Misingi Ya BIBLIA
Somo La 4: Mungu Na Mauti
Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali

4.7 Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani?

Mbali na sababu zilizo juu, yeyote anayekuwa mbinguni sio duniani ndipo patakuwa mahala pa ufalme wa Mungu, Yaani pa tuzo iliyoahidiwa, inahitajika pia kueleza kutokana na vipengele vifuatavyo:-

  • ‘Sala ya Bwana’ inaomba ufalme wa Mungu uje (yaani, kuomba Kristo arudi), ili mapenzi ya Mungu yatimizwe duniani kama mbinguni (Math. 6:10). Kwa hiyo tunaomba ufalme wa Mungu uje duniani. Ni huzuni kwa watu maelfu wanaomba maneno haya kila siku bila kufikiri wakati bado wanaamini kuwa ufalme wa Mungu tayari sasa umewekwa imara mbinguni, na kuwa dunia itaharibiwa.

  • "Heri wenye upole; maana hao watairithi nchi" (Math. 5:5) - Sio'…… maana nafsi, roho zao zitakwenda mbinguni’. Huu unataja katika kusema Zaburi 37, yote inakaza kusema ya kwamba thawabu ya mwisho ya wenye haki itakuwa duniani. Katika hii hii halisi ambayo waovu walifurahi ukuu wao wa muda, Wenye haki watapewa zawadi ya uzima wa milele, na kumiliki nchi ambayo waovu walitawala (Zab. 37:34, 35).'Wenye upole watairithi nchi ….. maana waliobarikiwa na yeye watairithi nchi …… wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele" (Zab. 37:11, 22,29). kuishi katika nchi/ nchi ya ya ahadi milele maana yake ni kwamba uzima wa milele kuwa mbinguni hauwezekani.

  • "Daudi, ……. Alifariki akazikwa …. Daudi hakupanda kwenda mbinguni" (Mdo. 2:29,34). Badala yake, Petro alielezwa kwamba tumaini lake lilikuwa ni ufufuo toka wafu Kristo akirudi (Mdo. 2: 22 -36).

  • Dunia ni uwanja wa shughuli za Mungu kwa watu: "Mbingu ni mbingu za Bwana, bali nchi amewapa wanadamu" (Zab. 115:16).

  • Ufunuo 5:9,10 yataja maono ya wenye haki kile watakachosema watakapo kubaliwa kwenye kiti cha hukumu: "(Kristo) umetufanya kuwa wafalme na makuhani kwa Mungu wetu. nasi tutamiliki juu ya nchi". Hii picha ya kutawala katika ufalme wa Mungu duniani inaondowa kabisa wazo lisilo dhahiri ya kwamba tutafurahi'furaha kamili’ mahala fulani mbinguni.

  • Unabii wa Danieli sura ya 2 na 7 zinatoa maelezo ya mambo ya mfululizo wa nguvu za utawala, ambazo mwishowe zitaingiliwa na ufalme wa Mungu Kristo akirudi. Mamlaka ya ufalme huu itakuwa "chini ya mbingu zote" nao utajaa "dunia yote" (Dan.7: 27; 2:35,44).Huu ufalme usio na mwisho "watapewa watu, Watakatifu wake aliye juu" (Dan. 7:27); thawabu yao basi ni uzima wa milele katika ufalme huu utakao wekwa duniani, chini ya mbingu.


  Back
Home
Next