Misingi Ya BIBLIA
Somo La 2: Roho ya Mungu
Ufafanuzi | Maongozi ya Mungu | Vipawa Vya Roho Mtakatifu | Kurudishwa kwa vipawa | Biblia ni Mamlaka pekee | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Je! Roho Mtakatifu ni Mtu?, Kawaida ya kuita kitu kana kwamba ni Mtu, Mambo ya kelvini, "Nanyi mtapokea Roho mtakatifu", "Na ishara hizi zitafuata") | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 4: Je! Roho Mtakatifu ni Mtu?

Somo la 2.1 na 2.2 yametoa ushahidi mkubwa wa kwamba Roho ya Mungu unatajwa uweza wake, unaotoa "Nia" yake katika kila njia pana. Kwa sababu ya namna Roho ya Mungu itendavyo kazi vivi hivi ni kioo sahihi cha nafsi na utu wa Mungu, baadhi ya watu wameleta ubishi na kusema ya kwamba Roho ya Mungu ni mtu ambaye pia ni Mungu. Kusoma tena kwa makini sehemu zilizotangulia zitaonyesha ya kwamba Roho ya Mungu ni akili na uweza wake; kama hivyo ndivyo, basi hakuna mfano wa kwamba nia - akili au nguvu yaweza kuwa mtu. Umeme ni nishati - nguvu isiyoonekana ambayo inatoa matokeo kwa mtu anayeutumia, lakini umeme hauwezi kuitwa ni mtu, Roho ya Mungu ina upendo wake, kama sehemu ya tabia yake, na tena unatajwa uweza wake, lakini hautajwi kuwa ni mtu aliyejitenga toka kwake.

Ni makosa ya kuonekana wazi kama shauri hili lilivyokosewa (la Roho Kuwa ni mtu) na kuonekana, ni dhana iliyoaminiwa na 'Wakristo’ walio wengi, kwa kuwa wanasadiki mafundisho ya 'Utatu’. Kwa maana hii imesemwa kuwa wapo Miungu watatu ambao kwa njia isiyoeleweka vile vile kuwa ni yule yule Mungu Baba, Roho Mtakatifu na Yesu. Watu hao hao wametoa kadhia kuwa Mungu si mtu, lakini wanasema ya kwamba Roho Mtakatifu ni mtu; hapa maneno yanaachana kabisa. Tena, Roho Mtakatifu atafanywa kuwa ni Baba ya Yesu.

Kuna sababu nzuri ya kuamini ya kwamba'Utatu’ kimsingi lilikuwa ni wazo la kipagani lililoingizwa katika Ukristo - basi hili neno halitoki katika Biblia. Wakiisha kubali dhana hii ya kuwa Mungu ana nafsi tatu, ndipo Wakristo wamelazimika kufikia wazo lisilo kweli na gumu kueleweka la kwamba uweza / Roho ya Mungu ni mtu, aliye Mungu tena, ingawa si Mungu. Wanapokabiliwa na maneno yaliyo mbali na akili kwa maono yao, njia ya kukwepa watu wengi zaidi ni kwa watu hawa kudai kwamba Mungu ni siri, nasi tukubali mambo haya kwa imani pasipo kutaka maelezo yenye maana ya akili.

Kwa maana hii ni kushindwa kutazama ushahidi ulio katika Agano Jipya katika Siri ya Mungu kuwa imefunuliwa ndani ya neno na kazi ya Kristo:-

"Kwa maana ndugu zangu sipendi msiijue siri hii" (Rum. 11:25).

"Kwa kuhubiri kwake Yesu ……. Na ufunuo wa ile siri" (Rum. 16:25)

"Akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake" (Efe. 1: 9; 3:3).

"Angalia, nawaambia ninyi siri ….." (1 Kor. 15:51).

Mahubiri ya Paulo yalikuwa "Katika kujulisha ile siri ya Injili" (Efe. 6:19; Kol. 4:3).

"Siri ile ……. Sasa imefunuliwa kwa watakatifu" (Kol. 1: 26, 27).

Kwa mkazo huu wote - ni kwamba - ni kule si sasa kuna siri yoyote iliyofungamana na mafundisho makubwa, atakuwepo tu mtu mwingine aliye gizani ambaye atadai kwamba kuna siri. Na mtu huyu hana wasi wasi wa kwamba Biblia inaita jina badala ya "Babeli" utaratibu wa dini ya upotovu ulioelezewa katika ufunuo, ni 'Siri’ (Uf. 17:5) ? kidokezo dhahiri ni kwamba utaratibu huu unatangaza ya kuwa imani zake ni siri; lakini waumini wa kweli wanafahamu siri ya mwanamke huyo (Uf. 17:7).

Fikira hizi zisizo dhahiri, kwa kweli zimetarajiwa toka kwao wawekao fahamu zao kwa Mungu juu ya mawazo ya vitu kama akutanavyo mwanadamu, au shughuli zisizo wazi, zisizoeleweka za nguvu nyingine kiroho juu ya fikira zao. kama kweli tunatarajiwa kweli kuwa wanyenyekevu katika fundisho la Neno la Mungu , kinachofuata tena tunatakiwa kutumia nguvu za kufikiri na akili ya kupata elimu ili kwamba tuvumbue ujumbe wake.

Mhubiri awaye yote wa Injili ambaye taarifa zake zimo katika Biblia, hakukimbilia kamwe kusema,'Hii ni siri sana, hamwezi kuanza kuielewa’ badala yake, tunawasoma wakiwasihi watu kutumia akili nao wavutwe na wazo litokalo katika Maandiko.

Katika kuhubiri kwake aina ya Injili kubwa ambayo tunaiona katika masomo haya, Paulo " alihojiana nao kwa njia ya Maandiko, akayafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu" (Mdo. 17:2,3). Huu ulikuwa ni utaratibu wenye muundo wa kufikiri maneno ya Biblia wastani wake ulio bora; fungu hili la maneno linatangulia taarifa "Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake …… alihojiana nao ……. " Basi, huu ulikuwa ni mtindo wa kawaida yake (tazama tena Mdo. 18:19). Kwa kupatana na huu, kipindi cha kampeni kubwa pale Korintho, Paulo "alitoa hoja zake katika Sinagogi kila sabato, akijaribu kuwavuta Wayahudi ……. (Lakini) walipopingana ….." (Mdo. 18:4-6). Wale walioongoka walienda njia ya ushawishi wa maneno ya Paulo ambayo msingi wake umo ndani ya Biblia; hapa hayakuwa 'Maono ya Yesu ndani ya chumba changu’; 'hisia zilinijia zisizoelezeka’, 'Nilikutana na Bwana jioni moja’.

Elewa vile vile, ya kwamba habari iliyovuviwa inatoa ombi la maneno yenye akili na busara, kwa kuonyesha kwamba "Walipingana wenyewe" vivyo hivyo kule Antiokia, Paulo na Barnaba "walisema nao (neno), wakawatia moyo ….." (Mdo. 13:43). Eneo lao lililofuata la kusita lilikuwa ni Ikonio, mahali ambapo "Walinena kundi kubwa …. Waliamini " (Mdo. 14:1).

Baadaye kidogo aliposimama kutetea maisha yake, maneno yale yale yenye utukufu na busarra yaliendelea katika kuvuviwa tumaini imara la Paulo kwa sababu ya kipindi kijacho: "Alitoa hoja zake katika habari ya haki, na kuwa na kiasi, na hukumu itakayokuja" na udhahiri huu unaopenya hata mwenye kubeza, hakimu wake "alihofu" (Matendo ya mitume 24:25).

Kwa kuwa kuongoka kwetu kunakuwa juu ya msingi huu wa njia ya kutumia akili, tunaweza kutoa maelezo yenye busara ya Biblia na tumaini letu na mafundisho:-

" kuwa tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizae habari za tumaini lililo ndani yenu"(1Petro. 3:15).

Kusema katika sauti yenye busara juu ya matukio ya mtu mwenyewe si kutoa hoja ya tumaini la Injili. Utegemezi unaoendelea juu ya ushuhuda wenyewe kama njia ya kuhubiri Wakaristo wengi wa Kiinjili, ukosefu wa 'hoja ya jibu la kutumia’ unajitokeza kwa 'tumaini’ lao. Maelezo yote yamezuka miongoni mwa Wakristo hawa kwa'kuwawezesha katika kushiriki yale Bwana aliyofanya katika maisha yangu’ n.k. Hizi hadithi fupi za maisha ya mtu zatofautiana vikali na maneno ya Paulo, "Hatujihubiri wenyewe, bali Kristo (2Kor. 4:5) - na kama toka mtu aliyekuwa na uhusiano binafsi na Yesu" zaidi kuliko wengi.

Maneno ya kutumia akili, maana ya jinsi ya kuongoka kwetu kibiblia yaweke mfano mzuri wa uhusiano wetu mpana na Mungu katika siku zetu zilizobaki. Mifano yetu, kama siku zote, ni ya Wakristo wa kwanza waliyotumia kwa "Kutoa Hoja" katika kutatua matatizo yao ya mambo ya kutoa mashauri (Mdo. 6:2).Nyaraka za Agano Jipya tena zinawasadikisha wasomaji wao wafahamu kutumia akili ya maneno ya Biblia. Basi, "Kwa akili ya kufahamu" jinsi makuhani wakuu walivyokuwa chini ya torati ya Musa, tunaweza kuelewa habari moja moja kuhusu kazi ya Kristo (Ebra. 5:3) akiisha unena upendo wa Mungu unaozidi katika Kristo, Paulo anatoa sababu ya kwamba ndiyo "Ibada yenu yenye maana (Kutuumia akili) sisi wenyewe kujitoa kabisa kwake katika kuitikia (Rum.12:1). Basi kuitikia kwetu katika maneno ya Biblia ni kumoja na kutumia 'akili’ yetu kunakopatikana toka katika neno la Mungu.

Katika mwangaza wa yote haya, yatakuwa dhahiri kwamba si busara kudai ya kuwa roho ya Mungu ni nafsi peke yake ambayo si Mungu lakini wakati huo huo ni Mungu - na kwa kukabili wazo hili kwa kusema kwamba jambo hili lote ni lenye siri na kwamba kutumia akili si muhimu, kwa maneno ya Biblia halikubaliki. kama hatuwezi kuchukua maneno toka Maandiko, basi kujifundisha kote Biblia ni bure, hakuna haja ya kuwa na Biblia, ambayo inaweza kupimwa kama maneno yanayofikiriwa kuwa kweli matamu tu au neno la kitabu kinachovutia. hiki kitabu pia kinaonekana kuwa juu ya makabati ya Wakristo wengi.

Ingawa hivyo, katika tumaini lao, baadhi ya wanaosadiki kuwa Roho ya Mungu ni mtu wanajaribu kutoa sababu za Biblia. Mafungu ya maneno yaliyonukuliwa ni yale ambayo yanataja roho wa Mungu kwa msemo wa peke yake, kama "Mfariji -Msaidizi" katika Yoh. 14:16, au ushahidi wa kuwa roho "alihuzunishwa".

Tumeonyesha kwa kuandika bayana katika somo la 4.3 kuwa "Roho ya Mwanadamu yaweza kuchukizwa (Mdo. 17:16), kufadhaika (Mwa.41:8) au kushangilia (Luka. 10:21). "Roho" yake, yaani, nafsi yake hasa, akili na kusudi lake, vinavyozusha matendo yake, kwa hiyo husemwa kuwa ni mtu tofauti, lakini bila shaka, si hivyo hasa, Vile vile, Roho ya/wa Mungu, yaweza kusemwa kwa jinsi hiyo hiyo.

Tena inabidi ieleweke ya kwamba mara nyingi Biblia imetumia msemo kutaja kitu au jambo kama ni mtu inaposema mambo ya kuwazika, kama. Hekima imetajwa kana kwamba ni mtu katika kitabu cha Mithali 9:1. Hivi ni kwa kutuonyesha mtu gani aliye na hekima anavyofanana katika kutenda matendo;'Hekima’ haiwezi kuwepo isipokuwa ndani ya akili ya mtu, ndivyo shauri hili la kuita kitu kana kwamba ni mtu limetumika. Maelezo zaidi juu ya hili, tazama tumeacha kitambo …… sehemu ya 5,

"Jambo la kuita kitu kama mtu".


   Back
Home
Next