Misingi Ya BIBLIA
Somo La 4: Mungu Na Mauti
Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 13: Kwa mwili upi tunafufuliwa

Tumeonyesha kwamba uzima wa milele na kubadilika kuwa na mwili wa Uungu utatolewa na kupewa waaminifu baada ya hukumu. Kwanza Kristo atawafufua walio na wajibu kwake; na kisha kuwahukumu baada ya kuwa wamekusanyika kwake kwa kuwa mwili usiokufa watapewa kwenye hukumu, kinachofuata ni kwamba wote waliofufuliwa kwanza wanakuwa na mwili unaokufa. kama wamefufuliwa wakiwa na miili isiyokufa, basi hakuna sababu ya kiti cha hukumu ambako thawabu zitatolewa.

Tunaingia ufalme wa Mungu moja kwa moja baada ya kiti cha hukumu (Math. 25:34); basi waaminifu hawawi katika ufalme wa Mungu kabla ya hukumu. "Nyama na damu haziwezi kurithi ufalme wa Mungu (basi) . Lakini sote tutabadilika . Maana sharti huu uharibikao uvae kutoharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa" (1Kor. 15: 50,51, 53). kifuatacho ni kuwa badiliko hili la mwili, toka kufa hadi kutokufa, linatolewa kwenye kiti cha hukumu, kwa kuwa ndipo tunaingia ufalme.

Walakini, mtume Paulo mvuviwa mara nyingi anataja "Ufufuo" katika maana ya "kufufuliwa uhai" - ufufuo wa wenye haki kisha watapata uzima wa milele baada ya hukumu. kwa kweli alifahamu "kuwa kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio na haki" (Mdo. 24: 15).alikuwa anajua ya kwamba wenye wajibu "Watatoka (makaburini); Waliofanya mema, kwa ufufuo wa kupewa uzima; na walio fanya mabaya, kwa ufufuo wa hukumu" (Yoh. 5:29).

Kwa njia ya kufaa, Paulo anaonekana mara nyingi alikuwa akitaja'Kurudishiwa uhai' anapozungumzia "ufufuo". wenye haki wanatoka makaburini mwao "kwa ufufuo wa uzima " baada ya kutoka mavumbini watahukumiwa na kisha kupewa uzima wa milele. Huu mlolongo mzima ni "kurudi kwenye uhai" ipo tofauti yao, " kutoka nje" ya kaburi, na "ufufuo wa uzima" Paulo anataja juhudi yake ya kuishi maisha ya Kikristo, "ili nipate kwa njia yoyote kuifikia kiama ya wafu - yaani ufufuo wa wafu" (Fl. 3:11). Kwa sababu alikuwa na wajibu atafufuliwa atoe hesabu kwenye hukumu kwa vyovyote; alifanya bidii "ili afike kwenye ufufuo inabidi kuwa na maana kuwa "ufufuo" anaoutaja hapa ni "kurudishwa uhai".

Mifano mingine ya "ufufuo" ikiwa na maana ya "kurudi kwa uhai" (Luk. 14:14) pamoja na Luka 20: 35; Yn. 11:24; 1 kor. 15:21, 42; Ebra. 11:35; uf. 20:6. katika Zab. 17:15 Daudi anazungumzia kupokea thawabu yake mara "akiamshwa". Alikuwa na mtazamo ule ule wa kufufuka, ingawa alijua kutakuwa na hukumu. kutumia fungu hili la maneno "ufufuo" kama hili katika 1 kor. 15 linasaidia kuelezea 1 Kor. 15:52 - " wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu" Fungu la maneno "wafu" linastahili kuangaliwa mara nyingine (na hasa katika 1 Kor. 15) linataja wafu wenye haki, ambao watafufuliwa kuupokea uzima wa milele kwenye hukumu: 1 Kor. 15:13,21, 35,42; 1 Thes. 4: 16; Flp.. 3:11; Uf. 14: 13: 20: 5, 6 1 The 4: 16,17 imeorodhesha orodha ya matukio yanayounganishwa kurudi kwa Kristo.

  1. Kristo kwa kuonekana amerudi

  2. Wafu wamefufuliwa

  3. Wanao wajibu ambao wapo hai wakati huo watanyakuliwa kwenda kwenye hukumu.

Kupewa uzima wa milele ni baada ya kukusanywa huku pamoja (Math. 25: 31 - 34; 13: 41 -43); kwa hiyo kutokufa hakutolewi wakati wa kufufuka, kwa kuwa hii inatangulia kukusanyika pamoja. tumeonyesha ya kwamba wote wenye haki watapewa thawabu kwa wakati ule ule (Math. 25:34; Ebra. 11:39 -40). hii haiwezekani ikiwa kutokufa wanapewa wakati wa kufufuka, kwa sababu baada ya ufufuo hufuata kukusanywa pamoja walio hai wenye jambo la kujibu.

Walakini, ijulikane kuwa wazo letu la wakati ni la kibinadamu sana; Mungu hafungwi nao kabisa. inawezekana kwenda mbali zaidi katika kujaribu kutimiza kuandika tarehe dhahiri ya matukio yatakayotokea karibu na wakati wa kurudi Kristo. Kufufuka na kubadilishwa kwetu na kupata kutoharibika kwenye kiti cha hukumu kumeelezewa kuwa kunatokea "Kwa dakika moja, kufumba na kufumbua jicho" (1Kor. 15:51,53).Kwa ulazima, muda utakwenda na mzunguko tofauti wakati wa kurudi Kristo, hasa kwa watakao hukumiwa. ni jambo kuu la Biblia kuwa kila atakaye paswa kujibu kwenye hukumu watatoa hakimu ya maisha yao mbele ya kiti cha hukumu, kutakuwepo kiwango fulani cha majadiliano na mwamuzi - hakimu wao, Bwana Yesu Kristo (Math. 25:44 n.k; mhub. 3:17; 12:14; Luk. 12:2, 3; 19:23;Ezek. 18: 21, 22; 1Tim 5:24, 25; Rum. 14: 11,12). Tumepewa idadi kubwa ya mambo ya kujibu, inatupasa tusadiki kuwa maana ya muda utazuiwa au kwa uwingi utabanwa ili sote tuhukumiwe haraka, lakini pia mmoja mmoja. kwa sababu muda utabanwa kwenye hatua hii ili kwamba mlolongo mzima wa hukumu na ufufuo utokee " Kwa dakika, kufumba na kufumbua jicho" inaeleweka kwamba ufufuo mara nyingine uliosemwa ni njia ambayo wenye haki watapewa uzima wa milele.

Ingawa hivyo hii ni kwa sababu ya kasi tutakayohamishwa toka kaburini hata kwenye kiti cha hukumu, na kisha, kwa neema ya Mungu, kupewa kutoharibika. ukweli bado umesalia toka mistari tuliyojadili awali, kuwa Biblia inafunza kwamba uzima wa milele utatolewa kwenye kiti cha hukumu sio kwenye ufufuo. Kwa sababu hii 1 Thes. 4:17 husemwa wenye haki wataitwa kwenda kwenye hukumu kwa mlio wa parapanda, wakati 1 Kor. 15:52 unazungumzia parapanda hiyo hiyo ikiwa imeunganishwa na wao kupewa kutokufa. Hii pia yaeleza ni kwa nini Paulo aliufikiria ufufuo ni ule ule wa kukubalika mbele ya kiti cha hukumu (k.m Flp. 1:23).


  Back
Home
Next