Misingi Ya BIBLIA
Somo La 8: Asili ya Yesu
Dibaji | Tofauti zilizopo kati ya Mungu na Yesu | Asili Ya Yesu | Ubinadamu Wa Yesu | Uhusiano Wa Mungu Na Yesu | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Akiwa Yuna na namna ya Mungu") | Maswali

8.5 Uhusiano Wa Mungu Na Yesu

Kupima ni jinsi gani Mungu alimfufua Yesu kunatuongoza tufikirie uhusiano kati ya Mungu na Yesu. Ikiwa wote wawili ni wa"usawa pamoja"…… milele pamoja; kama fundisho la utatu pamoja linavyosema, basi tungetegemea uhusiano wao kuwa huo wa uwiano ulio sawa. Tayari tumeona ushahidi mkubwa wa kuwa hili haliko hivyo. Uhusiano kati ya Mungu na Kristo ni hali moja kati ya mume na mke;"kichwa cha kila mwanaume ni Kristo;na kichwa cha mwanamke ni mwanamume; na kichwa cha Kristo ni Mungu"(1Kor 11:3). Mwanamume akiwa ni kichwa cha mke, basi Mungu ni kichwa cha Kristo, ingawa wana kusudi lile la umoja kama linavyokuwepo kati ya mke na mme. Hivyo"Kristo ni wa Mungu"(1Kor 3:23), kama mke anavyomhusu mwanamume

Mungu Baba mara nyingi ameelezewa kwa maneno kuwa Kristo ni wa Mungu. Uhakika wa kwamba Mungu amesemwa kuwa ni"Mungu ni Baba wa bwana wetu Yesu Kristo"(1Petro 1:3; Efe 1:17) hata baada ya Kristo kupaa kwenda mbinguni, kunaonyesha ya kuwa huu sasa ni uhusiano wao, kama ulivyokuwapo wakati wa maisha ya mwili hapa duniani. Mara nyingi mkazo umetiwa na hao waminio katika utatu pamoja ya kwamba Kristo amesemwa tu kuwa chini- mdogo kuliko Mungu ni wakati wa maisha yake duniani. Nyaraka katika Agano jipya ziliandikwa miaka mingine baadaye Kristo alipopaa kueleke mbinguni, lakini bado Mungu amesemwa kuwa Kristo ni wa Mungu na Baba. Bado Yesu anasema Baba ni Mungu wake

Ufunuo, kitabu cha mwisho cha Agano Jipya, kiliandikwa karibu miaka 30 baada ya Kristo kutukuzwa na kupaa, lakini kinasema Mungu ni"Mungu na baba yake (Kristo)" (Uf 1:6 U.V) katika kitabu hiki Kristo aliyefufuliwa na kutukuzwa alitoa ujumbe kwa waminio. Analitaja"hekalu la Mungu wangu…. Jina la Mungu wangu…… mji wa Mungu wangu"(Uf 3:12). Hivi inathibitisha ya kwamba hata sasa anadhani Baba kuwa ni Mungu wake na kwa sababu hii yeye (Yesu) sio Mungu.

Wakati wa maisha yake ya mwili wa kufa,Yesu alimtaja Baba yake kwa njia hii. Alisema napaa kwenda kwa "Baba yangu na Baba yenu; na kwa Mungu wangu na Mungu wenu"(Yohana 20:17). Msalabani Yesu alionyesha ubinadamu kabisa : Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha? (Math 27:46). Maneno haya hayawezi kueleweka ikiwa yanasemwa na Mungu mwenyewe. Uhakika wa kwamba Yesu alimtolea dua Mungu"na kulia sana na machozi"ndani yake wenyewe inaonyesha hali ya kweli ya uhusiano wao (Ebra 5:7; Luka 6:12).ni bayana Mungu hawezi kujiombea mwenyewe. Hata sasa, Kristo anamuomba Mungu kwa ajili yetu (Rum 8:26,27; 2Kor 3:18 U.V).

Sasa tumeonyesha kwa maelezo ya kwamba uhusiano wa Mungu na Kristo wakati wa maisha yake duniani haukuwekwa kimsingi tofauti na sasa ulivyo. Kristo amesimulia kuwa Mungu ni Baba yake na Mungu wake, naye alimwomba Yeye; nafasi iyo hiyo inapatikana sasa, baada ya ufufuo na kupaa kwa Kristo. Wakati wa maisha yake duniani, Kristo alikuwa mtumishi wa Mungu (Mdo 3:13,26; Isaya 42:1; 53:11). Mtumishi hufanya mapenzi ya Bwana wake, na kwa njia yeyote hawi sawa na bwana wake (Yohana 31:16). Kristo alitia mkazo wa kwamba uwezo na mamlaka aliyokuwa nayo vilitoka kwa Mungu, sio kutoka kwake mwenyewe;"Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe…. Sitafuti…… bali mapenzi yake aliyenituma … Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe….."(Yn.5:30,19).


  Back
Home
Next