Misingi Ya BIBLIA
Somo La 8: Asili ya Yesu
Dibaji | Tofauti zilizopo kati ya Mungu na Yesu | Asili Ya Yesu | Ubinadamu Wa Yesu | Uhusiano Wa Mungu Na Yesu | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Akiwa Yuna na namna ya Mungu") | Maswali

8.3 Asili Ya Yesu

Neno ‘hali ya tabia’ inatajwa kwa tabia ya kawaida sehemu muhimu ilivyo. Tumeonyesha katika somo la 1 ya kwamba Biblia inazungumzia hali ya tabia mbili - hiyo ya Mungu na hiyo ya binadamu. Kwa hali ya Mungu hawezi kufa, kujaribiwa n.k. Ni dhahiri kwamba Kristo hakuwa na mwili wa Mungu wakati wa maisha yake.Kwa hiyo Yesu alikuwa mwenye mwili wa mwanadamu kabisa. Kutokana na maelezo yetu ya neno ‘hali ya tabia’ itakuwa dhahiri kwamba Yesu hakuweza kuwa na miili miwili wakati ule ule. Ni muhimu kuelewa kuwa Kristo alijaribiwa kama sisi (Ebr 4;16) ili kwamba kwa kushinda kikamilifu majaribu aweze kuupata msamaha kwa ajili yetu. Mawazo mabaya ambayo ni msingi wa majaribio yetu yanakuja toka ndani ya mioyo yetu (Marko 7:15-23) toka ndani ya miili yetu wanadamu (Yakobo 1:13-15). Basi,ilikuwa ni lazima, kwamba Kristo awe na mwili wa binadanu ili kwamba aweze kuonja na kuyashinda haya majaribu.

Waebrania 2:14-18 yamewekwa yote haya kwa maneno mengi:-

"Basi, kwa kuwa watoto (sisi) wameshiriki damu na mwili (mwili wa kibinadamu) naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo (yaani hali ya tabia ile ile) ili kwa njia ya mauti amharibu….. ibilisi……. Maana ni hakika, hatwai asili ya Malaika bali anatwaa asili (hali ya tabia) ya mzao wa Ibrahimu. Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema,….ili afanye suluhu(upatanisho) kwa dhambi za watu wake. Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa".

Maneno haya yanaweka mkazo wa ajabu juu ya ukweli wa kwamba Yesu alikuwa wa asili ya mwanadamu:"Yeye naye vivyo hivyo"alishiriki yayo hayo (Ebra 2:14). Fungu hili linatumia maneno matatu yote yenye maana moja, kuleta maana alihsiriki asili"ile ile"; taarifa ingesema ‘alishiriki tu’, bali inasisitiza"alishiriki yayo hayo"Mstari wa 16 Waebrania mlango wa 2 kwa mfano mmoja unatoa maana ya kuwa Kristo hakuwa na asili ya malaika, kwa kuwa alikuwa mzao wa Ibrahimu, aliyekuja kuleta wokovu wa mkutano wa waaminio ambao wamekua wazao wa Ibrahimu. Kwa sababu hii, ilikuwa ni muhimu kwa Kristo awe na asili ya binadamu. Kwa namna yoyote ilimpasa kufananishwa na ndugu zake (Ebra 2:17) ili kwamba Mungu aweze kutupatia msamaha kwa njia ya dhabihu ya Kristo. Kusema kwamba Yesu hakuwa na mwili wa kibinadamu kabisa basi ni kutojua misingi kabisa ya habari njema za Kristo.

Popote waamini waliobatizwa wakitenda dhambi, wanaweza kumjia Mungu kwa kuungama dhambi zao kwa sala kupitia Kristo (1Yoh 1:9); Mungu anajua kwamba Kristo alijaribiwa kutenda dhambi hasa kama wao, bali alibaki kuwa mkamilifu, akashinda kabisa lile jaribu linalowashinda. Kwa sababu hii Mungu kwa ajili ya Kristo anaweza kutusamehe (Efeso 4:32). Basi, ni lazima tufahamu ni jinsi gani Kristo alijaribiwa kama sisi, na ilihitajika awe na mwili kama wetu kuwezesha hili. Waebrania 2:14 ni dhahiri inasema kwamba Kristo alikuwa na mwili na damu kuwezesha hili."Mungu ni Roho"(Yn. 4:24) kwa asili, na ingawa ana mwili wenye kuonekana, ukiwa ni ‘Roho’ hana mwili wa nyama na damu. Kristo akiwa na mwili wa"nyama"maana yake ni kwamba kwa vyovyote hakuwa na asili ya Mungu wakati wa maisha yake.

Majaribio yaliyotangulia ya watu kushika neno la Mungu, yaani kushinda jaribu kabisa yote yalishindikana. Kwa sababu hiyo"Mungu kwa kumtuma mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio na dhambi na kuwa dhabihu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili (Rum 8:3).

"Dhambi"ni kutaja uelekeo wa kuvunja sheria ambapo ni tabia yetu ya asili. Hii tayari tumeipa kipaumbele na tutaendelea kufanya hivo"kisha mshahara wa dhambi ni mauti". Ili kujiondoa kwenye hatari hii, binadamu anahitaji msaada toka nje. Yeye mwenyewe aonekana kutoweza kukamilika; kujikomboa hakukumo na hukumu ndani ya nyama za mwili. Basi, Mungu ameingila kati na kutupa mwanawe mwenyewe ambaye alikuwa na ‘mwili wa nyama ulio na dhambi ambao sisi tunao’pamoja na mvuto wa kuelekea kutenda dhambi kama sisi tulivyo wepesi kufanya dhambi. Tofauti na binadamu yoyote Kristo alishinda kila jaribu, ingawa alikuwa na uwezekano wa kuvunja sheria kama tulivyo. Rum 8:3 hueleza jinsi Kristo alivyo na mwili wa kibinadamu ni"mwili ulio na dhambi". Mistari michache iliyotangulia Paulo alisema jinsi gani ndani ya mwili"halikai neno jema", na namna kwa asili mwili unavyopinga kumtii Mungu (Rum 7:18-23). Katika maneno haya yote yanastahajabisha zaidi kusoma ya kuwa Kristo alikuwa na"mwili ulio wa dhambi"katika Rum 8:3.Ilikuwa sababu hii na huko kushinda mwili wake, hata tunayo njia ya kuuepuka mwili wetu; kwa nguvu Yesu alijua hali ya dhambi ya asili ndani ya mwili wake kidokezao cha kwamba alikuwa"mwema"na mkamilifu wa tabia ya asili alijibu:"Kwanini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu"(Marko 10:17,18)

Wakati mwingine watu walianza kushuhudia ukuu wa Kristo kwa sababu ya mfululizo wa miujiza ya kuonekana dhahiri aliyoifanya. Haya hayakumpatia faida"kwa kuwa yeye aliwajua wote, na kwa sababu hakuwa na haja na mtu kumshuhudia habari za wanadamu"(Yn. 2:23-25). Kwa sababu ya elimu yake ya kujua mwili wa mwanadamu (alijua yote kuhusu huu), Kristo hakutaka watu wamsifu yeye mwenyewe kwa haki yake mwenyewe, kwa kuwa alijua ni kiasi gani uovu ulivyokuwamo ndani ya mwili wake mwenyewe wa kibinadamu.


  Back
Home
Next