Misingi Ya BIBLIA
Mwishoni Mwa Kitabu
1: Maelezo Mafupi Ya Msingi Wa Mafunzo Ya Biblia | 2: Tabia Yetu Kujifunza Biblia | 3: Kristo Amekaribia Kurudi | 4: Haki Ya Mungu

Mwishoni Mwa Kitabu 4: Haki Ya Mungu

Kufundisha wanafunzi wa Biblia kumedhihirisha kuwa idadi ya maswali yanayohusiana mara nyingi hutokea wakati wa kusoma kukikamilika. Yote haya yanalenga karibu haki ya Mungu. Mifano ina:

Je! sio kweli kila mmoja anaitwa na Mungu aijue Injili.

Ni kwa sababu gani Mungu aliruhusu Adamu na Hawa kutenda dhambi, na hivyo kuleta masumbufu na shida katika maisha ya watoto wao mabilioni.

‘Kwa nini Mungu alichagua Israeli tu kuwa watu wake katika Agano la Kale, kuliko kumpa kila mmoja nafasi?

Shida hizi zitatokea kwetu sisi sote,hatua iwayo yote kwenye uhusiano wetu na Mungu. Mambo haya kupata kuwa magumu kuyaelewa yenyewe isiwe sababu ya kuchelewa kuitikia mwito wa Mungu. Upande huu wa kundi la Kristo, hatutaweza kamwe kufikia cheo cha mwisho wa maarifa kuhusu hayo. Miaka elfu mbili iliyopita, mtu "alipaza sauti aksema kwa machozi, Bwana naamini nisaidie kutoamini kwangu" (Marko 9:24). Sote tuna utu huu uliogawanyika; nusu tunaamini, lakini upande mwingine umetiwa katika daraja ya "wasio na imani" wakihitaji mno msaada wa Bwana kunyamazisha. Katika masiku au juma kabla ya ubatizo, hili ni wazo linaloonekana kwa kawaida, na kwa kiwango kingine itatokea tena siku zetu zote.

‘Kutoamini’ kwetu mara nyingi kunachukua mfano wa aina ya mifano ya maswali kwa Mungu yaliorodheshwa hapo juu. Jambo la msingi kwa macho ni kwmaba haidhaiwi ya kwamba tutamlaumu Mungu kuwa hana haki au si kweli. Kama tukifanya hivyo tunamhukumu Mwenyezi Mungu kwa maneno ya kuona kwetu. Tunasema ya kuwa kama tungekuwa ni Mungu, tungetenda kwa namna tofauti kwa jinsi gani Mungu anafanya. Ni moja ya makosa makubwa ya mwanadamu kutofahamu ni jinsi gani binadamu alivyojaa dhambi, na haki ya Mungu ya mwisho. Kama Mungu hayupo sawa mwisho, basi hakuna jambo la uadilifu linalopima ubora wa uwepo wote. Kwa hiyo hakuna dhana kweli ya sawa au kosa. Wazo zima la dini (kufungamana tena) na Mungu kwa hiyo halina maana. Kama watoto wanaweza kuwa na akili ya kuwafahamu watu wazima kwa upeo wao wa kuona na mfano wa kufikiri, ndivyo ilivyo mtu kwa Mungu. Yeremia alihoji njia ya Mungu, lakini katika juhudi kumfahamu kwa kina zaidi Mungu ndipo mwisho alikubali kuwa Mungu yupo sawa: "Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki (Yer 12:1; linganisha Zab 89:19,34,49,52).

Kidokezo cha kwamba Mungu hana haki kinatoa wazo la kwamba sisi tuna haki fulani, ambazo kwa njia isiyoeleweka Mungu anaharibu. Ukweli kwamba Mungu ndiye muumba wetu na ndiye mwenye kutufanya hai siku zote maana yake hatuna haki. Daima tunaishi katika huruma yake sio tu tunapokosa. ‘Haki za binadamu’ ni wazo la kibinadamu, limeundwa na wanadamu kwa kujihesabia haki mwenyewe. Tulikuja ulimwenguni bila kitu, na tutaondoka bila kitu. Yote tulionayo ni kipawa, tumepewa kwa kitambo kidodo kuona ni jinsi gani tutaitika. Ikiwa Mungu anatuita sisi kwenye uhusiano wa karibu naye, kwa furaha tuitikie. Kukataa kufanya hivyo kwa sababu wengine hawajaitwa kufanya hivi, ni kumhuzunisha Mungu katika moja ya njia ziwezazo kutia uchungu zaidi.

Kwa umbile sisi sote ni wanyama (Mhubiri 3:18-20). Tunaweza kusema, ‘ni kwa sababu gani mwanadamu alichaguliwa kuwa na uhusiano na Mungu, kuliko mnyama mwingine yeyote?’ Sababu hasa hatuwezi kufahamu hata kama tungeambiwa. Moja ya kweli na taarifa ya uumbaji katika kitabu cha Mwanzo. Maelezo ya kisayansi ya jinsi gani Mungu aliumba vitu vya kuonekana na kuratibu katika ajabu isiyo na kikomo ya ulimwengu ni nje ya uwezekano wa sayansi ya binadamu kufahamu. Kwa hiyo Mungu alieleza matendo yake ya uumbaji katika lugha ambayo mwenye hali kama mtoto aweza kukubali. Yayo hayo kwa uadilifu wa kuchagua katika mambo mawili ambayo tuliorodheshewa mwanzoni mwa maneno haya ya ziada mwishoni mwa kitabu. Kitabu hiki kimeeleza fundisho la Biblia kuhusu mambo haya. Kwa kawaida akili zetu hazinyenyekei katika neno la Mungu; tutakuwa na shida ya kufahamu na kukubali baadhi ya mambo katika njia ambayo Biblia inayaelezea. Lakini tunatakiwa kutambua ya kuwa tatizo ni letu, na sio Mungu. Kwa upana tunakosa maarifa binafsi yanayotakiwa kukubali kwamba kimsingi fikira zetu zina kasoro na makosa. Yatupasa tuelewe ukweli wa kwamba akili zetu tumeharibika mno zipotofauti na Mungu. Njia yetu ya kufikiri sio tu ni hatua kushuka chini toka kwa Mungu; kwa ukubwa ni wazo tofauti katika maendeleo na yake. Kwa sababu hii tumetakiwa kuwa na akili ya Kristo, kujifunza katika neno la Mungu kufahamu njia yake ya kufikiri, na kujaribu kufanya iwe yetu.

Sisi sote tutakiri kuwa kuna vitu vingi vya uumbaji wa Mungu ambavyo ni wazi ni vizuri sana; ni bayana kuna wazo lingine la haki linalotoka kwa muumba wetu, na liko wazi katika uumbaji wake. Tatizo ni, kuna mambo mengi tunayoyaona wanadamu ambayo mengine ni wazi maovu na yasiyofaa. Ni haya yanayosababisha machafuko mengine kama kuhoji haki ya Mungu. Kwa huzuni, wakati huo wengi wanaendelea kuionea shaka haki ya Mungu, na hata ikiwa yupo. Lakini sio bora zaidi kusema kuwa tunaamini ukuu wa wema wa Mungu na haki, kama anavyodai katika neno lake, lakini tuna shida kufahamu mahali pa ubaya katika uumbaji wake?

"Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu: lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi" (Kum 29:29). Injili imeitwa "mambo ya Mungu yanayojulikana" (Rum 1:19), inadokeza kuna mengi mengine ambayo bado kujulikana. Kuna mambo ya kweli makuu ambayo ni wazi tunaweza kuona katika Neno la Mungu; pia kuna sifa nyingine za Mungu zinazoendelea . Lakini mengine yasiohesabika yapo "mambo ya siri" yanahusu njia za Mungu, ambazo hatuwezi kuzipita kwa kuzifikia katika maisha haya. Hivyo Paulo aliweza kusema kuwa katika maana moja alimjua Kristo na Mungu, kama tuwezavyo sisi (2 Tim 1:12; 2Kor 5:16; Gal 4:9; Ebra 10:30; 1Yoh 2:13), hasa kwa kuona wenyewe upendo wa Mungu na kuitikia (1 Yoh 4:7,8); ila kwa maana nyingine "alijua kwa sehemu" (1 Kor 13:9,12), kutamani kurudi Kristo, "ili (wakati huo) nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake" (Flp 3:10).

Kama tunavyoogezeka kufunukiwa na haki ya Mungu kwa njia ya kujifunza neno lake, tutaongezeka kutamani kuwa Ufalme wake uje wakati hatimaye sifa zake zenye haki zitakuwa dhahiri, kwa mwili zitafunuliwa kwa namna ambayo watu wake wote kwa furaha watafahamu na kupenda.Kipindi hicho wataona ufumbuzi wa mwisho wa shida zote ambazo sasa zinawatesa watoto wa Mungu - kiakili, kwa mema na mabaya na kwa mwili. "Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo, kwa jinsi ya fumbo, wakati ule tutaona uso wa uso, wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama nami ninavyojuliwa sana " (1 Kor 13:12,13).


  Back
Home