Misingi Ya BIBLIA
Somo La 3: Ahadi za Mungu
Dibaji | Ahadi Katika Edeni | Ahadi Kwa Nuhu | Ahadi Kwa Abrahamu | Ahadi Kwa Daudi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (The Kuharibiwa kwa Mbingu na Nchi (Ufu. 21:1; 2Pet. 3:6-12)., Madai ya "Uisraeli wa Visiwa vya Uingereza") | Maswali

3.3 Ahadi Kwa Nuhu

Maendeleo ya historia ya mwanadamu yalipokwenda mbele baada ya kipindi cha Adamu na Eva, mwanadamu akaongezeka na kuwa mwovu sana, mambo yalifikia hatua ambayo ustarabu wa uadilifu ukaharibika mno ambapo Mungu akaamua kuuharibu utaratibu wa mambo, Isipokuwa nuhu na familia yake (Mwa. 6:5-8).Akaambiwa atengeneze safina ambayo ndani yake yeye na wanyama wote miongoni mwa waliochaguliwa wataishi kipindi cha wakati hapo ulimwengu utakapokuwa unaangamia kwa gharika. kwa kupita, ipo sababu kubwa ya kisayansi ya kuamini kwamba mafuriko haya makubwa yalitokea kweli, mbali ya taarifa za wazi za maandiko ! Fahamu kuwa dunia (Yaani, hii sayari halisi) haikuharibiwa, wanadamu waovu waliosimamishwa juu yake tu."Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi" (Mwa. 7:21).Yesu (Math. 24:34) na Petro (2Petr.3:6 -12) Wote wawili waliielewa hukumu ya ulimwengu wa Nuhu una mfano mmoja na itakayotokea Kristo atakapokuja mara ya pili. Maovu mengi mno ya mwanadamu katika kipindi cha Nuhu yanalingana na ya ulimwengu wa leo, ambao hu karibu kuadhibiwa Kristo atakaporudi.

Kwa sababu ya udhalimu wa dhambi ya mwanadamu na orodha ya mambo ya kuiharibu sayari hii yenyewe ambayo imeanza, imetokea imani, hata miongoni mwa wakristo, ya kuwa dunia hii itaangamizwa. Wazo hili ni wazi linaonyesha kutokufahamu kabisa ujumbe wa Msingi wa Biblia - wa kwamba Mungu ni mwenye uweza anayejihusisha na mambo ya sayari hii, Na ya kuwa mapema Yesu Kristo atarejea kuusimamisha ufalme wa Mungu hapa duniani.Ikiwa mwanadamu ameruhusiwa kuiharibu sayari hii basi ahadi hizi haziwezi kutungwa barabara. Ushahidi wa maana kuwa ufalme wa Mungu utakuwa duniani unapatikana katika somo la 4 -7 na somo la 5. Wakati ule ule ufuatao utakuwa ni uthibitisho wa kutosha kuwa dunia na utaratibu wa sayari hautaharibiwa: -

  • "Kama dunia aliyoiweka imara milele" (Zab. 78:69);

  • "Nayo dunia hudumu daima"

  • "…….jua na mwezi……nyota…..mbingu amevithibitisha hata milele na milele, ametoa amri wala haitapita" (Zab.148:3 -6).

  • "Dunia itajawa na kumjua BWANA, kama vile maji yanavyoifunika bahari" (Isaya.11:9)

  • (Hesabu 14:21) - Vigumu, ikiwa Mungu ataiacha dunia yenyewe iharibiwe. Ahadi hii bado kutimizwa.

  • "BWANA aliyeziumba mbingu asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara, hakuiumba ukiwa; aliiumba ili ikaliwe na watu " (Isaya 45:18). Ikiwa Mungu aliiumba dunia tu aione yaharibiwa, basi kazi yake ilikuwa haifai.

Bali nyuma kabisa katika Mwanzo Mungu aliyahahidi yote haya kwa Nuhu. kama alivyoanza kuishi tena katika ulimwengu ulioumbwa na gharika, labda Nuhu alihofu ya kuwa kutaweza kuwepo maangamizi mengine ya jumla. Popote ilipoanza kunyesha mvua baada ya gharika, Wazo hili lilibidi limjie akilini mwake. Na hivyo Mungu akafanya Agano (mfululizo wa Ahadi) kuwa jambo hili halitatokea kamwe mara ya pili:-

"Mimi, tazama, nalithibitisha Agano langu nanyi; …… na agano langu nitalithibitisha nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; …….(Ona mkazo wa "MIMI" - ajabu ya Mungu akichagua kufanya ahadi na mtu mfu !); Mwa.9: 9-12).

Agano hili lilithibitishwa na upinde wa mvua: -

"Hata itakuwa nikitanda mawingu (ya mvua) juu ya nchi, upinde utaonekana winguni: nami nitalikumbuka agano langu …… kati yangu nanyi ….. Agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilicho katika nchi ……Hii ndiyo ishara (Upinde wa mvua) ya agano" (Mwa 9:13 -17).

Kwa sababu ni Agano la milele kati ya Mungu na watu na wanyama wa dunia, kinachofuata ni kwamba dunia ilipasa watu na wanyama waishi milele humu. Huu wenyewe ni uthibitisho kuwa ufalme wa Mungu utakuwa kwenye dunia hii kuliko kusema mbinguni. Ahadi hii kwa Nuhu ni msingi wa Injili ya ufalme ; inaonyesha jinsi macho ya Mungu yanalenga kwenye dunia hii , na jinsi alivyo na kusudi nayo. hata katika hasira anakumbuka rehema (Heb. 3:2), na huu ndio upendo wake ambao hata viumbe wanyama wake anawajali (1 Kor. 9:9; Yona 4:11).


  Back
Home
Next