Misingi Ya BIBLIA
Somo La 3: Ahadi za Mungu
Dibaji | Ahadi Katika Edeni | Ahadi Kwa Nuhu | Ahadi Kwa Abrahamu | Ahadi Kwa Daudi | Tumeacha Kitambo sehemu ya (The Kuharibiwa kwa Mbingu na Nchi (Ufu. 21:1; 2Pet. 3:6-12)., Madai ya "Uisraeli wa Visiwa vya Uingereza") | Maswali

3.2 Ahadi Katika Edeni

Kisa cha kutia huruma cha kuanguka mtu kimetajwa mwanzo sura ya 3. Nyoka alilaaniwa kwa kunukuu vibaya neno la Mungu na kumjaribu Eva kirahisi. kwa kutokutii kwao mwanaume na mwanamke waliadhibiwa. lakini mwanga wa tumaini unaingia ndani ya picha hii yenye giza Mungu alipowaambia Nyoka: -

"Nami nitaweka Uadui (kuchukua upinzani) kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake: huo (Uzao wa mwanamke) utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino" (Mwanzo. 3:15).

Huu mstari kwa kirefu umeongeza nguvu; tunahitajika kupambanua kwa makini mambo mbali mbali yaliyohusishwa. "Uzao maana yake mwana au mtoto, lakini vile vile unaweza kutaja watu waliojumuika na "Uzao" mmoja. Tutaona baadae ya kuwa "Uzao" wa Abrahamu alikuwa ni Yesu (Gal.3:16), lakini ni kwamba kama tukiwa "Ndani" ya Yesu kwa njia ya Ubatizo, Basi vile vile tumekuwa na uzao (Gal. 3:27 -29). Hili neno "Uzao" pia linatajwa jambo la mbegu (1 Pet. 1:23); hivyo uzao wa kweli utakuwa na tabia ya sifa ya Baba yake.

Uzao wa Nyoka inabidi basi utajwe ule ulio na jamii ya kufanana na Nyoka:-

  • Unaharibu maana ya neno la Mungu

  • Unadanganya

  • Unawaongoza wengine katika kutenda dhambi.

Tutaona katika somo la 6 kuwa hayupo mtu halisi anayefanya hivi, bali ndani yetu sisi upo.

  • "utu wetu wa kale " wa mwili (Rum.6:6)

  • "Mwanadamu wa tabia ya asili" (1 Kor.2:14)

  • "Utu wa zamani, unaoharibika (Unaooza) kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya" (Efe. 4:22).

  • "Utu wa kale pamoja na matendo yake" (Kol.3:9).

Huu utu wa dhambi ulio ndani yetu ni "Ibilisi" wa kwenye Biblia, uzao wa nyoka.

Uzao wa mwanamke ulikuwa uwe ni mmoja dhahiri - "utamponda (uzao wa nyoka) kisigino" (Mwa.3:15) huyu mtu alikuwa daima akiuponda uzao wa nyoka, yaani dhambi -"Utakuponda kichwa". Kumpiga nyoka kwenye kichwa ni pigo la mauti kwa kuwa ubongo wake umo kichwani mwakeMtu pekee anayefaa heshima ya kuwa uzao wa mwanamke inampasa awe ni Bwana Yesu:

"Yesu Kristo, ambaye (kwa msalaba) ameondoa mauti (na hivyo ni nguvu ya dhambi - Rum.6:23) na kuufunua uzima na kutoharibika kwa ile Injili" (2 Tim. 1:10).

"Mungu kwa kumtuma mwanae mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili" yaani Ibilisi wa Biblia, Uzao wa nyoka (Rum. 8:3)

Yesu "alidhihirishwa ili aziondoe dhambi zetu" (1Yoh. 3:5).

"Nawe utamwita jina lake Yesu (maana yake 'Mwokozi’): maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao" (Math.1:21).

Yesu mwenyewe "alizaliwa na mwanamke" (Gal. 4:4) akiwa ni mwana wa Mariamu, Ingawa Mungu alikuwa ni Baba yake. Hivi kwa maana hii, pia, alikuwa ni uzao wa mwanamke, ingawa alitolewa na Mungu kwa namna ambayo hakuna mtu amewahi kutokea wa jinsi hiyo. huu uzao wa mwanamke uliumizwa kidogo na dhambi, uzao wa nyoka - "Utakuponda kisigino" (Mwa. 3:25). Nyoka akiuma kisigino kwa kawaida ni kuumia kwa muda, kukilinganishwa na siku zote kumponda nyoka kichwani. Mifano mingi ya misemo ina asili ya Biblia: "Mponde Kichwani" (Yaani kukikomesha kitu kabisa) labda msingi wake ni kwenye unabii huu wa Yesu akimponda Yesu kwenye Kichwa.

Kuihukumu dhambi, uzao wa nyoka, kwanza ilikuwa kwa dhabihu ya Kristo msalabani - fahamu jinsi mistari ilivyonukuliwa inavyousema ushahidi wa Kristo juu ya dhambi kwa wakati uliopita. maumivu ya muda kwenye kisigino aliyoyapata yesu, basi, kinatajwa kifo chake kwa siku tatu. Ufufuo wake ulithibitisha kuwa maumivu yalikuwa ni ya muda tu, ukilinganisha na pigo la mauti aliloipa dhambi. inavutia ya kwamba hakuna taarifa ya historia ya Biblia inayoonyesha ya kwamba watu wa kusulubiwa walipigiliwa misumari visigino vyao kwenye gogo la mti. Hivyo Yesu "alichubuliwa kisigino" kwa kifo chake. Isaya 53: 4 -5 yaeleza kristo "alichubuliwa" na Mungu kwa kifo chake msalabani. Hii ni wazi inataja unabii wa Mwa.3:15 kuwa Kristo alipondwa na uzao wa nyoka. Walakini mwishowe Mungu alitenda haki kwa mabaya aliyokabiliwa nayo Kristo, amesema hapa kuwa anamchubua (Isaya 53:10) kwa ajili ya kutawala nguvu ya mabaya yaliyomchubua mwanae. Hivyo pia Mungu anatenda kazi kwa mabaya kila anayoyapata mtoto wake.

PIGANO LA LEO

Lakini swali linaweza kuwa limezuka akilini mwako: "Ikiwa Yesu amebatilisha dhambi na mauti (uzao wa nyoka) ni kwa nini mambo hayo bado yapo leo ?" Jibu ni kwamba msalabani Yesu aliangamiza nguvu ya dhambi ndani ya nafsi yake mwenyewe: Unabii wa Mwa. 3:15 ni wa kwanza kumhusu Yesu kupingana na dhambi. Sasa hii inamaanisha ya kwamba kwa kuwa ametualika kuushiriki ushindi wake, hatimaye, nasi pia, tunaweza kushinda dhambi na mauti.

Wale ambao hawajaalikwa kuushiriki ushindi wake , au wanaokataa anapowapa, bila shaka, bado watapata dhambi na mauti. Ingawa dhambi na mauti vinawapata waamini wa kweli, kwa kuunganika kwao na uzao wa mwanamke kwa njia ya ubatizo katika Kristo (Gal. 3:27 -29) wanaweza kusamehewa dhambi zao na kwa hiyo hatimaye wataokolewa toka kwenye mauti, ambayo ni matokeo ya dhambi. Hivyo kwa kuangalia mbele"alibatilisha mauti" msalabani (2Tim.1:10), ingawa sivyo mpaka kusudi la Mungu kwa dunia liwe limekamilika mwishoni mwa baada ya miaka ya elfu hapo watu watakapo koma kufa - mauti hayatashuhudiwa tena juu ya dunia: "maana sharti amiliki yeye (kwa sehemu ya kwanza ya ufalme wa Mungu) hata awawekee maadui wake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti" (1 Kor 15:25,26).

Kaama "ukibatizwa katika Kristo" basi ahadi kumhusu Yesu, kama zile za mwanzo 3:15, zinakuwa zetu wenyewe; haziwi tena sehemu za kuvutia tu za Biblia, ni unabii na ahadi zilizofanywa kwetu moja kwa moja ! kama uzao wa mwanamke nasi pia, tutapata ushindi wa dhambi juu yetu kwa muhula mfupi. Bwana asiporudi wakati wetu tukiwa hai, nasi pia tutapondwa kisigino kama Yesu, ni kwamba nasi pia tutakufa. Lakini kama kweli tu uzao wa mwanamke , wakati huo hilo "Jeraha" litakuwa ni la kitambo tu. waliobatizwa vema katika kristo kwa kuzamishwa ndani ya maji, wanaunganika wenyewe na mauti yake na ufufuo - kunakoashiria kwa kutoka katika maji (Ona Rum. 6:3-5).

Kama tukiwa ni uzao wa mwanamke , basi maisha yetu yatarudisha mfano wa maneno ya Mwa 3:15 - daima kutakuwepo na akili ya kupigana ("Uadui") ndani yetu, kati ya haki na uovu. Paulo mtume kubwa ameeleza karibu ugonvi wa akilini katika kupingana kati ya dhambi na moyo wake halisi ambao ulichafuka ndani yake (Rum. 7:14 -25).

Baada ya kubatizwa katika Kristo, pigano hili na dhambi ambalo ni tabia ya kawaida ndani yetu litaongezeka na kuendelea kufanya hivyo siku zetu zote. Kwa akili ni vigumu kwa sababu nguvu ya dhambi ni kubwa. lakini kwa maana nyingine sivyo, kwa kuwa tumo ndani ya Kristo, ambaye tayari amepigana na kulishinda pigano. Fahamu jinsi waaminio walivyosemwa wao ni mwanamke katika Waefeso 5:23 -32, kana kwamba kwa kuwa uzao wa mwanamke vile vile tu mwanamke.

Kwa jinsi hiyo hiyo kama uzao wa mwanamke unamaanisha wawili Yesu na hao wanaojaribiwa kuwa na tabia ya kuwa na sifa yake, basi uzao wa nyoka unasemwa sehemu mbili dhambi ("Ibilisi"wa kwenye Biblia) na hao ambao kwa hiari wanaonyesha tabia ya dhambi na nyoka.Watu hawa hawatojari au hawatatoa maana nzuri ya neno la Mungu , ambalo mwishowe litawapeleka katika aibu ya dhambi na kutengwa na Mungu, Jambo lililotokea kwa Adamu na Hawa. Kwa kuwa Wayahudi walikuwa watu hasa walomuua Yesu -Yaani waliuponda uzao wa mwanamke kwenye kisigino - itegemewe ya kuwa walikuwa ni mifano mkubwa wa uzao wa nyoka. Hii imethibitishwa na Yohana mbatizaji na Yesu: -

"Hata alipowaona wengi (Yohana) miongoni mwa mafarisayo na masadukayo (kundi la Wayahudi waliomhukumu Yesu) wakiujia ubatizo wake, aliwaambia enyi uzao wa nyoka ,(Yaani wanaume na wanawake wameumbwa na) Nyoka nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja ?" (Math. 3:7)

"Basi Yesu akijua mawazo yao (Mafarisayo), akawaambia ….. Enyi wazao wa nyoka , mwawezaje kunena mema , mkiwa wabaya ?" (Math.12:25,34).

Ulimwengu - hata ulimwengu wa dini - una tabia hizi hizi za nyoka. waliobatizwa tu katika Kristo hao tu wameunganika na uzao wa mwanamke; wengine wote, wana viwango vinavyopishana, vya mbegu za nyoka. Jinsi Yesu alivyowatendea watu ambao walikuwa mbegu ya nyoka inabidi uwe ni mfano wetu: -

Aliwahubiri kwa roho na upendo na ipasavyo kweli, lakini

Njia zao na fikira havikumvuta, na

Aliwaonyesha tabia ya upendo ulio na Mungu kwa njia aliyoishi.

Lakini kwa yote hayo walimchukia. Bidii yake mwenyewe kuwa mtiifu kwa Mungu kuliwafanya kuwa na wivu. Hata jumla zake (Yoh. 7:5; Marko. 3:21) na marafiki wa karibu (Yoh. 6:66) waliweka vikwazo na wengine wakamwacha na kwenda zao. Paulo alipata jambo hilo hilo alipowalilia waliowahi kusimama pamoja naye katika makubwa na madogo:-

"Je ! nimekuwa adui wenu kwa sababu nawambia yaliyo ya kweli ?" (Gal. 4:14 -16).

Kamwe ukweli sio wa wote; kuujua na kuishi kwa huo kama inavyopaswa siku zote huleta aina nyingine ya matatizo kwetu, hata kusababisha maudhi:-

"kama vile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomuudhi yule aliyezaliwa kwa roho (Kwa elimu ya kweli ya neno la Mungu -1 Petro.1:23), ndivyo ilivyo na sas" (Gal. 4:29).

Ikiwa kwa kweli tumeunganika na kristo yatupasa kuonja mateso yake mengine, hivyo basi tutaweza pia kushiriki katika thawabu yake yenye utukufu. tena Paulo anatuwekea mfano usio na kifani kwa hili:-

"Ni neno la kuaminiwa: kwa maana , kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia (kristo); kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; ….. (2 Tim. 10 -12).

"Ikiwa waliniudhi mimi (Yesu), watawaudhi nanyi pia ……Mambo yote haya watawatendea kwa ajili ya jina langu" (Yoh. 15:20,21)

Yaani, kwa sababu tumebatizwa kwa jina la Yesu (Mdo 2:38;8:16).

Kukubaliwa na mistari kama hii, inajaribu kuleta sababu, "kama huko ndiko kuungana na Yesu, Uzao wa mwanamke, yahusika mambo yote, nisingependa hata kidogo" Lakini bila shaka hatutategemea kuingia jambo lolote ambalo hatuwezi kwa maana ya kushindana nalo. Wakati wa kujitoa nafsi ni dhahiri unatakiwa ili kutuunga wenyewe kabisa na Kristo, Sisi kuungana naye tutasababisha thawabu hii yenye utukufu "Kwani mateso ya sasa hayawezi kulingana na utukufu utakaodhihirika kwetu" Na hata sasa dhabihu yake inawezesha maombi yetu tusaidiwe katika masumbufu ya maisha kuwa hasa yenye nguvu kwa Mungu. Na nyongeza kwa hili yafuatayo ni matumaini yenye utukufu, kwa uzito yameelekezwa katika Biblia nyingi za Kristadelfiani:-

"Mungu ni mwaminifu, ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na hilo jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili" (1Kor. 10:13)

"hata (mambo) nimewaambieni mpatekuwa na amani ndani yengu. Ulimwernguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinnda ulimwengu" (Yoh. 16:33)

"basi, tuseme nini juu ya (mambo) hayo ? Mungu akiwepo upande wetu, ni nani aliye juu yetu ?" (Rum. 8:31).


  Back
Home
Next