Misingi Ya BIBLIA
Somo La 4: Mungu Na Mauti
Binadamu | Nafsi Au Roho | Roho ya Mtu | Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa | Ufufuo | Hukumu | Mahali pa Kupewa Thawabu: Mbinguni au Duniani? | Uwajibikaji Mbele Za Mungu | Kuzimu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Purgatory, Roho na mafunzo ya kuwa huingia kwenye mwili mwingine, Kwa mwili upi tunafufuliwa, Kunyakuliwa) | Maswali

4.8 Uwajibikaji Mbele Za Mungu

Kwa kawaida ikiwa binadamu ana'nafsi isiyokufa’ analazimika kuwa na maisha ya kuishi miele mahali pengine - aidha mahali pa kupewa thawabu au mahali pa kuadhibiwa. Hapa panadokezwa kwamba kila mtu ana wajibu mbele za Mungu. Kwa utofauti; tumeonyeshwa jinsi Biblia inavyofunza kuwa binadamu amefanana na wanyama, ndani yake hana kitu kisichokufa. Lakini, watu wengine wametoa tumaini la uzima wa milele katika ufalme wa Mungu. Na iwe dhahiri kuwa sio kila mtu aliyewahi kuishi atafufuliwa; kama wanyama, binadamu anaishi na kisha kufa, na kuoza katika mavumbi. Lakini kwa kuwa hukumu itawekwa na wengine wakisha hukumiwa, wengine kuzawadiwa uzima wa milele, inatubidi tusema kwamba watakuwepo aina ya watu ambao watafufuliwa ili wahukumiwe na kupewa tuzo .

Mtu ikiwa atafufuliwa au la hutegemea ikiwa anapasiwa na hukumu msingi wa hukumu yetu utakuwa vipi maarifa yetu yameitikia neno la Mungu. Kristo alieleza: -"Yeye anikataae mimi, asiyeyakubali maneno yangu anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalo mhukumu siku ya mwisho" (Yoh.12:48).Wale ambao hawajafahamu au kuelewa neno la Kristo, na hivyo hakuwa na nafasi ya kumkubali au kumkataa, hawatahesabiwa kwa hukumu. "Kwa kuwa wote waliokosa pasipo wenye sheria (ya Mungu) watapotea pasipo sheria; na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria (Kwa kuwa walielewa)" (Rum. 2:12). Hivyo wale ambao hawajajua matakwa ya Mungu wataangamia kama wanyama; wakati wote kwa kujua wanavunja sheria ya Mungu wanahitajika kuhukumiwa, na kwa sababu hii watafufuliwa ili waikabili hukumu.

Mbele za Mungu "Dhambi haihesabiwi isipokuwa sheria" Dhambi ni kuvunja sheria ya (Mungu)"; " kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria" (Rum. 5:13; 1 Yoh. 3:4; Rum 3:20). Pasipo kujua sheria za Mungu kama zilivyofunuliwa katika neno la Mungu, "Dhambi haihesabiwi" kwa mtu, kwa sababu hii hawahukumiwi au kufufuliwa. Wale wasiojua au kuelewa neno la Mungu basi watabakia wamekufa, kama watakavyokuwa wanyama na mimea, kwa Kuwait wana nafasi moja. "Mwanadamu ….. iwapo hana akili, amefanana na wanyama wapoteao" (Zab. 49:20). "Kama kondoo wanawekwa kwenda kuzimu" (Zab. 49:14).

Ni kujua njia za Mungu ndiko kunatufanya tuwajibike mbele zake kwa ajili ya matendo yetu na kwa sababu hii ni lazima kufufuliwa na kutokea kwenye kiti cha hukumu. Basi ifahamike kwamba sio peke yao wenye haki au waliobatizwa watakaofufuliwa, bali wote walio na wajibu kwa Mungu kwa sababu ya wao kumjua. Hili ni neno la maandiko lililorudiwa mara nyingi: -

  • Yohana 15:22 unaonyesha ya kwamba kujua neno kunaleta uwajibikaji: "Kama mimi (Yesu) nisingelikuja na kusema nao, wasingelikuwa na dhambi: Lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao" Warumi 1:20 -21 vile vile yasema kwamba kumjua Mungu kunawafanya watu "wasiwe na udhuru".

  • "Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba …..Nami (Kristo) nitamfufua siku ya mwisho" (Yoh. 6:44,45).

  • Mungu tu "amejifanya haoni" matendo ya wale wasiojua kabisa njia zake.Wale wanaojua njia zake, anawaona na kutegemea kuitikia (Mdo. 17:30).

  • Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya Bwana wake, asijiweke tayari; wala kuyatenda mapenzi yake,atapigwa sana.Naye asiyejua naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo (Yaani kwa kubaki mfu). Maana kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi, naye waliyemweka amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi" (Luk. 12:47,48) - Basi ni kiasi gani zaidi ?

  • "Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi" (Yak. 4:17).

  • Wajibu wa Israeli mahususi kwa Mungu ndio ulikuwa unaeleza ufunuo wake kwao kuhusu Yeye mwenyewe (Amosi. 3:2).

  • Sababu ya fundisho hili la uwajibikaji, "Ingekuwa heri kwao (wanaorudi na kugeuka toka kumfuata Mungu) wasingeliijua njia ya haki na, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa" (2 Pet.2:21). Mafungu mengine ya maneno ni pamoja na: Yoh. 9:19; 1 Tim. 1:13;Hosea 4:14; K/Torati 1:39.

Kumjua Mungu kunatufanya kufika kwenye kiti cha hukumu, kinachofuata ni kwamba wale wasio na elimu hii hawatafufuliwa, kwa kuwa hawahitajiki kuhukumiwa, na huko kukosa kwao elimu kunawafanya wawe "kama wanyama wanaopotea" (Zab.49:20). Zipo ishara kubwa zinazoonyesha kwamba sio wote waliokuwa hai watafufliwa:-

Watu wa zamani wa taifa la Babeli "Hawatafufuka" baada ya kufa kwao kwa sababu walikuwa hawamjui Mungu wa kweli (Yer.51: 39; Isa. 43: 17).

Isaya mwenyewe alijipa moyo: "Ee BWANA, Mungu wetu wa (Israeli), mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki (Yaani, Wafilisti na Wakaldayo) …..Wao wamekufa, hawataishi (tena); Wamekwisha kufariki hawatafufuka; ……… na kuupoteza ukumbusho wao umepotea" (Isa. 26: 13,14). Ona mkazo mara tatu hapa juu ya kutofufuliwa kwao: Hawataishi (tena) …… hawatafufuka na kupoteza ukumbushop wao" kwa utofauti, Israeli alikuwa na "Wafu wako (Israeli) wataishi, miili yao itafufuka (B.H.N)" (Isa. 26:19).

Akizungumzia kuhusu watu wa Mungu -Israeli, tumeambiwa ya kwamba Kristo atakaporudi, "wengi wa hao waliolala katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine kwa uzima wa milele, wengine kwa aibu na kudharauliwa milele" (Dan. 12:2). Hivyo "Wengi" bali sio wote, Wayahudi watakaofufuliwa, kwa ajili ya wajibu wao kwa Mungu wakiwa ni watu wake walioteuliwa. kati yao wasiomjua Mungu wao wa kweli'watalala, wasiamke tena’ kwa kuwa hawana uwezo kupata "Neno la Mungu" (Amosi 8:12, 14).

SASA TUMEJIFUNZA KWAMBA: -

  1. Kujua neno la Mungu kunafanya kuwajibika kwake.

  2. Wanaowajibika ndio tu watafufuliwa na kuhukumiwa.

  3. Wasiomjua Mungu wa Kweli kwa Sababu hii watabakia na hali yao ya kufa kama wanyama.

Vidokezo vya maneno haya vinafanya pigo baya kwa kiburi cha mwanadamu kwa kile ambacho kwa kawaida tunapenda kuamini: mamilioni ya watu,pande mbili, sasa na katika historia nzima, ambao hawaijui Injili ya kweli; kwa ugumu wa akili mbaya, ambao hawawezi kuelewa ujumbe wa Biblia; watoto wadogo na wachanga ambao wamekufa kabla ya kuwa watu wakubwa vya kutosha kuifahamu Injili; makundi yote hayo yanaangukia ndani ya aina ya wale ambao hawana elimu ya kweli juu ya Mungu, na kwa hiyo hawawajibiki kwake.

Hii ina maana kwamba hawatafufuliwa, bila kuangalia nafsi ya kiroho ya wazazi wao. Hiii huenda kinyume na chembe ya kufuata mambo ya binadamu na haja zetu zote za mwili na mawazo; Lakini unyenyekevu wa kweli kuhusu neno la Mungu kwa ukweli wa mwisho,ukiwekwa pamoja na unyenyekevu wa wazo linalostahili kwa umbo letu wenyewe, litatufanya tukubali ukweli huu. upimaji ulionyooka wa ukweli anaopata mwanadamu, hata bila ya mwongozo wa Andiko, pia tumaiani la maisha yajayo haliwezi kuwapo kwa makundi yaliyotajwa hapo juu.

Hoja yetu kwa njia za Mungu katika mambo haa ni nje mno ya amri: "Lakini, ewe binadamu, U nani hata uthubutu kumhoji Mungu ?" (Rum. 9:20 - B.H.N.). Tunaweza kukubali bila kufahamu, lakini kamwe haitupasi kumshitaki Mungu kwa udhalimu au kutokuwa na haki. Kidokezo cha kwamba Mungu anaweza kuwa katika njia yoyote ya kutopenda au katika kosa kunaendeleza mtazamo wa kuogofya kwa mwenyezi Mungu, Baba na Muumba anayewatendea viumbe wake bila akili na njia isiyo haki. Taarifa ya mfalme Daudi ya kupotewa na mtoto wake katika kuisoma inasaidia; 2 Sam. 12: 15 -24 habari imetolewa jinsi Daudi alivyoomba kwa bidii kwa ajili ya mtoto wakati akiwa hai, lakini akakubali mwisho wa kifo chake kuwa kilikuwa kitokee tu: "Mtoto alipokuwa hai, nalifunga, nikalia: kwa maana nalisema, Ni nani ajuaye kwamba Bwana atanihurumia, mtoto apate kuishi ?. Lakini sasa amekufa nifungie nini ? Je ! naweza kumrudisha tena ? ….. Hatanirudia mimi". Naye Daudi akamfariji mkewe, mapema iwezekanavyo akawa na mtoto mwingine.

Hatimae, inabidi isemwe ya kwamba watu wengi, kwa kushika jambo hili la wajibu kwa Mungu, wanaona kuwa hawana haja kupata elimu yoyote ya kumjua zaidi kwa kadhia wanakuwa na wajibu kwake na hukumu. lakini kwa kiwango kingine yaelekea kwamba watu hawa ni tayari wana wajibu kwa Mungu, wao kufahamu elimu ya neno la Mungu lililowafanya wajue ukweli kwamba Mungu anafanya kazi katika maisha, akiwapa uhusiano wa kweli pamoja naye. Inabidi ikumbukwe ya kwamba "Mungu Ni Pendo", naye "Hapendi mtu yeyote apotee", na akamtoa mwanae wa pekee, ili yeyote amwaminie asipotee, bali awe na uzima wa milele" (1 Yoh. 4:8;2 Pet. 3:9; Yn. 3:16).

Heshima hii na haki ya mtu isiyoepukika inaleta majukumu ya kujibu. Lakini haya hayajakusudiwa kuwa mazito sana au ya kututaabisha; Kama kweli tunampenda Mungu, tutafahamu ya kwamba yeye katupatia wokovu sio tuzo inayofanywa bila kufikiri kwa ajili ya matendo fulani, bali kwa upande wake ni nia ya upendo kufanya yote awezayo kwa ajili ya watoto wake, kuwapa uzima wa milele na furaha, kwa kufahamu tabia na sifa ya ajabu.

Tunapokubali na kusikia wito wa Mungu kwa njia ya neno lake, tutatambua ya kwamba tunapotembea katika kusanyiko, Mungu anatuangalia kwa nguvu maalumu, kwa shauku akitafuta nguvu za kuvutika kwetu kwenye upendo wake, kuliko kutusubiri kufikia majukumu yetu. Jicho hilo la upendo kamwe haliwi mbali nasi; wala hatuwezi kusahau wala kutangua maarifa yetu kwake ili kuufurahisha mwili, kuwa huru na wajibu kwa Mungu. Badala yake, tuweze kujifurahisha kwa tendo maalum la kuwa karibu na Mungu na hivyo tuamini ukuu wa pendo lake, tunapotafuta kumjua zaidi kuliko kidogo. Upendo wetu njia za Mungu na nia ya kuzijua, vivi hivi basi tuweze kwa usahihi zaidi kumuigiza, kuwe muhimu kuliko woga wetu kwa utakatifu wake mkuu.


  Back
Home
Next