Misingi Ya BIBLIA
Somo La 3: Ahadi za Mungu
Dibaji | Ahadi Katika Edeni | Ahadi Kwa Nuhu | Ahadi Kwa Abrahamu | Ahadi Kwa Daudi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (The Kuharibiwa kwa Mbingu na Nchi (Ufu. 21:1; 2Pet. 3:6-12)., Madai ya "Uisraeli wa Visiwa vya Uingereza") | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 9: The Kuharibiwa kwa Mbingu na Nchi (Ufu. 21:1; 2Pet. 3:6-12).

Lengo la Mungu likiwa ni kusimamisha ufalme wake hapa duniani (Ona somo la 5), haidhaniwi kuwa ataiharibu hii sayari yenyewe, na somo la 3.3 limeonyesha ya kuwa kwa uthabiti amehahidi kutofanya jambo hili. Mstari uliopo hapo juu kuangamiza mbingu na nchi inabidi uchukuliwe kwa mfano.

Fungu la maneno kutoka Petro laonyesha mfano mmoja kati ya hukumu iliyopita duniani wakati wa Nuhu na itakavyotokea kwenye "Siku ya Bwana" wakati ujao. "Dunia ile ilivyokuwepo wakati ule, iligharikishwa na maji, ikaangamia, Bali mbingu na nchi, zilizopo sasa …… zimewekwa akiba kwa moto zikilindwa hata siku ya hukumu" (2 Pet. 3:6,7).

Petro anaonyesha tofauti kati ya maji yakiwa ni wakala wa kuangamiza kwenye kipindi cha Nuhu, na moto utakaotumika atakapokuja mara ya pili.'Mbingu na nchi’ za kipindi cha Nuhu zenyewe hazikuharibiwa - wenye miili wote’ wenye dhambi waliharibiwa (Mwa. 7:21; 6: 5, 12).'Mbingu na nchi’ kwa sababu hii unatajwa utaratibu wa mambo au muungano wa watu. Wale wasiofahamu hili fungu la maneno wanaelekea kusahau kuharibiwa kwa 'Mbingu’ zinazosemwa karibu. hii haiwezi kuchukuliwa ilivyo - ni mahali ambapo ni makao ya Mungu (Zab. 123: 1), mahali ambapo hakuna wenye dhambi (Hab. 1: 13; Zab. 65: 4, 5), ni ambazo hutangaza utukufu wa Mungu (Zab. 19:1).Kama zinataja jambo lingine katika mfano, basi inabidi nayo 'nchi’.

Mafungu yafuatayo ya maneno yanaonyesha jinsi'Mbingu na nchi’ katika sehemu zingine za Biblia hazitafsiriwi jinsi zilivyo, bali zinataja kidogo mfumo wa mambo ya dunia.

  • "Naliangalia nchi, na tazama ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo hazina nuru ….. maana BWANA asema hivi, Nchi yote (ya Israeli) itakuwa ukiwa …… Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza na mbingu zitakuwa nyeusi" (Yer. 4:23 -28). Hizi ni hukumu kuja juu ya 'Mbingu na nchi’ za watu wa Israeli ambazo (si mbingu na dunia halisi) zitaomboleza.

  • Hapo kwanza Musa aliwatangazia Waisraeli wote "Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; na nchi isikie maneno ya kinywa changu" (Kum. 32:1). mkazo umetiwa wa kuwa palikuwepo aina mbili za watu ambao alizungumza nao: 1) "Wazee wote wa kabila zenu"na

  • 2) "Kusanyiko lote la wana wa Israelli" (Kum. 31: 28,30).Wakati ule wazee walilinganishwa na 'Mbingu’ na watu wa kawaida na 'Nchi’.

  • Isaya alianza unabii wake kwa jinsi hii: "Sikieni, enyi mbingu, tega sikio Ee nchi ……. Lisikieni neno la BWANA, enyi waamuzi ……tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu" (Isa. 1: 2,10). Tena ipo mistari sambamba kati ya mbingu na viongozi; na kati ya nchi na watu.

  • Ataziita mbingu zilizo juu, na nchi pia awahukumu watu wake" Israeli (Zab. 50:4) huu wajisema wenyewe.

  • "Nami nitatikisa mataifa yote … nitazitikisa mbingu na dunia" (Hagai 2:7,21) vile vile.

  • "Maana upanga wangu umekunywa na kushiba mbinguni: tazama utashukia Edomu, … upanga wa BWANA umeshiba damu … maana BWANA …. machinjo makubwa katika nchi ya Edomu" (Isa. 34:5,6) hapa'Mbingu' zimelinganishwa na Edomu; Unabii uliotangulia kama jeshi lote la mbingu litafumliwa’ (Isa. 34:4) kwa hiyo inatajwa Edomu kufumuliwa.

  • Mbingu na nchi zilizotajwa zikifumuliwa au kunyauka katika Isaya 13 wanatajwa watu wa Babeli. katika mfululizo wa taarifa kuhusu Babeli tunasoma ya kuwa Mungu'atazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake ….. itakuwa kama vile paa aliyetikiswa ….. kila mtu atageukia watu wake, nao watakimbia, kila mtu aende nchi yake mwenyewe" (Isa. 13:13,14). Kuondoka kwa mbingu na nchi kumewekwa sawa na huko kwa watu, Ebra. 9:26 yasema "Mwisho wa dunia" ukiwa unatokea katika karne ya kwanza B.K - katika maana ya kuwa ulimwengu wa Wayahudi ulikuwa unaisha wakati ule.Katika fikira yote haya yakishikwa kwa uthabiti, itegemewe kuwa mistari ya agano Jipya inayotaja mbingu mpya na nchi atakaporudi Kristo itataja utaratibu mpya wa mambo utakaoonekana hapo ufalme wa Mungu ukisimamishwa.

Uchunguzi wa karibu kwa 2 Pet. 3 unathibitisha hivi. tukiisha eleza namna'mbingu na nchi’ za sasa zitakavyoisha, mstari wa 13 unaendelea: "Lakini kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake" Huku ni kunukuu ahadi ya Mungu iliyo katika Isaya 65:17: "Maana tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya". Mistari inayoendelea katika Isaya 65 yaeleza utaratibu huu mpya kuwa ni hali timilifu hapa duniani:

"Tazama, naumba Yerusalemu iwe shangwe.. Hawatajenga, akakaa mtu mwingine …..mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia (yaani, maisha ya kuishi yatarefushwa) …. Mbwa mwitu na mwanakondoo watalisha pamoja" (Isaya 65: 18 -25).

Baraka zote hizi ni dhahiri zinahusu jambo la ufalme ujao wa Mungu duniani -'Mbingu na nchi mpya zitakazo ingia mahali pa hizi zilizopo zilizosimama kwa huzuni.


  Back
Home
Next