Misingi Ya BIBLIA
Somo La 4: Mungu Na Mauti
Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 11: Purgatory

TOHARANI - MAHALI AMBAPO ROHO ZA WALIOHAKI HUISHI

Purgatory: Mahala pa ahera pa kusafisha dhambi ndogo.

Kanisa la katoliki la Roma linafundisha ya kuwa roho za watu wa Mungu zaweza kwenda mahala paitwapo'Purgatory (toharani) baada ya kufa, ambapo ni nyumba iliyopo katikati ya'Mbinguni’ na'kuzimu’. wanafundisha kuwa ni mahali pa kutakasia ambapo roho itaona maumivu kwa muda kidogo kabla ya kufaa kupata wokovu mbinguni. Maombi, kuwasha mshumaa na kutoa fedha kwenye kanisa mtu na rafiki zake imedhaniwa huweza kupunguza muda ambao roho inaweza kupata machungu katika'Purgatory’ (Toharani) kosa kubwa la mawazo haya linawekwa kutokana na ifuatavyo:-

  • Biblia ipo kimya kuhusiana na uwepo wa sehemu hii.

  • Tumeonyesha kuwa roho /nafsi unatajwa mwili wetu, sio kitu fulani kisichokufa ndani yetu, na ya kuwa'Kuzimu’ ni kaburi sio mahala pa kuadhibiwa.

  • Wenye haki kamwe hawajaahidiwa wokovu mbinguni. kupewa wokovu itakuwa kwenye kiti cha hukumu cha Kristo akirudi, sio wakati mwingine baada ya kufa hapo idhaniwapo kuondoka katika'Purgatory’ (Toharani) (Math. 25:31 -34; Ufu.22:12).

  • Wote wenye haki wapokea tuzo kwa wakati mmoja, sio kila mtu hupata wokovu kwenye nyakati tofauti (Ebra. 11:39,40;2 Tim. 4:8).

  • Kinachofuatiwa na kifo ni ukimya kabisa wa kutokuwa na fahamu, sio shughuli zilizodokezwa kwa mafundisho ya Purgatory. (Toharani).

  • Tunatakaswa dhambi zetu kwa njia ya Ubatizo katika Kristo na kuendelea katika imani thabiti kwa kufanya matendo yake wakati wa maisha yetu ya sasa, sio kupitia kipindi kingine kuteswa baada ya kufa. tunaambiwa'Jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale’ ya dhambi katika maisha yetu (1 Kor. 5:7); tujitakase toka katika matendo yetu ya dhambi (2 Tim. 2:21; Ebra. 9:14).

Basi muda wetu wa kujisafisha ni sasa, katika maisha haya, sio mahala pa kutakasa (‘Purgatory’) (Toharani) ambayo tunaingia baada ya kufa. Wakati uliokubalika ndio sasa …… Siku ya wokovu ndio sasa" (2 Kor. 6:2). Tunapo mtii Mungu kwa ubatizo na kuendeleza tabia ya kiroho katika Maisha haya tutaongozwa kupata wokovu wetu (Gal. 6:8) - sio kutumia muda katika'Purgatory’ (Toharani).

  • Juhudi ya wengine kutuokoa kwa kuwasha mishumaa na michango mingine ya pesa kwa kanisa la katoliki, haita geuza wokovu wetu kabisa. " Hao wanaozitumainia mali zao …… hakuna mtu waezaye kumkomboa ndugu yake, wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake ….. ili aishi siku zote asilione kaburi" (Zab. 49: 6-9).


  Back
Home
Next