Misingi Ya BIBLIA
Somo La 4: Mungu Na Mauti
Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 12: Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine

Imani ya kuwa Binadamu anaendelea kuishi katika umbo la mtu mwingine au la mnyama akiwa ana roho yake, likuwa ni moja ya njia ya zamani ambazo binadamu alijaribu kujisadikisha mwenyewe kuwa kifo hakikuwa ndio mwisho kilipotokea. Tumeeleza kuwa roho ya binadamu inatajwa pumzi /nguvu ya kuwa hai iliyo ndani yake, ambayo humrudia mungu anapokufa (Mhubiri 12:7). Hii ina maana kwamba roho yake haihami na kuzunguka ikiwa ni'Mzuka’, wala ipo huru kuwa na mtu mwingine au mnyama hivyo basi utu wa mtu unaendelea katika wao. Kila mmoja tutahukumiwa kwa matendo yetu wenyewe (2Kor. 5:10). Ikiwa sifa na tunayotenda ni tabia inayotenda kazi ya mtu mwingine aliyepita, basi hili wazo la Mungu kuhukumu na kutupa tuzo kulingana na kazi zetu (uf. 22:12) halina maana.

Mtu anapokufa roho humrudia Mungu, fahamu zote zinakoma. Jaribio lolote la kukutana na wafu basi linaonyesha kutofahamu mno fundisho kubwa la Biblia kuhusu hili (tazama Isa. 8:19,20).Biblia ipo wazi kabisa kuwa watu hawazirudii nyumba zao za kwanza au miji kwa namna yoyote baada ya kufa; hakuna kitu kama'roho’ au'kizuka’ kurudia mahali hapa mtu akiwa amekufa: " (Binadamu) ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe: hao waliomwona watasema yupo wapi ? ….. hataonekana. Jicho lililomwona halitamwona tena; wala mahali pake (nyumba /mji) hapata mtazama tena" Ayubu. 7:9,10 ni kama huu: "Huyo ashukaye kuzimuni ….. hatarudi tena nyumbani kwake, wala mahali pake hapatamjua tena" Kukubali hili kwa unyenyekevu litatuongoza kubadilisha madai yote kuwa tumeona'mizuka’ ya watu waliokufa, wakirudi nyumba zao za zamani. mambo haya inabidi yawe ni udanganyifu wa mawazo ya kuwaza mambo asiyoona.


  Back
Home
Next