Misingi Ya BIBLIA
Somo La 3: Ahadi za Mungu
Dibaji | Ahadi Katika Edeni | Ahadi Kwa Nuhu | Ahadi Kwa Abrahamu | Ahadi Kwa Daudi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (The Kuharibiwa kwa Mbingu na Nchi (Ufu. 21:1; 2Pet. 3:6-12)., Madai ya "Uisraeli wa Visiwa vya Uingereza") | Maswali

3.4 Ahadi Kwa Abrahamu

Injili aliyoifundisha Yesu na Mitume kwa msingi haikuwa tofauti na alivyoielewa Abrahamu. Mungu, katika maandiko,"Alimhubiri Abrahamu Injili nzima" (Gal. 3:8) Ahadi hizi ni za maana sana hata Petro alizianza na kumaliza kutangaza hadharani habari njema akiwatajia hizo (mdo. 3:13,25). Kama tunaweza kuelewa alichofunza Abrahamu, ndipo tutakuwa na picha ya msingi kabisa ya Injili ya Kikristo. kuna ishara zingine ambazo zinaonyesha kuwa "Injili" sio jambo fulani ambalo lilianza barabara kwenye kipindi cha Yesu:-

"Tunawahubiri habari njema (Injili) ya ahadi ile waliyopewa mababa, ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo" (Mdo. 13:32,33).

"Injili ya Mungu, ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake (Yaani,Abrahamu,Mwa.20:7) katika Maandiko matakatifu" (Rum. 1:1 -2).

"Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili" (1Pet. 4:6) - yaani waamini ambao waliishi na kufa kabla ya karne ya kwanza.

"Maana ni kweli , sisi nasi tumehubiriwa Injili vile vile kama hao" (Ebra 4:2) - Yaani, Israel walipokuwa jangwani

Ahadi zilizofanywa kwa abrahamu zina mambo mawili ya msingi :

 1. Mambo yanayohusu uzao wa Abrahamu (mtoto maalamu) na

 2. Mambo yanayohusu nchi aliyoahidiwa Abrahamu.

Ahadi hizi zimefafanuliwa katika Agano Jipya, na, kuendelea na utaratibu wetu kuifanya Biblia ijieleze yenyewe , tutaunganisha mafunzo ya sehemu mbili za maagano ili tupate picha kamili aya Agano lililofanywa kwa Abrahamu.

Abrahamu awali aliishi Uri, mji wenye ustawi ambao sasa ni Iraki. Watafiti wa mabo ya kale wa siku hizi wanadhihirisha ustaarabu wa hali ya juu ambao ulifikiwa na wakati wa Abrahamu. ulikuwepo utaratibu wa mabenki, utumishi wa Serikali na utaratibu wa kutawala. Akijua hakuna tofauti, Abrahamu aliishia katika mji huu, kama tunavyomjua mtu wa ulimwengu. Lakini ndipo mwaliko wa Mungu ulio wa ajabu ukinijia -ayaache hayo maisha ya walimwengu na kuanza safari kuelekea nchi ya ahadi. Wapi kabisa na kwa ukamilifu haikufanywa dhahiri barabara. Akaambiwa yote, mwishowe ikawa ni safari ya maili 1,500.Nchi ilikuwa ni Kanani -Israeli ya sasa.

Mara kwa mara wakati wa uhai wake, Mungu alimtokea Abrahamu na akarudia na akapanua ahadi zake kwake. Hizi ahadi ndizo msingi wa Injili ya Kristo, basi kama tu wakristo wa kweli mwaliko huo huo unatujia kama ulivyofanywa kwa Abrahamu, ili kuyaacha mambo ya muda mfupi ya maisha haya, na kwenda mbele kwenye maisha ya Imani, Ahadi za Mungu zikichukuliwa kwa kuzithamini, kuishi kwa kufuata neno lake. tunaweza kuwaza vema ni jinsi gani Abrahamu alitafakari juu ya Ahadi alipokuwa anasafiri."Kwa imani Abrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali atakapopapata kuwa urithi; alitii, akatoka asijue aendako" (Ebra. 11:8).

Tunapoona kwa mara ya kwanza ahadi za Mungu , Nasi vile vile tunaweza kujiona kwamba hatujui hasa ni nchi gani ya ahadi ya ufalme wa Mungu itakavyokuwa. Bali imani yetu katika neno la Mungu iwe hivi ila nasi pia tuwe ni wenye bidii kutii.

Abrahamu hakuwa mtu wa kuzunguka asiyetaka kukosa mahali bila jambo jema moyoni kama kutengemea kubahatisha hizi ahadi. Alitoka kwenye maisha ya ulimwengu ambayo, kwa maneno makubwa yana mambo mengi yaliyo na hali iliyo sawa na yetu wenyewe. Maamuzi yenye sehemu nyingi yanayoumiza aliyakabili yalikuwa na sura moja kwa hayo yaliyotupasa kuyakabiri tunapofikiri ikiwa tukubali na kutenda kazi ahadi za Mungu toka mojawapo ya watu wafanyao mambo mageni, kuangaliwa kwa mzaha katika jicho toka kwa majirani ("amepata dini") …. Mambo haya yalikwisha julikana kwa Abrahamu. azimio ambalo abrahamu alilihitaji hata kufika katikati nalo lote lilibidi kuwa kubwa mno. Jambo pekee lililotoa azimio hilo pote pote katika miaka ya safari yake ndefu lilikuwa ni neno la ahadi. Ilimbidi kujikumbusha maneno hayo na kila siku akayatafakari hasa yalikuwa na maana gani kwake.

Kwa kuonyesha imani kama hii na kuitenda kazi, tunaweza kuwa na heshima ijayo hiyo kama Abrahamu - kuitwa marafiki wa Mungu (Isaya 41:8), kupata maarifa ya Mungu (Mwa. 18:17) na kuwa na tumaini imara la uzima wa milele katika Ufalme. tena tunasisitiza ya kuwa Injili ya Kikristo msingi wake ni ahadi hizi kwa Abrahamu. Kuuamini kwa kweli ujumbe wa Kikiristo, nasi pia, yatupasa kwa uthabiti kujua ahadi zilizofanywa kwa Abrahamu. Bila hizo imani yetu sio imani. Kwa macho yenye bidii basi tusome na kusoma tena mazungumzo yaliyoandikwa baina ya Mungu na Abrahamu.

NCHI

 1. "Toka wewe katika nchi yako …… uende mpaka nchi ambayo nitakuonyesha" (Mwa. 12:1)

 2. Abrahamu "akaendelea kusafiri ….. mpaka Betheli (ndani katikati ya Israeli).BWANA akamwambia Abrahamu ….. Inua sasa macho yako, ukatazame toka hapo ulipo, upande wa kaskazini na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi, maana hii nchi yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele ….. katembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo" (Mwa. 13: 3, 15: 18).

 3. "Siku ile BWANA akafanya agano na Abrahamu, akasema , uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huu mto mkubwa, mto Frati" (Mwa 15:18).

 4. "Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kaanani, kuwa miliki ya milele" (Mwa 17:8).

 5. "Ahadi ile ya kwamba (Abrahamu) atakuwa mrithi wa ulimwengu" (Rum. 4:13).

Hapa tunaona ufunuo wa kuendelea mbele kwa Abrahamu: -

 1. "Ipo nchi ambayo ningependa hata uende huko"

 2. "Sasa umefika katika eneo. Wewe na watoto wako mtaishi hapa milele" Elewa jinsi ya ahadi hii ya uzima wa milele ilivyoandikwa Pasi na uzuri wa kudanganya au mkazo; mwanadamu angeianzisha hapana shaka ingefanywa kuwa nyepesi.

 3. Eneo la nchi ya ahadi lilifafanuliwa na kuwekwa wazi zaidi:

 4. Abrahamu hakutarajia kupata ahadi katika maisha haya - alikuwa awe ni "mgeni" katika nchi, ingawa baadae ataishi milele humo. kidokezo cha hii ni kuwa atakufa na kisha baadae kufufuliwa na kumwezesha kupata ahadi hii.

 5. Paulo, akiongozwa na Roho kuandika, ni dhahiri aliona Ahadi kwa Abrahamu kuwa na maana ulimwengu wote ni urithi wake.

Maandiko yanaacha nia yake ili kutukumbusha ya kuwa Abrahamu hakupata kuona utimilifu wa ahadi katika zama za uhai wake:-

"Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama nchi isiyo yake (Panadokeza namna ya maisha ya muda) akikaa katika hema" (Ebra. 11:9).

Aliishi kama mgeni katika nchi, labda pamoja na akili hiyo hiyo kutoonwa kwa kukosa usalama wa kutokutembea ambako mkimbizi anaona. alikuwa anaishi kwa shida na uzao wake katika nchi yake mwenyewe. Pamoja na watoto wake Isaka na Yakobo, (ambao ahadi zilirudiwa kwao), "alikufa katika imani" asijapata ahadi , lakini akiisha kuziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni na wasafiri juu ya nchi" (Ebra. 11:13). ona hatua nne: -

 • Akizijua ahadi - kama tunavyofanya katika somo hili

 • Akiisha "Sadikishwa nazo" - kama zilichukua maendeleo ya ushawishi kwa Abrahamu, ni kiasi gani zaidi na sisi ?.

 • Kuzikubali kwa moyo - kwa kubatizwa katika Kristo (Gal. 3:27 -29).

 • Kukiri mbele ya ulimwengu kwa mwendo wetu wa maisha kuwa ulimwengu huu sio nyumbani kwetu hasa, bali tunaishi kwa kutumainia enzi ijayo duniani.

Abrahamu amekuwa shujaa wetu mkuu wa mfano kama tunafahamu mambo haya. mwisho wa kutambuliwa utimilifu wa ahadi ulikuja wakati wa baadae kwa mzee aliyechoka kwa mke aliyekufa; kwa kweli ilimbidi anunue kiwanja cha nchi ya ahadi kwa ajili ya kuzika (Mdo. 7:16). Hakika Mungu "hakumpa urithi ndani yake hata kiasi cha kuweka mguu: Lakini akaahidi kwamba atampa, iwe miliki yake, na ya uzao wake baadae alipokuwa hana mtoto" (mdo. 7:5). uzao wa Abrahamu uliopo sasa unaweza kuona kutopatana wanaponunua au kukodi miliki - duniani ambayo iliahidiwa kwao kuwa yao, urithi wa milele !.

Lakini Mungu anatunza ahadi zake. Itabidi ije siku hapo Abrahamu na wote ambao ahadi zilifanywa kwao watazawadiwa. Waebrania 11: 13, 39,40 neno limekazwa sana: -

"Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi; Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi".

Kwa hiyo Waaminifu wote watapewa thawabu kwenye kilele hicho hicho cha muda, yaani kwenye kiti cha hukumu siku ya mwisho (2 Tim. 4:1,8; math. 25:31 -34; 1 Petro 5:4). Kinachofuata ni yeye kuwako ili kuamuliwa, Abrahamu alikuwa na wengine waliozijua ahadi hizo itabidi wafufuliwe kabla ya hukumu. ikiwa sasa hawajazipokea ahadi ya kwamba watafanyiwa hivyo tu baada ya ufufuo wao na hukumu (yaani kuamuliwa na mwamuzi) Kristo atakaporudi, halipo shauri la pili bali kufahamu kuwa walio sawa na abrahamu kwa imani hivi sasa wamelala wakiwa hawana fahamu, wakisubiri Kristo arudi; Lakini vioo vilivyotiwa picha katika makanisa ya Ulaya yote imejulikana ya kuwa Abrahamu sasa yuko mbinguni, akipata thawabu kwa ajili ya maisha ya imani Maelfu ya watu kwa miaka mamia wameweka picha hizo za zamani, kwa dini wakikubali mawazo kama haya. Je ? utakuwa na ujasiri wenye misingi katika Biblia kuondika haraka nje ya hiyo jamii ?

Uzao (Mbegu)

Kama tulivyoelezwa katika somo la 3:2, ahadi ya uzao kwanza wamhusu Yesu na, Pili, kwa wale walio katika "Kristo" na kwa sababu hiyo nao vile vile wanahesabiwa kuwa ni uzao wa Abrahamu:-

 1. "Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki ….. na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa" (Mwa. 12:23)

 2. "Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi: hata mtu akiweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, Uzao wako nao utahesabika ….. Maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele" (Mwa. 13:15,16).

 3. "Tazama sasa mbinguni , hesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu …… Ndivyo utakavyokuwa uzao wako ….. Uzao wako nimewapa nchi hii (Mwa. 15:5,8)

 4. "Nami nitakupa ……. na uzao wako baada yako …… nchi ya Kanaani, kuwa miliki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao" (Mwa. 17:8)

 5. "Na katika kuzidisha nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchnga uliopo pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia" (Mwa. 22:17,18).

Tena, Abrahamu kufahamu "uzao" kwa kuendelea mbele kulipanuka: -

 1. Kwanza aliambiwa barabara ya kwamba kwa njia nyingine atakuwa na hesabu ya ajabu ya watoto, na kwa njia ya "uzao" wake dunia yote itabarikiwa.

 2. Baadaye aliambiwa ya kwamba atakuwa na uzao ambao utakuja kujumuisha watu wengi. Watu hawa watapata uzima wa milele, pamoja naye, katika nchi ambayo aliwahi kuifika, yaani Kaanani.

 3. Aliambiwa kuwa uzao wake utakuwa mwingi kama nyota za angani. Hii ahadi inaweza kuwa imedokezwa kwamba atakuwa na watoto wengi wa Kiroho (Nyota za mbinguni wengi sawa na wa mwili (kama "mavumbi ya nchi").

 4. Ahadi zilizotangulia zilitia mkazo wa nyongeza ya uhakika kuwa watu wengi watakao kuja kuwa sehemu ya uzao watakuwa na uhusiano wao na Mungu.

 5. Uzao utakuwa na ushindi juu ya adui yake.

Fahamu kuwa uzao utaleta "Baraka" zipatikane kwa watu walio juu ya uso wa dunia yote.Katika Biblia jambo la baraka mara nyingi limeungwa na kusamehewa dhambi. Isitoshe, huu ni mbaraka mkubwa zaidi wa kupenda Mungu unaoweza kuhitajika. Kwa hiyo tunasoma mabo kama "Heri (amebarikiwa) aliyesamehewa dhambi" (Zab. 32:1); "Kikombe kile cha baraka" (1Kor. 10:16), kinasema kikombe cha divai ambacho kinawakilisha damu ya Kristo kwa hicho msamaha unawezekana.

Mtoto pekee wa Abrahamu aliyeleta msamaha wa dhambi za ulimwengu, kwa kweli ni yesu, na ufafanuzi wa Agano Jipya juu ya Ahadi zilizofanywa kwa Abrahamu unatoa msaada madhubuti : -

"(Mungu) hasemi, kwa wazao, kana kwamba ni wengi, (yaani kwa wingi), bali kana kwamba ni mmoja, (katika mmoja), kwa mzao wako" yaani, Kristo (Gal. 3:16)

"….ambayo Mungu aliagana na baba zetu, akimwambia Abrahamu katika uzao kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa. Mungu akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabariki kwa kuwaepusha kila mmoja wenu na maovu yake" (Mdo. 3:25.26).

Ona hapa jinsi Petro anavyonukuu na kuifasiri Mwa. 22:18: -

Uzao = Yesu

Baraka = Msamaha wa dhambi.

Ahadi ya kuwa Yesu, uzao, atakuwa mshindi juu ya ahadi zake sasa inafaa zaidi kwa uzuri kuwa mahali ikiwa hii inasomwa kwa kutaja ushindi wake juu ya dhambi - Adui mkubwa zaidi wa watu wa Mungu, na kwa sababu hiyo naye Yesu, Pia.

KUJIUNGA NA UZAO

Kwa sasa itakuwa dhahiri kuwa mambo ya awali yaliyo ya msingi wa Injili ya Kristo ilieleweka kwa Abrahamu. lakini ahadi hizi muhimu zilikuwa kwa ajili ya Abrahamu na uzao wake, Yesu. Ni vipi ? kuhusu mtu yeyote mwingine ?. Hata walio wa ukoo wa mwili wa Abrahamu wao wenyewe kuwa hivyo hakuta mfanya mtu yeyote kuushiriki huo uzao mmoja maalum (Yoh. 8:39;Rum. 9:7). kwa njia nyingine yatupasa tuwe moyoni wa shirika wa Yesu, hivyo basi ahadi za mzao zitashirikishwa nasi vile vile. Hii ni kwa njia ya ubatizo katika Kristo (Rum. 6:3 -5); mara nyingi tunasoma ubatizo katika jina lake (Mdo. 2:38; 8:16; 10:48; 19:5). Wagalatia 3:27 -29 isingeweza kuweka maana yoyote iliyowazi:-

"Maana ninyi nyote (yaani mlio wengi tu) mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. hapana Myahudi wala Myunani (wa mataifa), hapana mtumwa wala huru, hapana mume wala mke; maana ninyi nyote mmekuwa mmoja (kwa kuwa) katika Kristo Yesu kwa ubatizo. na kama ninyi ni wa Kristo (kwa nia ya ubatizo katika jina lake), basi, mmekuwa uzao wa Abrahamu, na warithi sawa sawa na Ahadi".

Ahadi ya uzima wa milele duniani, kwa kupokea 'baraka’ ya msamaha kwa njia ya Yesu. Ni kwa kubatizwa katika Kristo, uzao, ambaye tunashirikishwa ahadi zilizofanywa kwake ; na hivyo Rum 8:17 inatuita sisi "Warithio pamoja na Kristo".

Kumbuka kuwa baraka ilikuwa inakuja juu ya watu wote toka pande zote za dunia , kupitia kwenye uzao; na uzao utakuja kuwa ni kundi la watu walioenea duniani pote, kama mchanga ulio kwenye ukingo wa bahari na nyota za mbinguni. kinachofuata ni kwamba hiki kinatokana na kupokea kwao kwanza baraka hivyo wanaweza kuwa uzao. Kwa hiyo uzao mbegu (moja) "Zitasimulia habari za Bwana kwa kizazi kitakachokuja" (yaani watu wengi ; Zaburi 22:30). Tunaweza kueleza kwa ufupi kuachwa ahadi mbili zilizotolewa kwa Abrahamu : -

1) NCHI

Abrahamu na uzao wake, Yesu, na wale walio ndani yake watairithi nchi ya Kaanani na kupanuka dunia yote, na kuishi humo milele. katika maisha haya hii ahadi hawakuipata, bali watapokea siku ya mwisho, Yesu atakaporudi.

2) UZAO

Kwanza kabisa huyu alikuwa ni Yesu. kwa njia yake dhambi ("Maadui") za watu ushindi utapatikana, hivyo basi mibaraka ya msamaha itafanywa ipatikane ulimwenguni pote.

Kwa kubatizwa katika jina la Yesu tunakuwa sehemu ya uzao .

Izi hizi njia mbili zinatokea katika mahubiri ya Agano Jipya, na sio ya kushangaza ni mara nyingi yameandikwa ya kwamba watu waliposikia wakiishafundishwa, wakati huo wakabatizwa. huu ulikuwa, na ndivyo ulivyo, mwendo ambao hizi ahadi zinaweza kufanywa kwetu. Tunaweza kuelewa ni kwa sababu gani, Mzee alipokabili kifo, Paulo aliweza kuainisha tumaini lake kuwa ni "tumaini la Israeli’ (mdo. 28:20): tumaini la kweli la mkristo ni tumaini la kwanza la Myahudi. Ufafanuzi wa Kristo ni kuwa "Wokovu watoka kwa wayahudi" (Yoh. 4:22) pia inabidi kutaja haja ya kuwa Myahudi wa Kiroho, hivyo basi tunaweza kufaidika kutoka kwenye ahadi za wokovu kwa njia ya Kristo ambazo ziliahidiwa kwa mababa wa Wayahudi.

Tunasoma ya kwamba Wakristo wa kwanza Walihubiri :-

 1. "Mambo yanayohusu ufalme wa Mungu na

 2. Jina la Yesu Kristo" (Mdo.8:12).

Haya yalikuwa ndiyo mambo mawili hasa aliyoelezwa Abrahamu mwanzoni mwa vichwa vidogo tofauti vya habari:-

 1. Ahadi zinazohusu nchi na

 2. Ahadi kuhusu uzao.

Angalia unapopita neno "Mambo" (yapo katika uwingi) yanayohusu Ufalme wa Yesu. yameelezewa kwa kifupi kuwa "akawahubiri Kristo" (Mdo. 8:5,12). yote hii mara nyingi imechukuliwa kuwa na maana "Yesu anakupenda ! sema bara bara unaamini alikufa kwa ajili yako nawe ni mtu uliyeokolewa !" Lakini fungu la maneno machache "Kristo" ni dhahiri linaelezea kwa ufupi mafunzo ya hesabu ya mambo kumhusu yeye na ufalme ujao. Habari njema kuhusu ufalme huu ambazo zilihubiriwa kwa Abrahamu zilihusika sehemu kubwa katika mahubiri ya kwanza ya Injili .

Katika mji wa Korintho, Paulo, "Kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu" (Mdo. 19:8); Katika efeso alikwenda huko na huko "Akihubiri ufalme wa Mungu" (Mdo. 20:25), na kazi yake kabla ya kufa kule Rumi ilikuwa ni ile ile "Akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sheria ya Musa na ya manabii" (mdo. 28: 23, 31). kama kuwepo mazungumuzo mengi mno ya karibu yanayoonyeshwa ya kwamba ujumbe wa msingi wa Injili kuhusu ufalme wa Yesu hayakuwa tu ni mambo ya kusema "Mwamini Yesu" ufunuo wa Mungu kwa Abrahamu ulieleza jambo moja moja zaidi kuliko hivyo, na mambo yaliyoahidiwa ndio msingi wa Injili ya mkristo wa kweli.

Tumeonyesha ya kuwa kubatizwa katika Jina la Yesu kunatufanya kuwa sehemu ya uzao na kwa sababu hii tunaweza kurithi ahadi (Gala. 3:27 -29), lakini ubatizo pekee hautoshi kutuwezesha kupata wokovu ulioahidiwa. yatupasa kubakia ndani ya uzao , katika Kristo, ikiwa tunataka kupokea ahadi zilizofanywa kwa uzao. Kwa hiyo ubatizo ni mwanzo unaostahili; tumeingia kwenye mbio ambazo zinahitajika wakati huo kukimbia. usisahau kwamba kuhusiana na uzao wa Abrahamu hauna maana kwamba tunakubalika mbele za Mungu. Waisraeli ni uzao wa Abrahamu kwa namna nyingine, Lakini hii haina maana kwamba wanaweza kuokolewa bila kubatizwa na kufuatisha maisha yao kwa Kristo na mfano wa Abrahamu; (Rum. 9: 7, 8; 4: 13,14). Yesu aliwaambia Wayahudi, "najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Abrahamu ; Lakini mnatafuta kuniua ….. kama mngekuwa watoto wa Abrahamu, mngezitenda kazi zake Abrahamu" (Yohana. 8:37,39), ambaye aliishi maisha ya kumwamini Mungu na Kristo, Uzao ulioahidiwa (Yoh. 6:29).

"Uzao" inabidi uwe na sifa za babu yake ikiwa tunataka kuwa uzao wa Abrahamu wa kweli basi yatupasa sio tubatizwe tu bali tuwe na imani hasa katika ahadi za Mungu, kama aliyokuwa nayo barabara kwa hiyo ameitwa "baba yao wote wanaoamini ….. ambao wanafuata vile vile nyanyo za imani hiyo ya baba yetu Abrahamu, aliyokuwa nayo" (Rum. 4:11,12) " Fahamuni basi, wale walio wa imani, hao ndio wana wa Abrahamu" (Gal 3:7).

Imani ya kweli inabidi ijionyeshe yenyewe kwa aina nyingine ya matendo kama sivyo, mbele za Mungu, sio Imani (Yakobo.2:17). Tumeonyesha wazi imani yetu katika ahadi hizi ya kuwa tumejifunza na kubatizwa kwanza, hivyo zinatuhusu sisi wenyewe (Gal 3:27 -29).Basi, unaziamini kweli ahadi za Mungu ?. Hili ni swali yatupasa hasa tujiulize katika maisha yetu yote.

AGANO LA KALE NA JIPYA

Itakuwa ni dhahiri kwa sasa kuwa ahadi kwa Abrahamu zinaeleza kwa ufupi Injili ya Kristo. Mkondo mwingine wa mkuu wa ahadi alizoahidi Mungu ulikuwa kwa Wayahudi katika maneno ya sheria ya Musa hizi alisema kuwa kama walikuwa watii kwenye sheria hii, basi wangebarikiwa katika maisha haya (Kum. 28). Haikuwepo moja kwa moja ahadi ya uzima wa milele katika huu mfululizo wa ahadi, au "agano". Hivyo tunaona kuwa kumekuwepo "Maagano" mawili yaliyofanywa:-

 1. Kwa Abrahamu na uzao wake , umeahidiwa msamaha na uzima wa milele katika ufalme wa Mungu Kristo ajapo. Ahadi hii pia iliahidiwa katika Edeni na kwa Daudi.

 2. Kwa Wayahudi kwenye kipindi cha Musa, wao waliahidiwa amani na furaha katika maisha haya ya sasa kama wangetii sheria ambazo Mungu alimpa Musa.

Mungu alimwahidi Abrahamu msamaha na uzima wa milele katika ufalme, lakini huu utawezekana tu kwa dhabihu ya Yesu. Kwa sababu hii tunsoma kuwa kifo cha Kristo msalabani kilithibitisha alichoahidiwa Abrahamu (Gal. 3:17; Rum 15:8; Dan. 9:27; 2Kor.1:20), hivyo damu yake imeitwa "Damu ya Agano Jipya" (Math. 26:28) Tulikumbuke hili kama Yesu alivyotuambia mara kwa mara tutwae kikombe cha divai, akiashiria mambo yake kutukumbusha mambo haya (Ona 1Kor. 11:25): "Kikombe hiki ni patano (Agano) Jipya katika damu yangu" (Luka. 22:20). Hakuna maana katika "kuumega mkate" kumkumbuka Yesu na kazi yake ila tukifahamu mambo haya.

Dhabihu ya Yesu imefanya msamaha wa dhambi na uzima wa milele katika Ufalme wa Mungu uwezekane. basi akafanya ahadi imara kwa Abrahamu; Yesu amekuwa mdhamini wa Agano lililo bora zaidi (Ebra. 7:22). Waebrania 10:9 yamsema Yesu "Aondoa la kwanza (Agano), ili kusudi alisimamishe la pili" hii inaonyesha ya kwamba Yesu alipothibitisha ahadi zilizofanywa kwa Abrahamu, aliliondoa Agano lingine, hilo lilikuwa ni agano lililotolewa kwa mkono wa Musa. mistari ambayo imenukuliwa kumhusu Yesu inaimarisha Agano Jipya kwa kufa kwake, inadokeza ya kuwa lilikuwepo agano la kale aliloondoa (Webra. 8:13).

Hii ina maana ya kwamba ingawa agano la kuhusu Kristo lilifanywa kwanza, halikuanza kutumika kamili mpaka alipokufa, kwa sababu hii limeitwa Agano "Jipya". Lengo la Agano la "Kale" lililofanyika na Musa lilikuwa likionyesha mbele kwenye kazi ya Yesu , na kuupa mkazo umuhimu wa kuamini ahadi kuhusu Kristo

(Gal. 3:19,21). Kwa kinyume, kumwamini Kristo kunathibitisha ukweli wa sheria aliyopewa Musa (Rum.3:31). Ya kupendeza kwa kuwa ya zamani, Paulo anaielezea kwa maneno machache: "Torati imekuwa (Mwalimu) kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani" (Gal. 3:24). Ni kusudi hili hata torati iliyokuja kwa mkono wa Musa imehifadhiwa, na bado inatusaidia kujifundisha.

Kwanza unaposema mambo haya sio mepesi kuyaelewa; tunaweza kueleza kwa maneno machache kama ifuatavyo: -

Ahadi za kumhusu kristo zilifanywa kwa Abrahamu - Agano Jipya.

Ahadi kwa Israeli zilijumuisha torati aliyopewa Musa - Agano la Kale.

Kifo cha Kristo. Agano la Kale likaisha (Kol. 2:14 -17) Agano Jipya likaanza kutumika.

Ni kwa sababu hii mambo kama kutoa fungu la kumi,kutonza sabato n.k, ambayo yalikuwa ya Agano la Kale , siyo ya lazima siku hizi - ona somo la 9.5. Agano Jipya litakujafanywa kwa Waisraeli wa kuzaliwa watakapotubu na kumkubali Kristo. (Yer. 31:31,32 ; Rum. 9:26,27; Ezek. 16:62; 37:26), Ingawa, kwa kweli Myahudi yeyote afanyaye hivyo na kubatizwa katika jina la Yesu, anaweza kwa mara moja kuingia kwa Agano Jipya (ambalo halimtofautishi Myahudi /mtu wa mataifa -Gal 3: 27 -29).

Hakika kufahamu mambo haya kunatufanya tutambue ukweli wa ahadi za Mungu. Wenye mashaka juu ya mafundisho ya dini walilaumu isivyo haki wahubiri wa Kristo wa kwanza kwa kutotoa ujumbe wa kweli. Paulo alijibu kwa kusema kwamba kufa kwake Kristo ni uthibitisho wa ahadi za Mungu, tumaini walilosema halikuwa jambo la kugusa na kisha kwenda, bali lilikuwa ni toleo la uhakika kabisa: - "Lakini kama Mungu alivyomwaminifu, neno letu (la kuhubiri) kwenu halikuwa ndiyo na siyo. Maana mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, ….. hakuwa ndiyo na siyo, bali katika yeye ni ndiyo. Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo, tena katika yeye ni, Amini" (2 Kor.1:17 -20). Kwa kweli huu mwenendo haufanyi kazi wa,'Vyema’, nadhani kunaweza kuwa na ukweli fulani katika hayo yote ……." ?.


  Back
Home
Next