifa inaelezea jinsi Filipo alivyosafirishwa kwa muujiza toka sehemu moja ya dunia kwenda sehemu nyingine.

Kristo ajapo, wale wanaopaswa kujibu mbele zake watakusanywa pamoja sehemu ya hukumu; hawataachwa wafanye safari peke yao. inawezekana njia ya kusafirishwa sisi hadi sehemu hiyo hasa itakuwa kupitia hewani.

Yesu alisema ya kuwa "Siku ambayo mwana wa Adamu atakayofunuliwa ….. watu wawili watakuwa kondeni; mmoja atwaliwa mwingine ataachwa" (Luk. 17:30,36). Hapa tumepewa picha ile ile ya kuhamishwa ghafla. Wanafunzi kwa bidii waliuliza, "Wapi, Bwana ? Naye akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai" (Luk. 17: 37). Kama tai arukavyo kwa akili yake kupitia hewani na kisha kutua juu ya nchi ulipo mzoga, basi wanaopaswa kwenda kutoa hesabu wataletwa hadi sehemu watakayokutana na Bwana wao kwa hukumu.

Yatupasa tena tutie mkazo ya mafunzo ya hukumu mbele ya kiti cha Kristo; wanaowajibika yawapasa kwanza kufika hapo, kabla wenye haki miongoni mwao kupewa tuzo. kusoma kijuu juu 1Thes. 4:16,17 kunaweza kutupeleka kusema kuwa wote wanaopaswa na hiyo hukumu watanyakuliwa hewani, na kusalia huko na Kristo milele. Badala yake, tunajua ya kuwa walio na wajibu watakusanywa sehemu ya hukumu, yawezekana kwa kusafirishwa kupitia hewani, na kisha kupokea thawabu zao.


  Back
Home
Next