Misingi Ya BIBLIA
Somo La 1: Mungu
Uwepo wa Mungu | Nafsi yake Mungu | Jina La Mungu Na Tabia Ya Sifa Yake | Malaika | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Mungu ni roho" (Yohana 4:24), "Matumizi ya jina la Mungu", "Ufunuo wa Mungu") | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 1: "Mungu ni roho" (Yohana 4:24)

Katika somo la pili tunafafanua kwa utaratibu zaidi jinsi Roho wa Mungu alivyo. Tunaweza kutoa maelezo kwa ufupi sababu zilizoonyeshwa hapo kwa kusema kwamba roho wa /ya Mungu ni nguvu au pumzi yake ambayo kwa hiyo nafsi yake mwenyewe, Utu wake na tabia, vimedhihirika kwa mwanadamu kwa njia ya matendo yake ambavyo Roho huyo anatimiza.Hivyo'Mungu ni Roho’ kama katika Yohana 4:24 atafsiriwe vema kwa kuwa Roho yake ndiyo inafanya utu wake.

Mungu amesemwa kuwa yumo katika vitu vingi, kwa mfano:-

‘Mungu wetu ni moto ulao’ (Ebr. 12:29)

‘Mungu ni Nuru’ (1 Yoh. 1:5)

‘Mungu ni Pendo (1 Yoh.4:8)

‘Neno (Kiyunani'Lagos’ - Mpango, Lengo,Kusudi, wazo) alikuwa Mungu’ (Yoh 1:1)

Hivyo,'Mungu’ ni sifa yake. Ni kosa lililo wazi kuleta sababu za kupinga kwamba sifa za upendo wa Mungu ni za kuwazika, kwa kuwa tunasoma kwamba 'Mungu ni pendo’ tunaweza kumwita mtu mwingine Mwema wenyewe; lakini hii haina maana kwamba haupo bila mwili ni namna ya kuwepo yeye ndiko kunatudhihirishia wema kwetu.

Roho ikiwa ni nguvu ya Mungu, mara nyingi tunasoma Mungu akiituma au akiiongoza roho yake kutimiliza mabo yake kwa kupatana na mapenzi yake na tabia ya sifa yake. Hata ameelezewa kuwa anaumba roho (Yaani Upepo UV). Kusema kwamba Mungu na roho yake katika maana safi iliyo halisi ni msemo ule ule kwa namna nyingine - katika maana inakuwa Uwepo wa Mungu.

Mifano ya Mungu akiiongoza Roho yake ni mingi, inaonyesha mtengano wa Mungu na Roho yake:-

‘Yeye (Mungu) aliyetia kati yao Roho yake mtakatifu’ (Isa. 63:11)

‘Nitatia Roho yangu (Mungu) juu yake (Yesu)’ (Math.12:18)

‘Baba huwapa Roho mtakatifu’ (Luk. 11:13)

‘Roho akishuka kama hua toka Mbinguni’ (Yoh. 1:32)

‘Nitawamwagia watu wote Roho yangu’ (Matendo. 2:17).

Kwa kweli ushahidi juu ya 'Roho wa Mungu’ ni uhakika wa kutosha kuwa Roho sio Mungu mwenyewe. Tofauti hizi kati ya Mungu na Roho ni shida nyingine ilio kwa wale wanao amini kuwa Mungu ana Nafsi'Tatu’ ambazo Mungu amelingana na Yesu na Roho Mtakatifu. Jambo hili kama lingekuwa la kweli, na kama Mungu amedhaniwa kuwa sio mtu, basi halikadharika hata Yesu naye sio mtu halisi.

Kwa umuhimu sana, Mungu asiye mtu hata sala kuelekea kwake inakuwa haina maana, kwenye alama ambayo sala ni mazungumuzo kati ya fahamu zetu na wazo la Mungu ambalo lipo katika akili zetu. Daima tunakumbushwa kwamba tunamwomba Mungu ambaye ana Umbo makao yake yapo Mbinguni (Mhu. 5:2; Math. 6:9,5:16, 1Fal. 8:30) na kwamba Yesu sasa yuko mkono wa kuume huko ili kutoa maombi yetu mbele zake (1Pet. 3:21, Ebr. 9:24).

Ikiwa Mungu si mtu binafsi, maneno haya yametolewa bila kuwa na maana. Bali, Mungu akieleweka kuwa ni wa kweli, Baba mwenye upendo, Sala ya kumwomba inakuwa ya kweli, Jambo lililowazi na dhahiri - hasa tukizungumza na mtu mwingine ambaye tunamwamini ana mapenzi sana na anaweza kujibu.


  Back
Home
Next