Misingi Ya BIBLIA
Somo La 8: Asili ya Yesu
Dibaji | Tofauti zilizopo kati ya Mungu na Yesu | Asili Ya Yesu | Ubinadamu Wa Yesu | Uhusiano Wa Mungu Na Yesu | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Akiwa Yuna na namna ya Mungu") | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 27: "Akiwa Yuna na namna ya Mungu"

"……Yesu alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa"(Flp 2:5-11). Aya hizi zimechukuliwa kuwa na maana ya kwambaYesu alikuwa ni Mungu, lakini alipozaliwa akawa binadamu. Ikiwa jambo hili ni kweli, basi kila kipengele kilicho katika masomo ya 7na 8 inabidi yaelezewe mbali vile vile. Imekubalika kwamba aya moja hairuhusiwi kuachana na maana yeyote ya mafundisho ya Biblia. Ni jambo la maana kwamba hili ndilo fungu pekee la maneno ambalo laweza kuwekwa mbele ili kueleza mtengano wa ‘kukosekana kiungo’ katika wazo la wanaoamini katika utatu pamoja - ni jinsi gani Yesu alihama toka kuwa ni Mungu katika Mbingu na kuwa kitoto kichanga ndani ya tumbo la Mariamu. Uchambuzi ufuatao unataka kuonyesha kwa maneno maana ya fungu hili hasa lilivyo.

  1. Kuna idadi ya maneno ambayo karibu yanatoka ndani ya fungu hili ambayo yanaachana kabisa na wazo la wanaoamini katika utatu:

    1. "Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno", Yesu,"akamkirimia yaani alimpa jina"(mst 9) yaonyesha kwamba Yesu hakujiadhimisha mwenyewe- ni Mungu aliyefanya hivyo. Imetokea kuwa hakuwa kwenye hali ya kuadhimishwa kabla Mungu hajamfanyia hivi, kwenye ufufuo wake.

    2. Muunganiko mzima wa mfululizo wa matendo ya kujinyenyekeza Kristo mwenyewe na baadaye kuadhimishwa na Mungu yote yalikuwa kwa ajili ya utukufu wa"Mungu Baba"(Mst 11). Mungu Baba kwa sababu hii hana uwiano ulio sawa na Mwanae.

  2. Maneno yenyewe ya fungu hili inabidi yapimwe kwa uangalifu. Paulo haanzi tu kusema kuhusu Yesu ‘nje ya utaratibu’. Anataja moyo wa Yesu katika Wafilipi1:8. Tukirudi katika Wafilipi 1:27 Paulo anaanza kusema umuhimu wa hali yetu ya moyo. Hii imekuzwa katika aya za awali za sura ya 2;"Mwe na nia moja….. roho- moyo mmoja…… mkinia mamoja….. kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia moyo uo huo ndani yenu, ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu…"(Wafilipi 2:2-5).Basi Paulo anazungumzia umuhimu wa kuwa na moyo, nia kama wa Yesu, alijitoa kuwatumikia wengine kwa upole. Aya zinazofuata kwa sababu hii zinaainisha juu ya ubinadamu wa moyo ambao Yesu alionyesha, si kuzungumzia badiliko lolote la mwili.

  3. Yesu alikuwa,"Yuna namna ya Mungu"Tumeonyesha katika somo la 8:3 ya kuwa Yesu alikuwa wa asili ya mwanadamu na kwa hiyo huu hauwezi kumtaja Kristo akiwa na mwili wa Uungu. Biblia habari njema B.H.N fungu hili la maneno lina upotoshaji mkubwa hapa. Kwa kupita, ijulikane ya kuwa matoleo mengine ya siku hizi yamepanga ‘usomaji rahisi’, yameelekea kurahisisha juu ya maana halisi ya maneno ya Kiyunani, nayo yamelekea kutoa ufafanuzi kuliko kutafsiri kwa maneno ya hakika. Wafilipi 2:5-8 huu ni mfano uliojulikana tangu zamani. Walakini, huu sio kuvunja sifa yao katika kutumia kwa namna nyingine.

"Namna"(Kiyunani ‘morphe’) haiwezi kutajwa asili ya mwili imethibitishwa na Flp 2:7 akinenwa Kristo akitwaa ‘namna ya mtumwa’. Alikuwa yuna namna ya Mungu, lakini akatwaa namna ya mtumwa. Mwili wa asili wa mtumwa hauna tofauti na ule wa binadamu yeyote mwingine. Kwa mapatano na maneno yenyewe, tunaweza kwa usalama kufasiri huu kuwa na maana ya kuwa ingawa Yesu alikuwa mkamilifu alikuwa na nia kama ya Mungu kabisa, lakini akapenda kutwaa mwenendo wa mtumwa. Aya zingine zilizofuata Paulo anatutia moyo"tufanane na kufa kwake (Kristo)"(Wafilipi 3:10). Tushiriki ‘morphe’, namna ya Kristo aliyotuonyesha kwa kifo chake. Hii haina maana hatuwezi kushiriki mwili wake aliokuwa nao wakati ule, kwa kuwa tayari tuna mwili wa kibinadamu. Tusijibadilishe wenyewe mwili huu, bali tunahitaji kubadili mwendo wa kuwaza, ili kwamba tuweze kuwa na morphe au mfano wa akili aliyokuwa nayo Kristo kwa kufa kwake.

Neno la Kiyunani ‘morphe’ maana yake ni mfano chapa au kufanana. Wanadamu wamesemwa wana"mfano(morphe) wa utauwa"(2Tim 3:5). Gal 4:19 yamsema"Kristo aumbike-awe Morphe ndani yenu"waaminio. Kwa kuwa alikuwa na tabia timilifu, mwendo wa ukamilifu kama Mungu kwa kuwaza, Yesu alikuwa"yuna namna ya Mungu".Kwa sababu hii hakuona kule kuwaza au kujua ya kwamba kwa maana hii alikuwa mmoja pamoja na Mungu. B.H.N. inatoa tafsiri tofauti kwa fungu hili la maneno ikisema lakini hakufikiri kwa kule kuwa sawa na Mungu ni"kitu cha kung’ang’ania kwa nguvu". Ikiwa tafsiri hii ni sahihi (ambayo vile vile inasaidiwa na U.V kwa sehemu)basi hii inatia kosa, kabisa wazo la kwamba Yesu alikuwa ni Mungu. Kulingana na B.H.N tafsiri yake, Yesu kwa muda hakushiriki wazo la kuwa sawa na Mungu alijua kwamba alikuwa chini ya Mungu, na sio uwiano sawa Naye.

  1. Kristo"akajifanya kuwa hana utukufu", Ukitamka unabii wa kusulubiwa kwake katika Isaya 53:12:"Alimwaga nafsi yake hata kufa", Yeye mwenyewe akatwaa namna (mwenendo) ya- wa mtumwa". Kwa msimamo wake wa kuwa kama mtumwa kwa wafuasi wake (Yn. 13:14), ulijionyesha kwa ukuu na kufa kwake msalabani (Math.20:28). Isaya 52:14 ulitabiri kuhusu mateso ya Kristo ya kwamba juu ya msalaba"uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya mwanadamu". Uendelevu huu wa kujinyenyekeza mwenyewe"hata mauti, naam mauti ya msalaba"ulikuwa ni jambo lingine lililotokea wakati wa maisha yake na kufa, sio wakati wa kuzaliwa kwake. Tumeonyesha maneno ya fungu hili yakitaja nia ya Yesu, unyenyekevu ulioshikwa kwa ajili yetu ukiwa ni mfano wa kuiga. Aya hizi yapasa basi kusema maisha ya Yesu alipokuwa hapa duniani, katika mwili wetu wanadamu, na jinsi gani alijinyenyekeza mwenyewe, mbali ya kuwa na moyo unaolingana na Mungu, kupima haja zetu.

  2. Ikiwa Kristo alikuwa Mungu kwa asili na kisha aliacha nyuma akatwaa asili ya mwananadamu, kama wanaoamini katika utatu pamoja na wanavyo jaribu kutafsiri fungu hili la maneno, basi Yesu hakuwa ‘Mungu kabisa’ wakati akiwa duniani: lakini waaminio katika utatu husema hivyo. Yote haya yanaonyesha kuachana kunako fanywa na wanao kubali kutoa pamoja ufafanuzi uliofanywa kama huu wa utatu.

  3. Hatimaye, maana inayohusu maneno"ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu". Hapa yeye mwazo haina maana ya kwamba asili alikuwa ni wa milele. Kristo kuwa"yuna namna ya Mungu" basi ina maana ya kwamba alikuwa na mfano na Mungu (kiakili) mstari huu haudokezi kuwa tangu mwanzo wa wakati alikuwa namna hiyo.


  Back
Home
Next