Misingi Ya BIBLIA
Somo La 10: Kubatizwa Katika Jina La Yesu
Maana Muhimu Sana Ya Ubatizo | Tubatizwe Jinsi Gani? | Maana Ya Ubatizo. | Ubatizo Na Wokovu | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Kubatizwa tena, Kiwango cha elimu itakiwayo kabla ya kubatizwa, Mnyang'anyi Msalabani, Mfano wa huduma ya Ubatizo) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 30: Kubatizwa tena

Watu wengi wanahisi kutofanya lolote kabisa kubatizwa baada ya kuwa tayari walifanya kile kinachodhaniwa kuwa ulikuwa ni "ubatizo" wa namna fulani aidha kwa kunyunyuziwa maji akiwa mtoto mchanga, au kuzamishwa kwenye maji mengi katika kanisa lingine. Ingawa hivyo, kabla ya ubatizo inabidi pawepo toba na imani sahihi ya Injili ya kweli (Mdo 2:38; Marko 16:15,16). Ubatizo basi ni ubatizo kwa sababu ya mambo haya yakiwa katika mpango kabla ya kuzamishwa kwenye maji. Mathayo 28:19,20 unaunganisha ubatizo na kusikia kwanza mafunzo ya Kristo aliyoeleza.

Mtoto mdogo hawezi kutubu au kufahamu Injili; kwa vyovyote, kunyunyuziwa si ubatizo. Mpiga mbizi akiogelea katika bwawa aweza kuzama katika maji lakini huo si ubatizo, kwa kuwa mtu hajui kuitikia Injili ya kweli. Vivyo hivyo ni kweli kwa hao wanaobatizwa katika maji mengi wakati wakiamini mafundisho potofu; wamezamishwa katika maji lakini hawajabatizwa.

Ila kuna "imani moja", yaani orodha ya mafundisho yanayofanya kuwa Injili ya Kweli, na kwa sababu hii tu "ubatizo mmoja" - ubatizo unaotokea baada ya kusadiki "imani moja". Kuna mwili mmoja (yaani kanisa moja la kweli)…… kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. "Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja"(Efe 4:4-6). Hakuna matumaini mawili, kama ilivyoaminika na hao wasemao kwama hayo ni mamoja ikiwa twaamini thawabu yetu itakuwa mbinguni au duniani. Yupo "Mungu" mmoja tu -basi Yesu si Mungu. Kwa sababu hiyo kama, wakati tulipobatizwa, tulishidwa kufahamu mafundisho ya msingi kama Ufalme wa Mungu, sifa na tabia ya Mungu na Yesu, n.k basi ‘ubatizo’ wetu wa kwanza haukuwa wa msingi.

Yohana mbatizaji aliwazamisha katika maji watu, akiwataka watubu na kuwafunza mambo hakika ya kuhusu Yesu (Marko 1:4; Luka 1:77). Lakini, huu haukutosha. Matendo 19:1-5 taarifa imetolewa kuwa wengine ambao Yohana aliwabatiza ikawabidi wabatizwe tena kwa kuwa hawakukamilika kushika mafunzo ya hakika. Kama wale ambao Yohana alibatiza, tunaweza kuona ya kwambva kwenye kuzamishwa kwetu kwa kuanza tulifanya toba halisi na kuanza upya. Huu waweza kuwa kweli lakini hauondoi haja ya kupokea "ubatizo mmoja (wa kweli) unaoweza kutokea tu baada ya kushika mambo ya "imani moja".


  Back
Home
Next