Misingi Ya BIBLIA
Somo La 10: Kubatizwa Katika Jina La Yesu
Maana Muhimu Sana Ya Ubatizo | Tubatizwe Jinsi Gani? | Maana Ya Ubatizo. | Ubatizo Na Wokovu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Kubatizwa tena, Kiwango cha elimu itakiwayo kabla ya kubatizwa, Mnyang'anyi Msalabani, Mfano wa huduma ya Ubatizo) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 31: Kiwango cha elimu itakiwayo kabla ya kubatizwa

Wasomaji wengi watakuwa wamewahi kukabiliwa na hao walio katika makanisa ya ‘Kiinjili’ wanao hoji ya kwamba mafundisho hayana umuhimu katika wokovu, na ya kwamba maneno tu ya kuungama kuwa ‘Nina amini, Yesu Kristo ni mwana wa Mungu’ ni sharti la msingi kupata wokovu. Kwa kijuu juu hii inaonekana kuwa kweli kwa sababu ya jinsi waongofu walivyoandikwa katika matendo, huku pia wakitaka mambo ya ‘upendo’ na ‘uvumilivu’ vyote vikiwa ni roho ya kipindi chetu. Somo hili linatoa uchanganuzi mmoja-mmoja zaidi umuhimu wa mafunzo.

NI UPESI SANA KWA NINI?

Hapawezi kuwapo shaka ya kwamba usomaji upesi wa Matendo ya Mitume kunatoa wazo la kuwa ubatizo mwingi ulitumia mafundisho kidogo yenye thamani katika misingi ya Injili, na pamoja na kuungama kifupi tu kuwa Kristo ni mwana wa Mungu. Kwa kusema maneno matatu: ‘Mimi namwamini Kristo’ ni wazi sio namna yenye maana kwa wokovu- na idadi kubwa ya madhehebu ya ‘Wainjilisti’ watakubali ya kwamba pawepo maarifa mengine baadhi au ufahamu moyoni mwa mtu awaambiaye maneno hayo kuwa ni yenye maana.

Hii maana haiwi ngumu kuiweka. Ni shida basi, kupinga ya kwamba maneno yanayotoa taarifa ya maungano ya kuamini Kristo kuwa ni mwana wa Mungu yanathibitisha msemo huu wa maneno kwamba ndiyo yanayohitajika kabisa. Karibu ni maana ya kawaida kuwa kusema tu kwa kifupi hiyo sentensi, bila kujali mawazo ya mtu mwingine na imani, hakuwezi kumweka kwenye njia ya wokovu. Vipengele vifuatavyo vitaweza kusaidia katika kueleza huku kuongoka kunakoonekana upesi:

  • Taarifa iliyo katika Matendo ya Mitume - kama katika maandiko mengi - ni kwa lazima habari imefupishwa sana. Inafanya mazoezi ya kuvutia kusoma kwa sauti baaadhi ya hotuba zilizoandikwa katika Matendo na kujua muda inayochukua kufanya hivyo; ni hakika kidogo zingechukua muda mfupi kwa kweli, ukijumuisha nyingi ambazo hazijaandikwa. Mifano kadhaa:

Utetezi wa Paulo katika mji wa Yerusalemu umechukua dakika nne kusoma (Mdo 22); hata mbele ya Feliki dakika moja; mbele ya Agripa dakika nne; Akiwahubiri watu Petro siku ya Pentekoste alichukua dakika nne tu; hata kwa Kornelio dakika tatu; Hotuba ya Bwana baada ya kulisha watu 5,000 (Yn. 6) dakika 6, mahubiri mlimani dakika 18. Petro alihubiri katika Matendo 3:12-26 alichukua karibu dakika mbili kusoma kwa sauti; lakini kwa kweli ulikuwa ni muda wa kutosha kwa habari iliyomo katika mahubiri yake kupelekwa hadi kwa "makuhani, na akida wa Hekalu na Masudukayo" na wao kuwatokea (Mdo 4:2).

Hivyo ukweli wa kwamba ‘mafunzo’, yaliongelewa kwa kirefu zaidi kwa atakaye kubatizwa muda haujaelezwa na si kwamba ushahidi hautatokea. Mjadala kuwa kimya si wa hakika sana kwa suala hili.

  • Kuwa na "kipawa cha maarifa (kufanya miujiza)…. Kuchunguza roho (mioyo)" kuliwawezesha wahubiri wa kwanza kuisoma mioyo ya watu kwa usahihi ya wale waliowahubiri, basi kufanya maulizo- mahojiano ya mafundisho, kama tunavyohitaji, si lazima.

  • Ipo sababu ya kuamini kuwa ubatizo wa watu wengi ambao ni Wayahudi wa Yerusalemu mwanzoni mwa Ukristo lilikuwa ni suala mahususi. Hakuna ushahidi ya kwamba utaratibu huu ni uwingi wa ubatizo uliofanywa baadae katika karne ya kwanza. Ikiwa waongofu wangeendelea kwa kiwango kile, basi Yerusalemu yote ingejawa na Ukristo ndani ya miaka michache. Watu hawa wakiwa ni Wayahudi kulikuwa na maana ya kwamba walikuwa na elimu nzuri ya Agano la kale na njia ya Mungu. Kina cha waraka wa Paulo kwa Waebrania na Petro (kwa Wayahudi vilevile) unaonyesha kwamba wasomaji wake walikuwa na uwezo wa kufahamu misemo iliyosemwa mingi katika Agano la Kale. Inashangaza kwamba Paulo anaelezea anachosema kuhusu Melkizedeki kuwa ni maziwa ya neno, kwa sababu yao kutokukua kiroho (Ebra 5:11,12). Hali hiyo akiwaagiza kwa kutokukua sana tangu wakati ule. Inaonekana kwamba nyaraka hizo kimsingi ziliandikwa kwa ajili ya Iklezia lililokuwepo Yerusalemu, wengi wao walikuwa wamebatizwa siku za kwanza zilizoandikwa mwanzoni mwa Matendo ya Mitume.

  • Tunatumaini kuonyesha ya kwamba kuhubiri jina la Kristo na kuungama ambako kumeelezewa katika Matendo ilikuwa sawa na kuelewa kabisa mafunzo yote yaliyonenwa.

  • Ilionekana toka 1 Kor 1:17 ya kwamba Paulo (na mitume wengine?) alishughulika katika kazi za siku zote pamoja na ya maana inayofuata ya waalimu na wanaobatizwa, hivyo basi alitumia kadiri ya muda mfupi tu kwa kila mahali alipohubiri.

JINA LA YESU

Jina la Mungu lina mafunzo mengi kumhusu Yeye na njia zake- Majina ya Mungu na vyeo vinaeleza tabia yake na nia. Jina la Yesu Kristo pia si utaratibu tu wa kupeana majina bali maneno yenyewe ni yenye mafunzo ya kina. Kuamini jina la Yesu kumelinganishwa na kubatizwa (Yn. 3:5,18,23). Gal 3:26,27 yafanya imani kwa Kristo kutoepukika imeungwa na ubatizo katika yeye: "Ninyi nyote ni wana wa Mungu kwa imani iliyo kwa Kristo Yesu. MAANA ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Mifano zaidi ya huku kuungwa kati ya kusadiki na kubatizwa kunapatikana katika Matendo 19:4; 10:42 linganisha na 48; 2:37,38; Lk 24:47. Apolo "aliujua" ubatizo wa Yohana (Mdo 18:25) ikionyesha kwamba ubatizo sio tu ni tendo, bali kunahusisha kujua mafundisho hakika.

" Filipo….. akawahubiri Injili" (Mdo 8:5) yaonekana kana kwamba alisema tu ‘Mumwamini Yesu’; lakini "Kristo" amefafanuliwa katika Matendo 8:12: " Lakini walipomwamini Filipo, akihubiri habari njema (Injili) za ya Ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa wanaume na wanawake. Elewa kwamba "mambo" yapo katika uwingi; si taarifa fupi tu kuhusu Kristo; na ‘kuwahubiri Kristo’ vile vile kulikuwa ndani yake mafunzo ya ubatizo. Yohana 6:40 unatuambia ya kwamba ni mapenzi ya Mungu "ya kwamba kila amtazamaye (amfaamuye) Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele", ambapo baadaye Yesu anasema kuwa "Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake (Mungu), atajua habari ya yale mafunzo" (Yohana 7:17). Basi kujua mafunzo ni sawa na ‘kumtazama’ Mwana. Maneno ya Kristo "Umelitunza neno langu, wala hakulikana jina langu" (Ufunuo 3:8) vile vile laonyesha ya kwamba neno la Kristo ni sawasawa na jina lake. Kristo akivuviwa ananukuu Isaya 42:4, "Visiwa vitaingojea sheria yake (Kristo)" kama "katika jina lake Mataifa watalitumainia"(Math. 12:21), tena jina lake linalingana na Injili kumhusu yeye. Waraka wa pili na wa tatu wa Yohana una ushahidi wa wahubiri wakisafiri "Walioshuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kama ipasavyo kwa Mungu, kwa ajili ya jina hilo, walitoka" (3 Yoh 6,7). Hii yaonesha kutaja siku za nyuma kazi waliyopewa kwa Marko 16:15,16, kwenda ulimwenguni kote na kuhubiri Injili, hivyo jina la Kristo na Injili yake vinalingana. "Kumwamini Kristo" kibiblia jambo la kubatizwa limejumuishwa: "Ninyi nyote ni watoto wa Mungu katika imani iliyo kwa Kristo Yesu. Maana (yaani, kwa sababu) nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo"(Gal. 3:26,27). Paulo anasema kana kwamba wao kumwamini Kristo kwa kawaida yalikuwepo maelezo yao ya hiyo imni ya ubatizo. Basi kumwamini Kristo ni mambo yanayoendelea kufuatana na utii, si kwa maneno tu ya haraka kuungama ‘Ninamwamini Kristo’. Hili limesemwa kutoka kwa Yohana 6:35: "Yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aaminiye na kubatizwa hataona kiu kamwe" ambalo ni sawa na kumwamini Kristo na KUJA kwake - laonyesha kwamba imani ni jambo la maendeleo.

Kuhubiri "Kristo" kwa hiyo yalikuwamo mfululizo wa mafundisho. Vivyo Luka 9:11 unamtaja Kristo akihubiri ufalme wa Mungu (ulinganishe Mthayo 4:23), wakati habari iliyo sambamba katika Marko 6:34 inamtaja akiwafundisha "mambo mengi". Injili ina "mambo mengi" - sio taarifa fupi tu kuhusu Kristo ambayo inaweza kusemwa kwa dakika. Hivyo tunasoma mafungu ya maneno kama, "Hata walipokwisha kuhubiri Injili katika mji ule, na kufundisha mambo mengi…." (Mdo 14:21 A.V), ni sawa sawa kuhubiri na kufundisha. Kusema hivi kungekua si muhimu kama Injili ilikuwa na taarifa moja pekee rahisi. Kuhubiri Paulo kule Beroya kulisababisha watu wakachunguza Maandiko kila siku (kwa nakala za Agano la Kale katika Sinagogi?) ili waone kwamba mambo hayo alioyafundisha Paulo msingi wake ulikuwa katika Agano la kale lote. Na ilikuwa kwa sababu ya watu maendeleo ya kuisoma Biblia baada ya kumsikia hata wakaamini - "Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini" (Mdo 17:12). Tunaposhughulika na watu walio na maarifa kidogo ya Biblila ya wasio chunguza mara kwa mara Biblia mara baada ya majadiliano, si ajabu ya kwamba wakati mafunzo unachukua muda mrefu kuliko katika Karne ya kwanza. "Kila mtu aaminiye kwamba Yesu amezaliwa na Mungu" (1Yoh 5:1) ni wazi aya hii inafanana na mistari kama "Kwa kupenda kwake alituzaa sisi kwa neno la kweli" (Yakobo 1:18)."Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili … kwa neno la Mungu….. neno hilo ni neno lile jema lilohubiriwa kwenu" (1 Petro 1:23,25). Hii yaonyesha ya kwamba kuamini kuwa Kristo ni mwana wa Mungu ni maelezo mafupi yenye ukweli wa kwamba mtu ameielewe Injili ambayo ndani ina neno la Mungu.

MFALME WA UFALME

Mkazo wa "kumwamini Kristo" unakuwa na maana zaidi mara ukifahamika ya kwamba cheo ‘Kristo’ kinaweza kusomwa kwa maana ile ile katika lugha moja ya maneno mengine ya Ufalme wa Kristo. Hivyo Bwana wetu aliwambia Mafarisayo ya kwamba hawakuwa na haja ya kwenda kuzunguka wakitarajia kuja kwa Masihi, kwa kuwa alikuwa tayari amesimama miongoni mwao. Ameeleza hivi kwa maneno "…Ufalme wa Mungu huko kati yenu(B.H.N)" (Lk. 17:21), waonyesha kwamba "Ufalme" utalingana na Mfalme wa Ufalme. Mahubiri ya Yohana ya kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia basi alikuwa anatoa habari ya kudhihirika kwa Kristo. Jiwe linaloponda sanamu ya ndoto ya Nebukadneza lasimama badala ya Ufalme wa Mungu (Dan 2:44); ni jiwe/Ufalme " utakaovunja falme zote hizi vipande vipande na kuziharibu", habari yaaonyesha kwamba jiwe ni Ufalme utakaovunja sanamu, vile vile’ baada ya kuziharibu. Katika uzi wa mfano mmoja wa Ezekieli na mzabibu kimeelezewa "kitawi chororo" vijiti vyake vimekatwa na kupandikizwa, hata ukawa ni mti mkubwa, " na chini yake watakaa ndege wa kila namna ya mbawa" (Ezekiel 17:22,23). Unapaswa huu mfano kuwa unamtaja Kristo, "mche mwororo" wa Isaya 53:2; hata hivyo upo muungano dhahiri wa mfano wake wa mbegu ya haradali, ambapo Ufalme wa Mungu umelinganishwa na punje ndogo ya mbegu ikakuwa hata ikawa mti mkubwa, chini yake ndege wa aina mbalimbali wakaweka viota vyao. Muungano huu kati ya neno la Ufalme na Yesu mwenyewe nafsi yake inaonyesha kwamba alijiona mwenyewe kuwa ni neno lililohai la Ufalme. Kwa mwanga huu unaelekea kwamba ‘kumwamini Kristo na kuiamini Injili yote ya Ufalme wa Mungu vyote ni mamoja.

INJILI NI NINI?

Sasa tunajadili kwa maelezo zaidi yale yaliyodhaniwa kuwa ni maunzo ya muhimu miongoni mwa waaminio katika karne ya kwanza. . . Inabidi itambulike ya kwamba palikuwepo muundo mkuu katika Nyakati za Agano Jipya ambao kwa karibu sana ulikuwa sawa na "Habari ya Imani" yetu. Kigawanyo kingine muhimu kumbuka walikuwepo ndugu wenye kipawa cha unabii -‘utabiri ulionyooka wa ufunuo toka kwa Mungu chini ya kuvuviwa. Ipo sababu ya kuamini kuwa pamoja na muda mwingine wa kunena usemi ulipovuviwa uliongezeka kwenye muundo mkuu wa mafundisho.

MUUNDO MKUU WA MAFUNZO

Paulo aliweza kusema ya kuwa kwenye iklezia la Ruma karibu "walitii kwa mioyo yao ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake" (Rum 6:17) kabla ya kubatizwa kwao. Kwa kiyunani "namna" imetafsriwa "Mfano" na "Mfano mzuri " - kana kwamba ilitaja mafundisho ambayo yaliigwa kila mahali. Ushuhuda wa Paulo kwa huu unaonyesha umuhimu wa muundo mkuu ulioainishwa na mafunzo yanayopaswa kueleweka kabla ya ubatizo, na vile vile hazikuwa ni habari chache fupi ambazo zilitajwa kabla ya ubatizo. Wengine ndani ya Iklezi walikuwa na "mfano wa utauwa, huku wakikana nguvu zake" (2Tim 3:5), labda imedokezwa ya kwmba walishika mafunzo ya msingi wa imani lakini bila ya kutambua nguvu halisi ya KWELI katika maisha yao ya kila siku. Paulo aliweza kuwakumbuka Wagalatia ya kwamba "Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulubiwa" (Gal 3:1). Kwa Kiyunani "kuwekwa" maana yake halisi "iliandikwa picha kwa maneno yaliyoandikwa, kana kwamba maagizo ya kwanza yalikuwa kwa njia nyingine - mfano ulioandikwa wa maagizo ya mafundisho.

Akifafanua mafunzo ya ufufuo, Paulo aliweza kusema "Naliwatolea ninyi…. yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa….." (1Kor 15:3), yaonyesha jinsi gani alipokea ufunuo kuhusu mambo haya, naye akawatolea wao kama mafunzo yanayowapasa kukubalika kuwa ya muhimu. 2 Petro 2:21,22 kwa uzuri unaangukia hapa: "Ingelikuwa heri kwao kama wasingalijua njia ya haki: ….. kuiacha ile amri takatifu waliyopewa. Lakini…… aliyeoshwa (kwa ubatizo) amerudi kugaa-gaa matopeni".

Hapa "njia" na "amri takatifu" ambavyo "aliwatolea" kwao vyote viwili vimeungwa na kuoshwa kwa ubatizo; basi "amri" katika umoja yaweza kudokeza ya kwamba ulikuwepo muundo mkuu wa mafunzo ulioainishwa wazi wazi kabisa ambao ilibidi ufahamike kabla ya kubatizwa. Yapo mafungu kadhaa ya maneno yasemayo ‘kupokea’ mafunzo yahusuyo Elimu na "Injili": Gal 1:9,12; Flp 4:9; Kol2:6; 1The 1:6; 2:13;4:1. Hii inathibitisha ya kwamba ‘Injili’ ilikuwa na muundo wa namna yake maalum wa mafundisho ambayo ‘yalipokelewa’ ya kwanza na mitume na kisha kwa wale ambao walihubiriwa.

"IMANI"

Yuda nae anazungumzia "imani waliyokabidhiwa watakatifu (wote) mara moja tu" (Yuda 3). Kwa hivi "imani" ni sawa sawa na "ile imani ya elimu" iliyokabidhiwa kwao kabla ya kubatizwa, yalikuwa ni maneno mengine katika msamiati wa karne ya kwanza uliotaja muundo mkuu wa mafundisho. Onyo la Paulo "kushika sana ungamo la tumaini (imani) yetu" (Ebra 10:23) laweza kuwa linataja nyuma ungamo lao mbele ya watu imani katika "tumaini" kabla ya ubatizo wao. Kulishika lile "neno la imani" (Tito 1:9) mara ya kwanza inatajwa kuitengeneza hii ‘habari ya imani’ ambayo awali ilifundishwa. "Imani tuishirikiyo" (Tito 1:4) yaonyesha jinsi gani huu muundo wa mafundisho walishirikiana wote waaminio; ili kuwepo "imani moja" tu (Efe 4:5). "Imani" na jina la Kristo ni jina lingine kwa fundisho lile lile lililomo ndani ya "Imani". Kwa mambo yote mawili ya mazoea (1Tim 6:10) na mafundisho (1Tim 4:1) Paulo alitahadharisha ya kwamba wengine"watajijenga na Imani". Hatua ya kwanza katika huko kukengeuka ilikuwa ni kusema ya kuwa "imani" haikuwezekana kuiainisha.

MAMBO YA MAZOEA

Mambo ya desturi vilevile yalikuwa sehemu ya muundo huu wa mafundisho. "Kumwamini Kristo" kulijumlisha hoja ya kuhusu "haki, kuwa na kiasi na hukumu itakayokuja" (Mdo 24:24,25). Paulo anazungumzia maagizo yanayohusu kumega mkate kama anavyofanya mafunzo juu ya ufufuo. "mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi" (1Kor 11:23). Hapo yaonekana lilikuwepo kundi lenye desturi ya mambo haya, ambayo baadaye Paulo aliyapanua kwa kuongeza mafunzo juu ya nafasi ya wa dada katika Iklezia: "Nanyi mmeshika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea. Lakini nataka mjue ya kuwa…… kichwa cha mwanamke ni mwanamume…."(1Kor 11:2,3). Haya yanaonekana kuwa maelezo ya mambo yawe kabla ya kubatizwa, nayo yalikuwa sehemu ya muundo mkuu uliosisitizwa kwenye karne ya kwanza. Kwa Kiyunani "amri" pia ni neno lililotafsiriwa "mapokeo" katika 2 Thes 3:16 na 2:15: "Jitengeni ….. na kila ndugu aendaye….. si kwa kufuata mapokeo mliyopokea kwetu…… simameni imara, mkayashike mapokeo mliofundishwa, ama kwa (kuvuviwa, Unabii) wa maneno, au kwa waraka wetu".

Haya yaonyesha umuhimu mkubwa wa kushika muundo huu mkuu wa mafunzo, na haja ya kujitenga toka kwa hao wasio wa utii: "Kwa kushika lile neno la imani (namna nyingine ya maelezo ya u huu mkusanyiko wa muundo wa mafundisho) vile vile kama alivyofundishwa, apate kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga" (Tito 1:9).

Tunajua walikuwepo "manabii wa uongo"katika Iklezia ya kwanza, wakidai kuwa na mafunuo toka kwa Mungu juu ya mafundisho ambayo yaliongezwa ili muundo wa mafunzo ukubalike. Basi Paulo anakazia "neno la kuaminiwa" la ufunuo wa elimu iliovuviwa (Tito 1:9; 3:8; 2Tim 2:11; 1Tim 4:9), ambalo "linastahili kukubalika" (1Tim 1:15; 4:9) - yaani, katika muundo mkuu wa mafundisho yanayofanya "imani". Hii ndiyo sababu Yohana alitoa tahadhari "….msiiamini kila roho" inayodai imevuviwa (1 Yohana 4:1).

HABARI YA MAMBO MOJA MOJA DHAHIRI

Ifuatavyo ni baadhi tu ya mifano iliyowazi mahali mafunzo mengine kuliko "kumwamini Kristo" tu ilifundishwa kama sehemu ya msingi wa injili ambayo ilieleweka kabla ya kubatizwa.

-"Mungu atazihukumu siri za wanadamu, sawa sawa na Injili yangu" (yaani, ile moja aliyoihubiri Paulo; Rum 2:16). Mafunzo ya kiti cha hukumu na kuhusika kwa sababu hiyo yamepimwa kuwa ni ‘jambo la kwanza’ tazama pia Matendo ya Mitume 24:25, Ebra. 6:1,2.

-Wazo la tohara kwamba lilikuwa la muhimu kwa wokovu lilielezwa na Paulo kuwa ni "Injili nyingine" (Gal 1:6) Hivyo kujua ya kwamba tusishike torati ya Musa, k.m Sabato, ni sehemu ya kuwa sasa tunafahamu Injili.

-"Injili ya Ufalme" sio tu ni kuhusu Kristo bali pia ni juu ya Ufalme wake unaokuja; Isaya 52:7 (linganisha na Rum 10:15) anasema mhubiri wa Injili anayetaja kipindi hapo itakapoweza kusemwa Sayuni "Mfalme wako anatawala "- yaani katika Ufalme.

-Kuelewa vema ‘maana nzuri’ jinsi Kristo alivyokuwa lilikuwa ni jambo la ushirika (2Yn. 7-10); kwa sababu hii Injili ilihusu "mambo" ya uwingi, juu ya Kristo (Mdo 8:12). Tena, kusema tu ninamuamini Kristo haitoshi.

-Umuhimu wa ahadi kuhusu Ufalme ni sehemu kuu ya Injili; ilikuwa na kwa ahadi hata Injili ilihubiriwa kwa Abrahamu (Gal 3:8) na Israeli (Ebra 4:2). Hivyo Paulo alinena katika kuhubiri kwake juu ya ahadi zilizofanywa kwa Daudi kuwa ni "neno la wokovu" (Mdo 13:23,26). Kwa hiyo zilikuwa ni sehemu muhimu ya ujumbe wa wokovu. Hivyo anasema "Na sisi tunawahubiri habari njema ya ahadi ile waliyopewa mababa" (Mdo 13:32). Vivyo hivyo Rum 1:1-4: " Injili ya Mungu yaani, habari za mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili ….. Yesu Kristo".

-Ili kuelewa ahadi unatakiwa kufahamu hakika historia ya Israeli. Somo la mahubiri ya Paulo pale Antiokia katika Matendo 13 linamwonyesha akieleza habari ya historia ya Israeli na mkazo maalum juu ya ahadi akasisitiza jinsi gani zilitimilika kwa Yesu. Hivyo mahubiri yake msingi ulikuwa juu ya historia ya Israeli, nayo ilikuwa tunayoweza kuiita ‘uwazi’ akimaliza kwa kuonya matokeo ya hukumu kwa kutoitika neno alilokuwa anahubiri (Mdo 13:40,41). Katika mahubiri yetu yawe namna hii.

MWISHO

Ukubwa wa yote haya hauwezi kukaziwa zaidi. Ila "Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako; Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusiao pia" (1Tim 4:13-16). Orodha ya mafundisho makubwa kama haya yaliyotolewa mwishoni mwa kitabu sehemu ya 1 ya kitabu hiki kwa udhahiri hayakuvuviwa, bali katika wazo la mwandishi unaonekana ni muhustasari mzuri wa mambo mengi ya namna yake maalum yaliyotajwa kwenye mafungu ya maneno ya Biblia yanayozungumzia mambo ambayo ni ya sehemu ya "imani", "mapokeo" n.k . Kwa matumaini somo hili limeonyesha kwamba ipo haja halisi ya kuwa na muundo mkuu wa mafundisho ambayo sote tunaukubali na kutokuwa wavivu kuthibitisha utii wetu utupasao kwake. Yaliyomo katika muundo huu mkuu wa mafundisho yawe ni maagizo yetu kwa watakao ubatizo., tena ni vizuri kwao kuchunguza kwa kujadiliana kabla ya kutumbukizwa kwao ili wafahamu kabisa mambo waliyofundishwa. Mara nyingi waaminio walitiwa moyo waambatane na "Imani" katika wakati wa shida. "Msingi wa Mungu ulio imara umesimama". Mazoea yetu kwa mambo makuu ya kwanza, na njia ya ajabu ya kusudi la Mungu kushikamana pamoja, ndani yake yenyewe yatutie moyo. Kwa kuhubiri kwetu kabisa kila mara au kujifunza tena na tena mambo haya hii itakuwa faida na maana ya kina ya matumaini yetu, hivyo kama Paulo katika saa yake ya giza na upweke tunaweza kusema "….. mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda…. Maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake (maisha yetu, utu wetu wote) hata siku ile" (2 Tim 4:7; 1:12).

MAELEZO YALIYO CHINI YA UKURASA: KUMKIRI BWANA YESU

"Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kumuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka" (Rum 10:9).

Vipengele vifuatavyo vinahitaji kufanywa:

-Tumeonyesha kwamba ‘Bwana Yesu’ ni neno lililoelekea kuwa na maana ile ile na jingine katika Lugha moja ya Muundo mzima wa mafunzo makuu yaliyo na "mambo yanayohusu Ufalme wa Mungu na jina lake Yesu Kristo", pamoja na ubatizo (Mdo 8:5 linganisha mst. wa 12). ‘Kukiri’ anakosema Paulo vema kunaweza kuwa kwenye ubatizo. Kwa suala hili alikuwa anataja kwa kusema Marko 16:16 "Aaaminiye (linganisha, kukiri kwa kinywa) na kubatizwa (linganisha, kufufuka na Kristo toka kwa wafu) ataokoka".

-Kuelewa ufufuo wa Kristo kunahusisha kufahamu fundisho la Biblia jinsi mwanadamu alivyo.

-Rum. 10:8,9 yaonekana kuwa sawa na mst wa 13: "Kwa kuwa, kila atakaye liitia

(yeye mwenyewe, kwa Kiyunani) Jina la Bwana ataokoka." Paulo anasemwa kama amebatizwa na hivyo akiliitia mwenyewe jina la Bwana (Mdo 22:16); Ubatizo tu unatupatia kuingia katika jina la Bwana (Math 28:19).

-Umuhimu wa kubatizwa ukishatiliwa mkazo katika sura chache awali Warumi 6, haiwezekani kwamba Paulo angefundisha sasa ya kuwa haukuwa na ulazima kwa ajili ya wokovu katika sura ya 10.

-Rum 10:9 umetanguliwa na mst 6-8: "Usiseme moyoni kwako, Ni nani atayepanda kwenda mbinguni ….. Ni nani atayeshuka kwenda kuzimu? …lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako na katika moyo wako: yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo". Neno (lile) la imani" basi lilikuwa lenye kuwapasa kulikiri, sawa sawa na "Bwana Yesu" katika mst wa 9. Tumeona ya kwamba "Imani" inatoa maelezo ya muundo mzima wa mafundisho yaliyo na Injili. Paulo ananukuu toka Kum. 30:11-14: "Maagizo haya nikuagizayo leo, …. si mbinguni wala si ng’mbo ya pili ya bahari (kilindini)…. lakini neno li karibu nawe sana". Anaonekana akitafsiri "neno" …. "maagizo haya" kama kumtaja Kristo. Kwa njia iyo hiyo ikiwa kama Israeli wangelitunza neno wangelibarikiwa (Kum 30:16), hivyo kama Israel wapya waliamini neno kuhusu Kristo wangaliokolewa. Basi kumkiri Kristo kwa kinywa kunalingana na kukubali fundisho juu ya Kristo. "ukiwa utaifuata sauti ya BWANA" (Kum 30:10) ni sawa na Rum 10:9: "Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako". Huku kuwa sawa sawa tena inaonyesha kwamba "Bwana Yesu" ni jina lenye maelezo mafupi yenye fundisho la msingi wa neno la Mungu.


  Back
Home
Next