Misingi Ya BIBLIA
Somo La 1: Mungu
Uwepo wa Mungu | Nafsi yake Mungu | Jina La Mungu Na Tabia Ya Sifa Yake | Malaika | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Mungu ni roho" (Yohana 4:24), "Matumizi ya jina la Mungu", "Ufunuo wa Mungu") | Maswali

1.4 Malaika

Yote ambayo tumeyapima sana katika somo hili yanaletwa pamoja kwenye tafakari ya Malaika:

 • Viumbe walio na mwili

 • Huchukua jina la Mungu

 • Wao ni njia ambayo roho wa Mungu anatenda kazi ya kutimiza mapenzi yake

 • Wanapatana tabia na kusudi lake

 • Na kwa hiyo wanamdhihirisha yeye.

Tumetaja kwenye somo la 1.3 ya kwamba moja kati ya maneno yanayotumika zaidi katika Kiebrania lililotafsiriwa "Mungu" ni' Eloi’ ambalo hasa maana yake ' Wenye nguvu’ hawa,'Wenye nguvu’ ambao huchukua jina la Mungu wanapotokea wana weza kuitwa 'Mungu’ kwakushirikiana kwao pamoja na naye karibu. Hawa viumbe wanaitwa Malaika.

Taarifa ya uumbaji wa ulimwengu katika mwanzo 1 inatuambia ya kwamba Mungu alitamka amri halisi kuhusu Uumbaji'Ikiwa hivyo’ walikuwa ni Malaika waliotimiza amri hizo:

"Enyi Malaika zake, mliohodari mtendao neno lake, mkiisikiliza sauti ya neno lake (Zab. 103:20).

Kwa sababu hii busara husadiki kuwa tunaposoma 'Mungu’ akiumba ulimwengu, kazi hii kweli ilifanywa na Malaika. (Ayubu 38:4-7) anadokeza vile vile namna hii. Sasa ni wakati mzuri kuelezea kwa kifupi matukio ya uumbaji kama yalivyoandikwa Mwanzo 1:

Siku ya Kwanza‘ Mungu akasema, Na iwe nuru, Ikawa’ (Mstari 3)

Siku ya Pili 'Mungu akasema, Na iwe anga katikati ya maji, likayatenga maji na maji.Mungu akalifanya anga ,akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga: Ikawa hivyo’ (Mstari 6,7)

Siku ya Tatu ‘Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, (akifanya Bahari na Bahari kuu) ili pakavu paonekane; Ikawa hivyo’ (Mstari wa 9)

Siku ya Nne ‘Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu… Ikawa hivyo’ (Mstari 14:15)

Siku ya Tano ‘Mungu akasema, Maji na yajae kwawingi na kitu kiendacho chenye uhai …. ndege waruke juu ya nchi ….. Mungu akaumba kila kiumbe chenye uhai (Mstari wa 20:21), Ikawa hivyo.

Siku ya Sita ‘Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe haikwa jinsi zake…. Mnyama wa kufugwa,nacho kitaambaacho …. Ikawa hivyo (Mstari 24)

Siku hiyo hiyo ya sita mtu aliumbwa. Mungu akasema, na tufanye mtu kwa mfano wetu, na kwa sura yetu (Mwa 1:26). Tuliwahi kutoa maelezo juu ya mstari huu katika somo la 1.2. Kwa muda uliopo, tunataka kujua hapa ya kwamba.'Mungu’ sio tu anatajwa Mungumwenyewe katika utu'Na tufanye mtu’ inaonyesha kuwa Mungu anatajwa mtu zaidi ya mmojaNeno la Kiebrania linalotafsiriwa hapa'Mungu’ ni Elohim (Eloi), Maana yake'Wenye nguvu’ Ukiwa ni ushahidi unaotaja Malaika. Ukweli ni kwamba Malaika walituumba sisi kwa mfano wao maana yake ni kuwa wana sura ya mwili ule ule kama tulio nao. Kwa sababu hiyo ni wa kweli, wa kugusika, viumbe wenye mwili, wakishiriki mwili ule ule kama wa Mungu.

‘Mwili’ Kwa maana hii unatajwa kwa msingi jinsi mtu mwingine alivyo kwa sababu ya muundo wa mwili wao. Katika Biblia ipo "Miili" ya aina mbili katika maana halisi ya neno haiwezekani kwa wakati huo huo kuwa miili hii ya aina mbili.

Mwili wa Mungu (‘Mwili wa Uungu’)
Hauwezi kutenda dhambi (Mkamilifu) Rum 9:14,6:23; Zab. 90:2, Math 5:48,Yak 1:13)
Haupatikani na Mauti (1Timotheo 6:16)
Una nguvu tele na uweza (Isaya 40:28)

Huu ndio mwili wa Mungu na Malaika na ambao alipewa Yesu baada ya kufufuliwa (Matendo 13:34; Ufunuo 1:18; Ebr. 1:3) Huu ndio mwili ambao tumeahaidiwa kupewa (Luka 20:35,36; Isa. 40:28,31)

Mwili wa mwanadamu
Hujaribiwa na kutenda dhambi (Yak 1:13-15) kwa nia mbaya ya asili (Yer 17:9; Marko 7:21-23)
Huangamia mautini, Yaani unapatwa na kifo (Rum. 5:12,17; 1Kor 15:22)
Una kikomo cha nguvu, sehemu mbili, kwa mwili (Isa. 40:30) na kwa akili (Yer 10:23)

Huu ni mwili ambao watu wote, wema na wabaya, kwa sasa wanao mwisho wa mwili huo ni kifo (Rum 6:23). Ulikuwa ni mwili ambao Yesu alikuwa nao wakati wa maisha yake ya mwili unaokufa hapa duniani (Ebr. 2:14-18,Rum. 8:3 Yoh 2:25, Marko 10:18)

MATENDO YA KUONEKANA NA MALAIKA

Malaika wakiwa na mwili wa Uungu, inabidi wawe hawana dhambi na kwa sababu hiyo hawawezi kufa kwa kuona kwamba dhambi huleta mauti (Rum. 6:23). Inapasa wawe na umbo halisi na mwili wa kuwepo mauti "Na yaletwe basi maji kidogo ukanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu"(Mwanzo 18:4)

Wawili kati ya hao Malaika wakati ule walikwenda kwa lutu katika mji wa Sodoma. Tena, walitambuliwa kuwa ni watu na lutu pamoja na watu wa Sodoma.'Basi, wale malaika Wawili wakaja Sodomaa jioni aliowakaribisha wakae kwake usiku. Lakini watu wa Sodoma wakaja kwenye nyumba yake, wakiuliza kwa namna ya kutisha,'Wawapi wale watu waliokuja kwako usiku huu ?’ Lutu akawasihi,' Watu hawa msiwatende neno’ Taarifa ya maandiko ya Mungu pia inawaita ni'Watu’, Wale watu (Malaika) wakanyoosha mikono yao, wakamwokoa Lutu, Basi wale watu wakamwambia Lutu ….., BWANA ametutuma tuuharibu Sodoma (Mwanzo 19: 1,5,8,10,12,13).

Ufafanuzi wa Agano jipya juu ya matukio haya yanadhibitisha kwamba Malaika wanafanana na umbile la watu. "Msisahau kuwafadhili wageni; Maana kwa njia hii wengine (Kwa mfano Lutu na Abrahamu) waliwakaribisha Malaika pasipo kujua (Ebr 13:2)

Yakobo alishindana usiku kucha na mtu mmoja (Mwa 32:24) ambaye baadae tumeambiwa kuwa alikuwa Malaika (Hosea 12:4)

Watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe walikuwepo kwenye ufufuo (Luka 24:4) na wakati wa kupaa (Mat. 1:10) Yesu, kwa uhakika hawa walikuwa ni Malaika.

Ona vidokezo vya'Kipimo cha Kibinadamu, maana yake cha Malaika’ (Uf 21:17).

MALAIKA HAWATENDI DHAMBI

Malaika wakiwa na mwili wa Uungu, hawawezi kufa, kwa sababu dhambi huleta mauti, Basi wao hawawezi kutenda dhambi. Maneno ya asili katika lugha ya Kiyunani na Kiebrania yaliyotafsiriwa'Malaika’ maana yake ni mjumbe; Malaika ni wajumbe au watumishi wa Mungu, Watiifu kwake, Kwa hiyo hawafikiriwi wao kuwa ni wenye dhambi. Kwa hivyo neno la Kiyunani’Agelos’ lililotafsiriwa'Malaika’ vile vile limetafsiriwa'Wajumbe’ Wanaposemwa wanadamu kwa mfano Yohana mbatizaji, (Math 11:10) na wajumbe wake (Luk. 7:25) wajumbe wa Yesu (Luk. 9:52) na watu walioupeleleza mji wa Yeriko (Yak. 2:25). Kwa kweli inawezekana kwamba'Malaika’ katika maana ya wajumbe wanadamu wanaweza kutenda dhambi.

Mafungu ya maneno yafuatayo ni wazi kwamba Malaika wote (Sio tu baadhi yao) kwa umbile ni watiifu kwa Mungu, na hivyo hawawezi kutenda dhambi.

‘BWANA ameweka kiti chake cha Enzi mbinguni Na Ufalme wake unavitawala vitu vyote (Yaani haiwezekani kuwepo uasi juu ya Mungu mbinguni)Mhimidini BWANA, Enyi Malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkisikiliza sauti ya neno lake Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake Yote; Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake (Zab. 103:19-21)

"Msifuni, enyi Malaika wake wote …. Majeshi yake yote (Zab 148: 2)

Je ! hao wote si roho (Malaika) watumikao, wakitumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu ? (Ebra. 1: 13,14)

Kurudiwa kwa neno'Wote’ linaonyesha ya kwamba Malaika hawajagawanyika katika makundi mawili, kundi moja zuri na jingine lenye dhambi. umuhimu wa kufahamu vema umbile la malaika ni kwamba thawabu ya waaminifu ni kushiriki mwili wao. "Wale wahesabiwao kuwa wamestahili…. Hawaoi wala hawaolewi … wala hawawezi kufa tena. kwa sababu huwa sawa sawa na Malaika (Luk 20:35, 36).

Hili ni neno la muhimu kulishika. Malaika hawawezi kufa'Maana hatwai asili ya Malaika (Kwa kuwa tangu asili hawajatenda dhambi). Ila atwaa asili ya mzao wa Abrahamu -,sababu ya dhambi’ (Ebr 2:16) Ikiwa Malaika waweza kufanya dhambi, Basi wale ambao watakuwa wamestahili thawabu ya Kristo atakapo kuja bado wataweza kutenda dhambi pia, Na kwa kuwa dhambi huleta mauti (Rum 6:23) kwa sababu hiyo hawataweza kuwa na uzima wa milele, kama tukiwa na uwezekano wa kutenda dhambi ni kufanya ahadi ya Mungu ya uzima wa milele haina maana, kwa kufahamu kuwa thawabu yetu ni kushiriki mwili ule wa Malaika. Ushuhuda wa'Malaika (Luk. 20:35,36) unaonyesha kwamba hakuna aina ya Malaika wema na wenye dhambi; ipo aina moja ya Malaika tu.

Ikiwa Malaika waweza kutenda dhambi, Basi Mungu ameachwa hana nguvu za kutenda tendo la haki katika maisha yetu na mambo ya ulimwengu, kwa kufahamu kuwa ameeleza kwamba anafanya matendo yake kwa njia ya Malaika zake(Zab 103:19-21) Wamefanywa kwa'Roho wa Mungu katika maana ya kwamba anatimiza yote kwa nguvu zake. Akitenda kazi katika Malaika (Zab 104:4). Kwamba wanamwasi Mungu haiwezekani. Mkristo amwombe kila siku, Mungu ili ufalme uje duniani, ili mapenzi yake yafanyike kama sasa yanavyofanyika mbinguni (Math 6:10) Ikiwa Malaika wa Mungu iliwapasa washindane na Malaika wenye dhambi huko mbinguni, basi, kwa utimilifu mapenzi yake hayakuweza kufanyika huko, na kwa sababu hiyo hali hiyo hiyo itapatikana kwenye ufalme wa Mungu ujao. Kutumia maisha ya milele kwenye ulimwengu ambao utakuwa ni uwanja wa vita kati ya dhambi na utii, kwa shida hayo sio matazamio ya kutia moyo, lakini hilo, kwa kweli, sio ndiyo suala lenyewe.

MALAIKA NA WATU WANAOAMINI

Ipo sababu nzuri ya kuamini kuwa kila mwamini wa kweli ana Malaika pengine mmoja maalumu-wa kuwasaidia katika maisha yao:-

‘Malaika wa BWANA hufanya kituo, akiwazungukia na kuwaokoa wamchao’ (Zab 34:7)

Mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio (Yaani wafuasi dhaifu- Zek, 13:7 Mat 26:31)…Malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu’ (Mat. 18:6,10)

Wakristo wa kwanza ni wazi waliamini kwamba Petro alikuwa na Malaika mlinzi (Matendo 12:14,15).

Watu wa Israeli walipita katika bahari ya Shamu, waliongozwa na malaika kwenye jangwa kuelekea nchi ya Ahadi. Kutembea kupitia katika bahari ya shamu maana yake ni Ubatizo wetu katika maji (1Kor 10:1), Hivyo nasi vile vile ina maana tusadiki kuwa baadae tunaongozwa na kusaidiwa na Malaika tunaposafiri katika jangwa la maisha kuel;ekea nchi ya ufalme wa Mungu.

Ikiwa Malaika wana weza kuwa waovu katika maana ya kuwa wenye dhambi, basi Ahadi hizi za Malaika kuongoza na kushawishi katika maisha yetu zinakuwa laana badala ya Baraka.

 • Basi tufahamu ya kuwa Malaika ni Viumbe………

 • Wenye mwili ulio sawa na Mungu na huonekana kwa mwili

 • Ambao hawawezi kutenda dhambi

 • Daima hufuata amri za Mungu

 • Wao ni njia ambayo Mungu katika Roho nguvu hunena na

 • kutenda kazi (Zab. 104:4)

LAKINI..?

Makanisa mengi ya'Kikiristo’ yana wazo la kwamba Malaika wanaweza kutenda dhambi, na kwamba Malaika wenye dhambi sasa hivi wapo na wao wanahusika na dhambi pamoja na matatizo yaliyopo hapa Duniani. Tutajadili zaidi vya kutosha juu ya kutofahamu vema jambo hili kwenye somo la 6. Kwa sasa tutatengeneza vipengele vifuatavyo:-

Inawezekana kwamba uumbaji ulikuwepo uliotutangulia sisi wa kweli, yaani huo ulioandikwa katika Mwanzo 1. Pia inaweza kusadikika ya kwamba Malaika waliopo walikuja kuwa na fahamu za'Wema na Ubaya’ (Mwa. 3:5) walipo kuwa katika hali kama hii tuliyonayo katika maisha haya.

Ya kwamba viumbe wengine walioishi kwa kipindi kile walitenda dhambi hatujakatazwa kufikiri; lakini yote haya ni mawazo ambayo mioyo ya watu hupenda kujishughulisha. Biblia yatuambia kile ambacho tunakihitaji kujua kuhusiana na hali iliyopo, ambayo ni kwamba hawapo Malaika watenda dhambi, Malaika wote ni watiifu kwa Mungu kabisa.

Hawawezi kuwepo viumbe wenye dhambi mbinguni, kwa kufahamu kuwa Mungu'ana macho safi na hawezi kuangalia uovu’ (Ab. 1:3) katika maelezo haya, Zaburi 5:4,5 yatuambia:-

‘Mtu mwovu hatakaa kwako. wajivunao hawatasimama mbele za macho yako’ yaani makao ya mbinguni. Jambo la kwamba ulikuwepo Uasi juu ya Mungu mbinguni na Malaika watenda dhambi ni wazo linalopingana kabisa na maneno yaliyotolewa.

Neno la kiyunani lililotafsiriwa'Malaika’ maana yake'Mjumbe’ linataja wanadamu, kama tulivyoonyeshwa'Wajumbe’ wanadamu hawa wanaweza kwa kweli kufanya dhambi.

Ya kwamba upo uovu, viumbe wenye dhambi ambao juu yao mwelekeo wa maisha yote yasiyofaa wanaweza kutupiwa lawama kwa kawaida ni moja ya Imani zaidi iliyoshikiliwa katika Upagani.Kwa njia hiyo hiyo mambo yanayohusu Krismas yameingia kwenye kile kinachodhaniwa ni'Ukristo’ Basi, vile vile Ukristo una fikra hizo za Kipagani

Yapo mafungu ya maneno ya Bibilia yaliyojaa tele ambayo yanaweza kutoeleweka kusaidia wazo hili la Malaika wenye dhambi kwa sasa wapo. Haya yamepimwa katika 'Kumsaka Shetani’ yanapatikana kwa wachapishaji - Mafungu haya ya maneno hayawezi kuruhusiwa kupingana na mafunzo tele ya Biblia kwa kutofautiana na haya yaliyokwisha tolewa.


  Back
Home
Next