Misingi Ya BIBLIA
Mwishoni Mwa Kitabu
1: Maelezo Mafupi Ya Msingi Wa Mafunzo Ya Biblia | 2: Tabia Yetu Kujifunza Biblia | 3: Kristo Amekaribia Kurudi | 4: Haki Ya Mungu

Mwishoni Mwa Kitabu 2: Tabia Yetu Kujifunza Biblia

Yawezekana kabisa kujifunza mafunzo ya msingi wote wa Biblia lakini akashindwa kufahamu hali ya kweli yenyewe kwa ujumbe wake. Ukweli huu unaweza kuwa wakuleta huzuni sana kwa wale ambao hutumia kitabu cha mafundisho kama hiki na maelezo kwa wengine ambao wakati huo wanaonekana kushindwa kushika mambo yaliyozungumziwa.

Watu waliitikia kwa kweli kwenye mahubiri ya Injili katika karne ya kwanza. Watu "walilipokea neno" la Injili wakabatizwa (Mdo 2:41). Bila kuguswa na ujumbe moyoni - "imani yenye moyo wa kupenda", kama Robert Roberts mara nyingi alivyoielezea - hakuna maana ya kubatizwa. Wale ambao wapokea ujumbe tu kwa sababu ya kusongwa na wenza wao au wazazi hawaelekei kusimama kwenye mwendo. Kwa kuwa tunavutiwa na kuwaleta watu kwenye wokovu kuliko kuwa na idadi ya wanaobatizwa, inafaa kuchukua muda wa kuhubiri kwetu Injili na kuhakikisha kwamba waongofu wetu wanaujia ubatizo na msimamo ulionyooka.

Wale Waberoya "walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo wakayachunguza maandiko kila siku" kuchunguza kile alichohubiri Paulo (Mdo 17:11). Kitabu hiki cha mafundisho - kwa kweli vitabu vyovyote vya mwanadamu vyenye ufasaha - ni jaribio tu la kufikiri kwa usahihi fundisho la Biblia. Kwa maana ili pawepo uitikiaji wa kweli wa Injili, inabidi iwepo akili nyepesi kusikia Neno, kwa kweli ukitamani kuchunguza maandiko kwa usawa wake. Hili ndilo jambo fulani ambalo muhubiri wa Injili kwa ulazima hawezi kulileta; tunaweza tu kuvuta macho kuangalia mafungu ya Biblia yanayohusu jambo lenyewe. Waumini wa pale Rumi "walitii kwa mioyo yao ile namna ya elimu ambayo waliipokea" kabla ya wao kubatizwa (Rum 6:17).

Wale ambao kwa ukaidi wanadumu katika njia za mwili kamwe hawata weza kufahamu vema ujumbe wa kweli ya Injili; wataishi wakiwa "wenye mfano wa utauwa, huku wakikana nguvu zake……. Wakijifunza siku zote, lakini wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli" (2 Tim 3:1-7). Kamwe hatufahamu kile tusichotaka. Kama hatuipendi hasa haki, hakuna haja kweli ya kuleta maisha yetu chini ya uongozi wa Mungu, kamwe hatutaweza "kufikia ujuzi wa kweli", pamoja na kusoma kwetu Biblia; kujifunza kwetu kutakuwa ni kufanya mazoezi tu ya kujizoeza kusoma bila maana.

Kuna mifano kadhaa ya watu wakisoma Maandiko, lakini si kwa namna ya kuyasoma. Huu ni ugonjwa ambao sote sisi tunaelekea. Wayahudi wakati wa Kristo walionekana kuwa na juhudi kubwa kwa ajili ya neno la Mungu; waliyaamini maandishi ya Agano la Kale kuwa yalivuviwa (Yn. 5:45; Mdo 6"11); walijua ya kwamba kwa kusoma Maandiko haya wanaweza kuwa na tumaini la uzima wa milele (Yohana 5:39), na kila juma walisoma mbele ya watu (15:21). Kwa nyongeza, baadhi yao kwa karibu walisoma mafungu haya ya maneno wakati wa juma. Walakini, walishidwa kabisa kufahamu maana halisi ya Maandiko haya, kwa kuwa yalilenga mbele kwa Kristo. Yesu aliwaambia wazi wazi: "Mwayachunguza Maandiko……… kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi: kwa sababu yeye aliandika habari zangu. Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu? Msipowasikia Musa na manabii" (Yohana 5:46,47; Luka 16:29-31).

Tunaweza kufikiri uchungu wa Wayahudi: ‘Lakini tunafanya kuisoma Biblia! Tunafanya kuiamini! Ila, kwa sababu ya tabia yao ya karibu, kwa namna ya kipekee hawakufanya hivyo - wanasoma, ila hawakuielewa; walitazama, lakini hawakuona. Kwa kweli hakuna walio vipofu kama hao wasiotaka kuangalia. Katika hatua zote kwa maendeleo yetu ya kiroho yatupasa kujilinda sana juu ya jambo hili.


  Back
Home
Next