Misingi Ya BIBLIA
Somo La 2: Roho ya Mungu
Ufafanuzi | Maongozi ya Mungu | Vipawa Vya Roho Mtakatifu | Kurudishwa kwa vipawa | Biblia ni Mamlaka pekee | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Je! Roho Mtakatifu ni Mtu?, Kawaida ya kuita kitu kana kwamba ni Mtu, Mambo ya kelvini, "Nanyi mtapokea Roho mtakatifu", "Na ishara hizi zitafuata") | Maswali

2.4 Kurudishwa kwa vipawa

Vipawa vyenye miujiza ya Roho ya Mungu vitatumika tena na waumini ili kwamba ulimwengu huu wa sasa ubadilishwe uwe Ufalme wa Mungu, Kristo atakaporudi. Basi vipawa vimetajwa Kuwa ni 'Nguvu za zamani (Zama) zijazo’ (Ebr. 6:4, 5); naye Yoeli 2: 26 -29 umwagaji mkubwa wa karama baada ya toba ya Israeli. Uhakika sana wa kwamba vipawa hivi watapewa waaminio Kristo akirudi ni ushuhuda wa kutosha ya kwamba kwa sasa vipawa watu hawana - Kwa kuwa Mkristo awaye yote mwenye macho yaliyo wazi pande zote mbili Maandiko na matukio ya ulimwengu, ni hakika kurudi kwa Bwana inabidi kuwa amekaribia sana (tazama yaliyo mwisho wa kitabu cha 3).

Upo Unabii dhahiri wa Biblia kama katika maana fulani kwa kipindi cha kati ya karne ya kwanza, vipawa vilipokuwepo, na kuja mara ya pili ilibidi vipawa vya Roho viondolewe:-

" ……Ukiwepo Unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwepo maarifa, yatabatilika. kwa maana tunafahamu kwa sehemu (yaani, nusu); na tunafanya Unabii kwa sehemu; lakini ijapo ile iliyokamili,iliyo kwa sehemu itabatilika (yaani, kuondolewa)". 1 Kor. 13:8 -10 - Karama za Roho zilikuwa za muda tu.

Karama za Roho walizokuwa nazo katika karne ya kwanza ilibidi ziondolewe 'Ilipokuja ile iliyokamili’ Hii si kuja mara ya pili Kristo, kwa Kuwa kipindi hicho karama za Roho zitatolewa tena. Neno la Kiyunani lililotafsiriwa'Kamili’ maana yake hasa ni kile ambacho kimetimilika au Kizima; akimaanishi kwa lazima Kuwa ni kitu kingine kisicho na dhambi.

Hiki kitu kizima kitaingia mahali palipo na maarifa yaliyo kwa sehemu ambayo Wakristo wa kwanza walikuwa nayo kama tokeo la Kuwa na kipawa cha kutoa Unabii. Kumbuka kwamba kutoa unabii kilikuwa ni kipawa cha kutabili maneno yenye kuvuviwa na Mungu ; ni taarifa iliyoandikwa ya maneno haya yanayoifanya Kuwa Biblia.

Kwenye karne ya kwanza, Muumini wa kawaida alijua sehemu ndogo tu ya Agano Jipya kama tunavyolijua. Alisikia maneno mengine ya Unabii toka kwa wazee wa kanisa lake juu ya matukio mbali mbali ya matendo ; aliweza kujua vema juu ya maisha ya Yesu, na aliweza kusikia vema barua moja au mbili za Paulo zikisomwa kwa sauti. Lakini mara taarifa ilipoandikwa ya maneno ya Unabii na kuweza kutimilika na kugawanywa, hapakuwepo na haja ya kipawa cha kutoa Unabii kiendelee wawe nacho. kile ambacho kilikuwa kamili, kwa sababu hiyo kilichoingia mahali pa huduma ya karama ya Roho,

basi likawa ni Agano Jipya lililotimilika:-

"Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe kamili (ametimilika)" 2 Tim. 3:16 -17.

Kile ambacho kinafanywa kuwa kamili, au kutimilika, ni'Maandiko yote’; hivyo mara'Maandiko yote’ yalipovuviwa na kuandika, " Kile ambacho kilikuwa kamili" kikawa kimekuja, nazo karama zenye miujiza zikaondolewa.

Waefeso 4: 8 -14 yaweka sasa wazi kikamilifu sawia fumbo lisiloeleweka vema:-"(Yesu) alipopaa juu (katika mbingu), ….akawapa wanadamu vipawa (vya Roho) ….. kusudi mwili wa Kristo ujengwe: hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani (yaani, Imani moja), na kumfahamu sana mwana wa Mungu, hata Kuwa mtu mkamilifu …. Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu".

Vipawa vya karne ya kwanza vilitolewa hadi mtu alifikia kukamilika au apevuke, (yaani, akomae) nao waraka wa 2 Tm. 3:16- 17 unasema ya Kuwa " Hadi mtu wa Mungu awe kamili" kwa kufahamu mwongozo wa 'Maandiko yote’ Tena, Kol. 1:28 unatufundisha ya kwamba 'Ukamilifu’ huja kwa kuitikia katika Neno la Mungu. Mara maandiko yote yakishikwa. Hakuna udhuru kweli wowote tena wa kukatizwa na wingi wa mafundisho yatolewayo na makanisa mbali mbali. Ipo biblia moja tu, na Kuwa

"Neno lako ndiyo kweli" (Yoh. 17:17), kwa kujifunza katika kurasa zake tunaweza kufikia "Umoja wa imani", imani moja ambayo Efe. 4:13 inaizungumzia. kwa hiyo wakristo wa kweli wamefikia kuishika hiyo imani moja; kwa maana hiyo wametimilika (wamekuwa'Kamili’) kwa kutokana na 'kile ambacho ni kamili’ au kimetimilika, Neno la Mungu lote - lililoandikwa.

Kwa kupita, tazama ni jinsi gani Efe. 4:14 unalinganisha kuwa chini ya utumishi wenye karama za miujiza, na utoto kiroho; na kwa maneno yenyewe ya kutoa unabii, namna karama zenye miujiza zilipoondolewa. 1 Kor. 13:11 unasema hayo hayo. Kufanya makelele haya kuhusu kuwa na karama za roho, basi si ishara ya kukomaa kiroho. Kusonga mbele kila msomaji wa maneno haya kufanye sasa kuelekea kufahamu kwa kina neno la Mungu lililoandikwa. Na kufurahia utimilifu wa msingi wa ufunuo wa Mungu mwenyewe ndani yake kwetu, kwa kuitikia neno katika Utii wa kunyenyekea.

KADHIA ZILIZOPO ZENYE KUWA NA ROHO

Hatimae, hesabu ya maana nyingine inabidi ifanywe kuhusu kadhia zilizorudiwa za hao wadhaniao wana vipawa vyenye miujiza sasa:-

-"Wanenao kwa lugha" siku hizi wanaelekea kurudia rudia maneno yale yale mafupi zaidi na zaidi tena, k.m. "lala, lala, lala, shama, shama. Yesu, Yesu ……" huu sio mpangilio uliojumuika na maneno ya lugha yoyote; mtu akimsikia mwingine akinena katika lugha ngeni, mara kwa mara inawezekana ya Kuwa wanaongelea jambo fulani kwa mfano mzuri wa matamshi ambao watu hutumia, ingawa hatuwezi kuyaelewa maneno hayo. Lakini wanenao lugha siku hizi hawaangalii jambo hili, uhakika ni kwamba lugha wanenayo haijengi kanisa, ambapo hiyo ilikuwa shabaha ya kutolewa karama kwenye karne ya kwanza.

-Wapentekosti wengine wanatoa kadhia ya kwamba kunena katika lugha ni ishara ya Kuwa 'Wameokoka’na kwa sababu hii kila mwongofu wa kweli hii ishara itafuatana naye. Kadhia hii inagongana na ugumu wa maelezo kuhusu makanisa ya kwanza ulikuwa mwili, ambapo wale wanaomiliki karama tofauti - tofauti walikuwa kama viuongo mbali mbali. si kila mtu alikuwa mkono au mguu, na vivyo hivyo si kila mmoja alishika kipawa kimoja chochote, k.m Lugha. 1Kor.12:17, 27 -30 mistari hii yote inabainisha wazo hili:-

"Kama mwili wote ukiwa jicho, kuwapi kusikia ? kama mwili mzima ni sikio kuwapi kunusa ? …. Basi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. Na Mungu amewaweka wengine katika kanisa , wa kwanza Mitume, wa pili Manabii, wa tatu Waalimu, kisha Miujiza, kisha karama ya kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za Lugha. Je! wote ni Mitume ? wote ni Manabii.? Wote wana karama za kuponya wagonjwa ? wote wanena katika lugha ? wote wafasiri.

Awali, maana hiyo hiyo imeonyeshwa katika mlango huo:-

"Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho yule yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine Unabii; na mwingine kupambanua Roho; mwingine aina za lugha; mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. Maana kama mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo" (1Kor. 12: 8 -12)

Mkazo wa jinsi hii hauwezi kutoangaliwa:-

Shida nyingine kwa ubishi wa Mpentekosti ni kwamba Filipo aliwaongoa watu wengi katika mji wa Samaria - yaani, walibatizwa katika maji baada ya kuelewa Injili, lakini hawakupokea karama za Roho; kwa Kuwa baada ya hivi, Petro na Yohana waliwaendea " ….. Waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu …. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao waka mpokea Roho Mtakatifu …..Simoni aliona Kuwa watu wanapewa vipawa vya Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono yao mitume" (mdo. 8: 4 -18). inawezekana kwamba kupewa vipawa vya Roho ilikuwa ni kuwekewa mikono juu yao tu, tendo ambalo Wapentekosti hawalifanyi mara nyingi siku hizi.

Wapentekosti wengine wanasema kwamba kunena kwa lugha si ushahidi wa kuwa umeokoka. Huu ni ukweli unaojitokeza kuwa ipo tofauti kubwa ya mafundisho kati ya wenye kadhia ya kushika vipawa. Baadhi ya watu wa 'Kiroho’ huamini kwamba ufalme wa Mungu utakuwa duniani, ambapo wengine wanasema utakuwa mbinguni. Wakatoliki 'wa Kiroho’ wanasema kwamba Roho Mtakatifu anawaambia wamwabudu Bikira Maria na Papa, wakati wapentekoste wengine 'wa Roho’ wanasema ya kwamba wao huongozwa na Roho Mtakatifu anayewaamuru wamkane Papa, wamwone kuwa yeye ni mnyama na mpinga Kristo, wanapinga mafundisho ya Katoliki. Hata hivyo Yesu alisema pasipo shaka kwamba wale walio na msaidizi, " ambaye ni Roho Mtakatifu" wataongozwa 'kwenye kweli yote’ ….tena siku ile (hamtahitaji) kuuliza neno lolote …..Msaidizi …..atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia" (Yoh. 16: 13,23; 14: 26).

Usingekuwepo Mgawanyiko wowote katika mafundisho ya msingi miongoni mwao wenye kuwa na msaidizi - uhakika ni kwamba upo, unaonyesha kwamba wale wanodai wanaye hawamchukui kwa kusema kweli. Udhaifu umeonekana kwa baadhi ya hao wasemao ya kuwa wenye msaidizi, Katika Biblia ili kuthibitisha imani zao lakini wanaonekana kwamba hawajaongozwa katika kweli yote na maarifa kabisa ya msaidizi.

-Umuhimu mkubwa uliofuatana na baadhi kwa kunena katika lugha haupo sawa na taarifa za Biblia. Orodha ya vipawa katika Waefeso 4:11 haitaji, orodha kama hii inatokea chini katika 1 Kor.12: 28 -30. kwa kweli, zipo nafasi tatu pekee zilizoandikwa katika Agano Jipya mahali ambapo kipawa kilitumika (mdo. 2:4; 10:46; 19:6).

Madai ya kunena katika lugha na kufanya miujiza kulikotimizwa na Wakristo wa roho siku hizi inabidi yapimwe karibu na taarifa yenye maana ambayo tumeiandika katika somo hili kuhusiana na kazi ya Roho Mtakatifu. Kutengeneza maana yenye msingi ni kwamba lolote ambalo watu hawa wamelitimiza, haliwezi kuwa ni tokeo la wao kuwa na Roho Mtakatifu. Yeyote aletaye sababu za kusaidia mashauri ya kuwa wanamiliki karama za Roho, anayo kazi kubwa ya kufanya ili kujibu maneno ya Biblia tuliyotoa.

Ingawa hiyo ni sababu yenye maana katika kutazamia baadhi ya maelezo ya sababu gani uzushi wa kuponya kwa sehemu na kunena kwa'Lugha’ (Kwa mtindo wa kunena kwa kupayuka - payuka) hutokea.

Imefahamika kwamba wanadamu hutumia sehemu ndogo ya nguvu ya ubongo wao - chini ya 1%, kulingana na makadirio mengine. Tena, akili (Moyo) imetambuliwa kuwa inaweza karibu kutawala viungo vya mwili; hivyo kwa nguvu zao za mwili hivyo huamini kuwa moto hauwezi kuunguza, Wahindu wametembea juu ya moto nyayo zao zikiwa wazi bila kuungua. kwa vipindi vya kuchochewa, upo uwezekano wetu kutumia asilimia kubwa ya uwezo wa ubongo wetu kuliko kawaida, na kwa sababu hiyo kuwa na uwezo ya kutimiza matokeo ya viungo juu ya mwili wetu unapokuwa nje ya matendo ya kawaida. Hivyo, kwa kuchochewa na mapigano, askari anaweza kutojua kabisa kuwa mkono wake umekatika mpaka muda wa baadae.

Imani ya dini kuwa katika hali ya moto na msisimko unaoamshwa na nyimbo fulani, na mvuto wa kiongozi wa kiroho, inawezekana kabisa mambo yaliyo nje ya miliki ya kawaida kwa mwanadamu yatatokea.'Miujiza’ iliyodaiwa kufanywa na'Wakristo’ wa leo ni ya mpango mmoja isiyofuata utaratibu kama ya majaribio ya dini nyingine; Vivyo hivyo hata dini ya waabudu uchawi imejaribu mambo hayo hayo ya kunena kwa kupayuka - payuka, Waislamu vile vile wanaweza kutumik a kama 'Ishara’ za mpango wa namna hii na hizo zilizodaiwa na Ukristo wa sasa. Lakini maana nzima ya karama za Roho zilizomilikiwa katika karne ya kwanza ilikuwa kuonyesha bayana ukuu wa Ukristo wa kweli juu ya dini nyingine zote. Uhakika ni kwamba 'Miujiza’ ya Ukristo wa siku hizi upo kwa mpangilio wa namna moja na dini nyingine, yaonyesha kwamba karama za Roho Mtakatifu zilizokuwa katika karne ya kwanza kwa sasa hazishikwi na watu.

Taarifa nyingine zenye maana katika eneo hili zimetolewa katika Upentekosti wa Williamu Camp bell (Makanisa ya Kristo, mwaka 1967). Anaonyesha ya kwamba dini nyingi za kipagani zina jambo hili hili la kunena 'Lugha’. Hivyo katika sehemu ya Kawaii, makuhani wa Mungu Oro wamewaza kuwa anafunua nia yake kwa sauti isiyosikika ambayo inatafsiriwa na makuhani wengine. Jambo hilo hilo hutokea katika mikutano ya Pentekosti. Ushindi unaoendelezwa na Uislam juu ya Ukristo katika sehemu nyingi za Afrika kwa kweli usingeonekana kama 'Ukristo’ wa watu wengi ulikuwa unafanya miujiza ya kweli kwa utaratibu na kwa nguvu zenye kuthibitisha za wale waliokuwa karne ya kwanza. Kwa kweli wale wenye kuwa na'Msaidizi’ wa kipawa cha Roho Mtakatifu watafanya, naam, "Kazi kubwa" kuliko alizofanya Yesu (Yoh. 14: 12,16). Udhuru wa kwamba Wakristo wanaweza kufanya miujiza ya namna hii kama walikuwa na imani zaidi, hapa wanakumbana na shida kubwa. Aidha wakiwa na karama zenye miujiza ya msaidizi, au wakiwa hawana, na kama wanadai kwamba wanafanya - " Kazi kubwa kuliko hizi atafanya" (Yoh. 14:12) - si'Utaweza kufanya’ !


   Back
Home
Next