Misingi Ya BIBLIA
Somo La 1: Mungu
Uwepo wa Mungu | Nafsi yake Mungu | Jina La Mungu Na Tabia Ya Sifa Yake | Malaika | Tumeacha Kitambo sehemu ya ("Mungu ni roho" (Yohana 4:24), "Matumizi ya jina la Mungu", "Ufunuo wa Mungu") | Maswali

1.2 Nafsi yake Mungu

Ni mwenye enzi, Mungu aliyeandikwa katika Biblia na kwamba ni kweli, mtu wa kugusika, naye yupo katika umbo. Vilevile ni mafunzo ya kwanza ya Ukristo kuwa Yesu ni mwana wa Mungu. Ikiwa Mungu hana umbo , basi haiwezekani yeye kuwa na mwana ambaye alikuwa ni 'Chapa ya nafsi yake' (Ebr 1:3) Tena inakuwa vigumu kuendeleza maisha ya uhusiano wake na mungu ikiwa Mungu ni wazo lililo kwenye akili zetu, Mkusanyiko wa roho mahali popote juu katika anga lisilo na kitu. Ni huzuni kusikia kwamba dini za watu wengi zina wazo lisilo la kweli lisilotambulika kuhusu Mungu. Yeye akiwa mkubwa mno kuliko sisi, inaeleweka ya kwamba imani ya watu wengi imeweka kikwazo kwenye ahadi dhahiri kuwa mwishowe tutamwona Mungu. Israeli walikosa imani ya kumwona Mungu alivyo (Yoh. 5:37) ni dhahiri ana umbo halisi, Imani hii huja kutokana na kumjua Mungu kwa kuamini neno lake

Heri walio safi wa moyo, Maana watamwona Mungu (Math 5:8)

Na watumwa wake (Mungu) watamtumikia, nao watamwona uso wake, na jina lake(Jina la Mungu) litakuwa katika vipaji vya nyuso zao (Uf 22:3-4)

Tumaini hili la ajabu kama kweli tunaliamini litaonyesha matokeo ya matendo kwenye maisha yetu:

  • Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao hakuna mtu atakaye mwona Bwana asipokuwa nao (Ebr 12:14)

  • Tusiape, kwa kuwa aapaye kwa mbingu, Huapa kwa kiti cha Mungu na kwa yeye na kwa yeye aketiye juu yake (Math 23:22) hii itakuwa haina maana ikiwa Mungu sio mtu mwenye mwili.

  • Tutamwona kama alivyo (akidhihirika katika kristo) na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu (1 Yoh 3:2,3)

Katika maisha yetu haya kumfahamu Mungu wetu wa mbinguni, hakujakamilika sana. Tunaweza kutazama mbele, kupitia giza linalotatanisha la maisha haya hadi mwisho wa kukutana naye. Kumwona kwa macho yetu hapana shaka kutakuwa sawa na kumfahamu kwa akili zaidi. Kutoka vina vya masumbufu ya mwanadamu. Ayubu aliweza kufurahia uhusiano wake wote na Mungu ambao utimilifu wake atauona mwisho wa siku.

Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi (Yaani katika mauti),Lakini pasipokuwana mwili wangu (Yaani pasipo mwili unaoharibika) nitamwona Mungu;Nami nitamwona mimi nafsi yangu,na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine (Ayubu 19:26,27)

Mtume Paulo aliyatazamia maisha mengine yasiyo machungu yasiyo na msukosuko: "Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; Wakati ule tutaona uso kwa uso" (1Kor 13:12)

USHAHIDI WA AGANO LA KALE

Ahadi hizi zilizo katika Agano Jipya zimejengwa juu kwenye ushahidi wa mambo yake makubwa ya Agano la kale, Kuwa ni Mungu aliye na mwili. Ushahidi hauwezi kukaza zaidi lakini ni mwanzo wa kukubali hali ya Mungu kama tunataka kuwa na ufahamu wa kweli yoyote kuhusu dini ambayo msingi wake upo kwenye Biblia. Agano la Kale lina mazungumuzo ya Mungu kuwa ni mtu na mtu uhusiano wa mtu na mtu pamoja Mungu, ambao Agano la Kale na Jipya linausema ni wa pekee kwa tumaini la Ukristo wa kweli. Yafuatayo ni majadiliano ya nguvu kwa ajili yake, Mungu aliye na mwili.

"Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu" (Mwa. 1:26) Hivyo mtu amefanywa kwa mfano na sura ya Mungu, Kama ilivyodhihirika kupitia Malaika. Yakobo 3:9 anasema … Wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu. Maneno haya hayatumiki kutaja mfano wa akili ya mwanadamu, kwa kuwa hali ya fikra zetu zipo mbali kabisa toka zake Mungu na katika njia nyingi kwa kikubwa zimepingana na haki yake."Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu, asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu" (Isa 55:8 - 9). Kwa hiyo mfano na sura, tunavyoshirikiana naye Mungu, inabidi uwe ni mfano wa mwili- Lakini yeye hana wa dhambi.

Popote Malaika walipoonekana duniani wamesemwa kuwa wana umbo la watu, kwa mfano, Abrahamu aliwakaribisha malaika bila kujua, akizania kuwa walikuwa watu wa kawaida. Sisi jinsi tulivyoumbwa kwa mfano wa Mungu kwa kweli maana yake ni kwamba tunaweza kufahamu jambo lingine kuhusu mtu halisi, ndivyo tulivyo, lakini tunafanana. Basi, Mungu tunaye mshabihi siyo mtu mwingine asiyedhahiri ambaye hatuwezi kumfikiria.

"Wao wenyewe Malaika wanafanana na Mungu. Hivyo Mungu aliweza kumsema Musa, "Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, maana wazi wazi wala si kwa mafumbo. Na umbo la Bwana yeye ataliona" (Hesabu 12:8) Haya yalikuwa yanamtaja Musa, akifunzwa na Malaika aliye kuwa na jina la Bwana (Kut. 23:20:21) Ikiwa Malaika alikuwa na umbo la Bwana, Inaonyesha kuwa Mungu amefanana na Malaika Yaani - Kimwili ana umbo la Mwanadamu. "BWANA alisema na Musa uso kwa uso kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. (Kut. 33:11: Kum. 34:10). Bwana alijidhihirisha katika Malaika wake, ambaye uso na kinywa alifanana na Bwana mwenyewe.

"Kwa maana yeye anatujua umbo letu, (Zab. 103:14).Ana tutaka yeye, tumfikirie kuwa ni mtu, Baba ambaye tunaweza kuunganishwa naye.Huyu ataelezwa kwa ushahidi mwingi wa mikono ya Mungu, Viganja,Macho n.k. Ikiwa Mungu alikuwa ni furushi la Nafsi mahali fulani katika mbingu, ambazo inabidi ziwe Mungu, ni wazo letu kama tukitaka utu wake; basi ushahidi huu unatupotosha kukuza kusudi lolote.

"Maelezo ya sehemu ya makao ya Mungu, Wazi wazi yanaonyesha kwamba "Mungu" ana mahali pake; "Mungu yuko Mbinguni"(Mhubiri 5:2);Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu, toka mbinguni BWANA ameiangalia nchi (Zab 102:19,20); "Usikie huko mbinguni, Makao yako" (1Fal. 8:39). Lakini kwa kupambanua zaidi kuliko hivi tunasoma kwamba Mungu ana "Kiti cha Enzi" (2 Nya. 9:8, Zab 11:4; Isa. 6:1,66:1).Lugha kama hii ni ngumu kuitumia nafsi isiyo wazi kabisa, inayokaa katika milki ya Kimbingu. Mungu amesemwa kuwa "Ameshuka kuja chini" wakati mwenyewe anapojidhihirisha. Hapa panadokeza makao ya Mungu yaliyo mbinguni. Inakuwa vigumu kueleza wazo la udhihirisho wa Mungu bila kukubali hali ya umbo la Mungu. Isaya 45 ina ushahidi tele wa Mungu kujihusisha kwake katika mambo ya watu wake: "Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine ….., mimi ni BWANA anayetenda haya yote …., Mimi, BWANA nimeiumba Ole wake ashindanaye na Muumba wake … Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu …, niangalieni mimi mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia. mstari hasa kweli huu wa mwisho unaonyesha uwepo wake Mungu - Anawataka watu wamwangalie yeye, Kuwaza uwepo wake halisi pamoja na jicho la imani.

Mungu amejifunua kwetu akiwa ni mwenye kusamehe anayesema, maneno kwa watu. Hata hivyo msamaha na usemi unaweza tu kutoka kwa mtu: ni matendo ya akili, Hivyo Daudi alikuwa ni mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu (1 Sam 13: 14), inaonyesha kwamba Mungu ana moyo, unaoweza kunakiliwa kwa kiwango kidogo na mtu, ingawa mwanadamu wa mwili haupendezi moyo wa Mungu. Mafungu ya maneno kama BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani akahuzunika moyo (Mwa. 6:6), hufunua hisia ya Mungu, mwenye ufahamu kuliko kuwa kishindo cha roho ya kuwazika katika hewa. Hapa tunasaidiwa tukubali jinsi kwa kweli tunaweza pande zote mbili kumpendeza na kutokumpendeza, Kama mtoto anavyoweza kwa baba wa mwili.

IKIWA MUNGU SI MTU MMOJA

Kama Mungu si wa kweli, mmoja mwenye kuwepo, Basi wazo la kupenda mambo ya roho ni vigumu kushikana nayo. ikiwa Mungu ni mwenye haki kabisa lakini si mtu mwenye umbo, basi kwa kweli hatuwezi kuiwazia haki yake ilivyodhihirika kwa watu. Pande zote mbili, Ukristo uliokenguka na wayahudi wana wazo la kwamba haki ya Mungu inaingia katika maisha ya watu kwa njia ya

‘Roho Mtakatifu’ Asiyedhahiri ambaye kwa namna isiyoeleweka tunafanywa mfano kwenye akili ya Mungu, na kukubalika kwake. Kwa maneno mengine, mara tukitambua ya kwa mba yupo mtu mwenyewe aitwaye Mungu, basi tunaweza kurekebisha tabia yetu kufuata atakavyo, Kwa msaada wake utokao kwenye ushawishi wa neno lake na kwa kuleta sifa inayoonyesha tabia ya Mungu katika utu wetu.

Lengo la Mungu ni kujidhihirisha mwenyewe katika mkutano wa watu waliotukuzwa. Jina la kumbukumbu yake, YEHOVA ELOI, linamaanisha hivi (Atakaye kuwa kwa wenye nguvu ni tafsiri iliyo karibu sahihi.) ikiwa Mungu si mtu mwenye umbo, basi thawabu ya waaminifu katika ufalme wa Mungu ujao duniani inaonyesha ya kwamba watakuwa nayo wazi tena dhahiri wakiwepo katika mwili, Ingawa hawatakuwa katika udhaifu wa mwili wa Mwanadamu tena. Ayubu alitamani' Siku ya mwisho’ atakapofunguliwa na mwili wake (Ayubu 19:25:27); Abrahamu itabidi awe mmojawapo wa wale wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi ambao wataamka…… Kwa uzima wa Milele wa nchi ya Kanani (Dan. 12:2) hivyo basi ataweza kupata ahadi ya urithi wa milele wa nchi ya kanaani, Sehemu inayoonekana katika dunia hii

(Mwa. 17:8.) " Na wataua wake watashangilia….. waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao….. ili kufanya kisasi juu ya mataifa (Zab 132: 16; 149: 5,7) Kushindwa kwa watu wote wa pande mbili, Wayahudi na watu wa mataifa,

Kutambua mafungu ya maneno kama haya vyema, kwa ukubwa wa maneno yenyewe Kuletwa ahadi za kuonekana kwa Abrahamu, kumeongoza watu kwenye imani potovu la' Nafsi haifi’ ya kwamba Mwanadamu halisi anakuwepo hai akifa. Wazo hili halina msaada wa Biblia kabisa. Mungu hapatikani na mauti, Mtu mwenye utukufu, analifanya lengo lake, ili kwamba wanaume na wanawake waweze kuitwa na kuishi katika ufalme wake ujao kwenye dunia hii, Kushiriki sifa, zilizoelezwa katika umbo la mwili.

Waaminifu wameahidi wa kwamba watarithi mwili wa Mungu (2 Pet. 1:4) Ikiwa Mungu si mtu mmoja, basi hii ina maana tutaishi milele kwa roho zisizo na mwili. Lakini hili si fundisho la Biblia. Tutapewa mwili kama ule wa Yesu. (Flp. 3:21), Nasi tunajua kwamba tutakuwa na mwili halisi kwenye ufalme mwili utakaokuwa na mikono macho na masikio (Zek. 13:6, Isa. 11:3), mafunzo ya Mungu kuwa ni Mmoja, kwa sababu hii yanasimulia Injili ya Ufalme.

Itakuwa wazi kwamba hakutaweza kuwa na wazo la kujua Ibada, dini au uhusiano mmoja na Mungu mpaka itambulike kuwa Mungu ni mtu mmoja, na kwamba kwa mwili sisi ni mfano wake. Ingawa ni mfano usio kamili sana unahitajika kuukuza kufuata mfano wa akili yake, Hivyo basi, tutaweza kupata utimilifu wa mfano wake unaoonekana katika ufalme wa Mungu. Maana nyingi zaidi na faraja tunaweza kupata kutoka mafunzo ya maneno ambayo yanamtaja Mungu kuwa ni Baba aliye na upendo, akiturudi kama Baba afanyavyo kwa mwanae (mfano. Kum. 8:5). Katika maneno yenyewe ya mateso ya Kristo tunasoma kwamba,'Lakini BWANA aliriidhika kumchubua’ (Isa. 53:10),Ingawa "Alimlilia Mungu" aliisikia sauti yangu…….. Kilio changu kikaingia masikioni mwake (Zab.18:6). Ahadi ya Mungu kwa Daudi kuhusu mzao atakaye kuwa ni mwana wa Mungu ilitakiwa azaliwe kwa Muujiza kwa Mwanadamu; Ikiwa Mungu hakuwa ni mtu mmoja, asingekuwa na mwana huyo.

Kumfahamu Mungu kwa usahihi ni ufunguo unaofungua maneno mengi mengine ya muhimu katika mafundisho ya Biblia. Lakini kama uongo mmoja huongoza kwenye uongo mwingine, Hivyo dhana potovu juu ya mungu inaficha utaratibu wa kweli ambao maandiko yanatoa. Kama umepata kuona kuwa hii sehemu inadhibitisha, au hata ikiwa ni ndogo, basi, swali linakuja. Je? Unamjua Mungu kweli?. Sasa tutachunguza maandiko ya Biblia zaidi kuhusu yeye.


  Back
Home
Next