Misingi Ya BIBLIA
Somo La 2: Roho ya Mungu
Ufafanuzi | Maongozi ya Mungu | Vipawa Vya Roho Mtakatifu | Kurudishwa kwa vipawa | Biblia ni Mamlaka pekee | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Je! Roho Mtakatifu ni Mtu?, Kawaida ya kuita kitu kana kwamba ni Mtu, Mambo ya kelvini, "Nanyi mtapokea Roho mtakatifu", "Na ishara hizi zitafuata") | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 8: "Na ishara hizi zitafuata"

Neno hili limekazwa, ya kwamba kila mtu aaaminiye kweli atapokea karama zenye miujiza. Lakini hili linathibitisha mno -"Watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono juu ya wagonjwa, nao watapona" (Marko 16:18). Hii si ahadi ya mambo ambayo kinadharia yaweza kutokea ikiwa aaminiye alikuwa na imani ya kutosha; hizi zilikuwa ahadi za uhakika kwa udhahiri kitakachofanywa na Waaminio. Ishara hizi zilipofanywa kwa uwazi, ahadi ya mstari huu haiwezi kutuhusu sisi kwa wakati uliopo. Unaweza kukumbuka jinsi Paulo aliweza kumshika nyoka mwenye sumu bila kugongwa (Mdo. 28: 3 -7), uthibitisho wa mahubiri yake ukatokea ya kuwa yametoka kwa Mungu.

Wakristo wa madhehebu yaitwayo yote ya kiroho waliodai kuwa na karama kipindi cha wakati uliopita miaka mia moja iliyopita, haukuwepo ushuhuda wenye ukweli wa nguvu hizi kutendwa. Kila aaminiye asipoweza kuonyesha ishara za ukubwa huu, ahadi hii haitahusu leo. Hii inatuacha na dhana tuliyoileta toka kwenye uchunguzi wetu kwa Biblia ifundishayo kuhusu Roho: hizi karama zenye miujiza zilikuwa na wakristo wa kwanza katika karne ya kwanza, lakini zilikoma kushikwa baada ya Agano Jipya maandiko yake kukamilika.

Aya ya mwisho kwa Marko 16 inadokeza kuwa miujiza "itafuatana" na hao walioamini kwa madhumni maalum ya kuthibitisha neno la Injili lililosemwa "Ishara zitafuatana na hao waaminio …….. wakaenda na kuhubiri kila mahali, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kuthibitisha neno kwa ishara zilizofuatana nalo"

(Marko 16:17,20). Mara neno lililotamkwa likaandikwa kwa ukamilifu, kama tulivyonalo sasa katika Agano Jipya, hapakuwa na haja ya Ishara za Miujiza kuwafuata wale walioamini.

Maelezo yaliyoandikwa chini ya Ukurasa :

Siku hizi yameenea mno madai ya kuwa na karama za Roho ya kwamba katika mwaka 1989 mijadala miwili ya halaiki ilifanyika kati ya mchungaji wa dhehebu la kiroho, Yohana Liliekas, na Wakristadelfiani wawili; Bwana John Allfree na mwandishi wa sasa. Mwendo ulikuwa: "Je ! karama zenye miujiza ya Roho Mtakatifu wanayo watu leo?" Mwaliko ulitumwa kwenye makanisa mengi ya U.K; ukatokea mkutano wa watu walioungana zaidi ya watu 1000. Inastahili kusadiki ya kwamba' Ushuhuda’ mzuri sana wenyekuwa na karama ungeonyeshwa. Nakala ya Habri inapatikana toka kwa :

CHRISTADELPHIAN ADVANCEMENT TRUST PO Box 3034 South Croydon SURREY CR2 0ZA ENGLAND


   Back
Home
Back