| Mwishoni Mwa Kitabu 1: Maelezo Mafupi Ya Msingi Wa Mafunzo Ya Biblia
MUNGU
 
Yupo mtu mmoja aitwaye Mungualiye na mahali maalum katika mbingualiye hai mwenye mwili halisiambaye tumechukuwa sura yakeMalaika ni wajumbe wakeambao hawatendi dhambi,wakishiriki tabia ya Mungu.Lipo umbo moja tu la kuwapo hai limefundishwa na Biblia - uwepo katika umbo la mwili. Mungu na Malaika wanaishi katika umbo la kimwili. Tumaini la Mkristo ni kupewa tabia ya Mungu katika umbo la kimwili Kristo akirudi. 
ROHO YA MUNGU
 
Inapotajwa Roho ya Mungu ni uweza wake, pumzi na akili,ambayo kwayo anatimiliza mambo yotena kuwepo kila mahali.Roho Mtakatifu anatajwa uwezo huu uliotumika kutimiza miishi fulani.Kwenye nyakati mbalimbali zamani, watu wamekirimiwa kuwa na vipawa vyenye miujiza ya Roho.Hivi vimeondolewa,Uweza wa Mungu sasa umefunuliwa kwetu katika neno Lake.Roho Mtakatifu hawashurutishi watu kuwa wa kiroho kinyume na mapenzi yao wenyewe.Biblia ilivuviwa na Roho wa Mungu kabisa.Biblia tu ndio yenye mamlaka yetu katika uhusiano wetu na Mungu. 
AHADI ZA MUNGU
 
Injili ilihubiriwa kwa namna ya ahadi zilizofanywa kwa mababa wa Kiyahudi.Uzao wa mwanamke katika Mwa 3:15 unataja Kristo na wenye haki, "waliochubuliwa" na wanachubuliwa kwa muda na dhambi, uzao wa nyoka.Kwa kutimilika ahadi za Mungu, sayari duniani haitaharibiwa.Uzao wa Abrahamu na Daudi alikuwa ni Kristo;twaweza kuwa ndani ya Kristo kwa kuamini na ubatizo,kwa hiyo basi ahadi hizi zinawahusu waamini wa kweli. 
MUNGU NA MAUTI
 
Kwa tabia mwanadamu ni mfu, mwenye kuelekea kutenda dhambi, naamelaaniwa kwa matokeo ya kosa la Adamu. Kristo alikuwa na huu mwili wa kibinadamu.Nafsi hutajwa ‘sisi’, mwili wetu, mawazo au mtu.Roho ni kutaja nguvu za uhai wetu/pumzi na silika.Hakuna mtu awezaye kuishi akiwa na roho pasipo mwili.Mauti ni hali ya kutokuwa na fahamu.Atakaporudi Kristo kutakuwa na ufufuo wa mwili kwa wale tu wenye kuijua Injili ya kweli.Maarifa na kufahamu Neno la Mungu vitakuwa msingi wa hukumu.Kupewa kabisa kutokufa kutatokea kwenye kiti cha hukumu.Adhabu ya waovu wahusika itakuwa mauti ya milele.‘Kuzimu’ ni kaburi.‘Jehanamu’ lilikuwa eneo nje ya Yerusalemu mahali pa takataka na walipochomwa wavunja sheria. 
UFALME WA MUNGU
 
Watu wa Israeli walikuwa Ufalme wa Mungu zamani.Huu uliisha sasa, lakini utaanzishwa tena Kristo akirudi, kwa namna ya kuwa wa  kuenea pote Ufalme wa Mungu duniani, ukitawaliwa na Kristo kwa niaba ya Mungu.Miaka 1000 ya kwanza (au ‘Kikwi’) ya huu Ufalme itaona waamini wa kweli wa zama zote watakuwa hai Kristo akirudi.Kwa hiyo sasa Ufalme kiutawala haujaanzishwa.Tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani yetu, wala si kwa matendo yetu. 
MUNGU NA UBAYA
 
‘Ibilisi’ kwa maana ya neno ni ‘mshitaki’ au ‘msingiziaji’‘Shetani’ kwa maana ya neno ni ‘adui’,laweza kutumika kutaja watu wa pande mbili wema na wabaya.Kwa mfano ibilisi na shetani yaweza kutajwa dhambi na mwili wa nyama.Nyoka wa Edeni alikuwa mnyama halisi;taarifa ya kitabu cha Mwanzo ya uumbaji wa mtu na kuanguka ieleweke ilivyo si kwa maneno ya kimfano.‘Mashetani’ kama roho iliyojaa dhambi, roho waliotoka au nguvu ya dhambi hawapo.Kristo ‘kuwatoa pepo’ yaweza kufahamika kama sehemu ya lugha ambayo kwa namna yake inamaana ya kuwa aliponya magonjwa.Lusifa hatajwi Malaika aliyejaa dhambi.Mungu ni mwenye nguvu zote; hashirikiani uweza wake na kiumbe awaye yote mwenye dhambi apingaye  njia zake.Majaribu katika maisha ya aaminiye mwisho huja toka kwa Mungu wala sio kwa matokeo ya  ‘bahati mbaya’ au kwa kiumbe mwenye dhambi sana aitwaye Ibilisi. 
YESU KRISTO
 
‘Utatu’ kama kwa upana unavyofahamika katika Ufalme wa Kikristo ni elimu ambayo haijafundishwa katika Biblia.Kristo alizaliwa na bikira Mariamualiyekuwa mwanamke wa kawaida mwenye mwili wa kibinadamu.Yesu alikuwa na mwili wa kibinadamu,ila alikuwa na tabia timilifu isiyo na dhambi,ingawa Mungu hakumshurutisha kutofanya dhambi; Yesu alikufa kwa hiari yake mwenyewe akiwa dhabihu timilifu kwa dhambi.Yesu alifufuliwa baada ya mauti yake msalabani.Kabla ya kuzaliwa Yesu hakuwahi kuishi,ingawa alikuwa katika nia/ kusudi la Mungu tangu mwanzo.Yesu alikufa akiwa sadaka kwa ajili ya dhambi zetuili kupata wokovu kwa ajili yetu na yeye mwenyewe.Yesu alikufa akiwa mwakilishi wetu.Sio badala yetu kama kwa upana inavyoaminika na ufalme wa Kikristo.Kwa kifo cha Kristo Torati ya Musa ilikoma,Kwa sababu hiyo haitupasi kuitunza sasa, pamoja na Sabato. 
UBATIZO
 
Bila ubatizo, hakuna tumaini la wokovu;kuamini na kubatizwa kunatuingiza kushiriki ahadi za Abrahamu, na kwa kupata msamaha wa dhambiUbatizo ni kwa kuzamishwa ndani kabisa ya majimtu mzima aliyeijua Injili.Hao waliozamishwa pasipo kuwa na elimu ya kutosha kwa Injili hawana budi kubatizwa tena. Kwa uzuri.Kufahamu Injili ya kweli unahitaji ubatizo kuwa thabiti. 
MAISHA KATIKA KRISTO
 
Baada ya ubatizo, mwamini hanabudi kufanya bidii yenye akili kujitenga katika njia zilizojaa dhambi za ulimwengu,na kuendeleza tabia yenye sifa kama Kristo.Kujishirikisha katika shughuli za anasa zitakazopeleka kuvunja maagizo ya Mungu, k.m kutumia nguvu na unywaji pombe kupita kiasi, haiwezi kupatana kwa kweli na maisha ya Kristo.Waamini waliobatizwa wana wajibu kukutana na kushirikiana, popote wakati wowote kibinadamu ikiwezekana.Waamini waliobatizwa kila mara wamege mkate na kunywa divai kwa ukumbusho wa dhabihu ya Kristo.Sala ya kila mara na kusoma Biblia ni muhimu kwa mwamini aliyebatizwa.Mwamini aliyebatizwa tu ana ushirika na wale ambao wanashika mafundisho ya kweli na kujaribu kwa hali ilivyo kutenda kazi.Kwa hiyo ambaye anakoma kuamini au kuitendea kazi ile Kweli anakoma kuwa mshirika wa mwili wa waumini. Angalia: Taarifa ya Imani moja ya utaratibu ambao umekuwa ukitumika zaidi ya miaka 100 unapatikana kwa wachapishaji. |