Misingi Ya BIBLIA
Study 9: Ushindi Wa Yesu
Ushindi Wa Yesu | Damu Ya Yesu | Kutoa Dhabihu Kwa Ajili Yetu Na Kwa Ajili YaNafsi Yake Mwenyewe | Yesu Ni Mwakilishi Wetu. | Yesu Na Torati Ya Musa | Sabato | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Sanamu ndogo ya Yesu Msalabani, Je? Yesu alizaliwa December 25?) | Maswali

9.6 Sabato

Moja ya mifululizo iliyoenea zaidi katika ‘Ukristo’ wa leo kwa matendo yao na Torati ya Musa yameonekana katika wazo la kwamba yatupasa kuishika sabato. Makundi mengine yanadai kwamba tuishike sabato ya Wayahudi hasa kama ilvyoainishwa katika sheria; wengi wengine wanaona kwamba Wakristo wawe na siku moja ya juma iwe siku ya kuabudu, ambayo mara nyingi wanaiainisha kama Jumapili. Kwa kudhihirisha jambo la kwanza ni kuwa Sabato ilikuwa siku ya mwisho ya juma, Mungu alipumzika baada ya siku sita za uumbaji (Kut 20:10,11). Jumapili ikiwa ni siku ya kwanza ya juma, haiwi sahihi kuitunza siku hii kuwa ni sabato. Kwa namna sahihi Sabato ilikuwa ni "ishara kati yangu mimi (Mungu) na Israel wapate kujua ya kwamba mimi, BWANA, ndimi niwatakasae"{Ezek 20:12). Kama hivi, kamwe haikusudiwi kuwafunga watu wa mataifa (wasio Wayahudi).

Tumeona ya kwamba kwa kufa kwake Yesu Kristo Msalabani, Torati ya Musa iliondolewa, kwa hiyo sasa haupo ulazima wa kuitunzu Sabato, au kweli, sikukuu yoyote kama siku ya kifo cha Kristo (Kolos 2:14-17). Wakristo wa kwanza waliorudia kuishika sehemu ya Torati ya Musa kama Sabato wamesemwa na Paulo ni kurudia "mafundisho manyonge, yenye upungufu ambayo mnataka tena kuyatumikia. Mnashika siku (kama Sabato), na miezi, nyakati na miaka (yaani sikuu za wayahudi). Nawachelea (nina wasiwasi), isiwe nimejitaabisha bure kwa ajili yenu" (Gal 4:9-11). Ni jambo la kufikiri kujaribu kuishika Sabato kuwa ni njia ya Wokovu. "Mtu afanya tofauti kati ya siku na siku (katika umuhimu wa kiroho) mwingine aona siku zote kuwa ni sawa sawa. Kila mtu athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishae siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu"…. (Warumi 14:5,6).

Kwa sababu hii, inaeleweka ya kuwa hatusomi taarifa ya kwanza ya Waamini wa kwanza wakiitunza Sabato. Hakika imeandikwa kwamba wao walikutana "siku ya kwanza ya juma", yaani, Jumapili; "Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokutana ili kumega mkate……" (Mdo 20:7). Kama haya yalikuwa ni mazoea yaliyoenea pote yameonyeshwa na Paulo akiwashauri Waamini wa Korintho wachukue michango "siku ya kwanza ya juma" (1Kor 16:2), yaani katika mikutano yao ya kawaida kwa siku hiyo. Wote wanaoamini wamesema kuwa ni Makuhani (1Petro 2:9)- waliosamehewa kuishika Sabato (Math 12:5).

Kama tunatunza Sabato, yatupasa kufanya hivyo kwa uzuri; awali tumeoneswa ni jambo la kufisha kushika Torati ya Musa nusu-nusu, kwa kuwa hii itasababisha tokeo la hukumu yetu(Gal 3:10; Yakobo 2:!0). Wokovu ni wakutunza sheria ya Kristo kuliko ya Musa. Israel hawakuruhusiwa kutenda kazi yeyote ya utumishi siku ya sabato: "Mtu awaye yote atakaye fanya kazi yoyote siku hiyo atauawa". Vilevile waliamriwa: " Hamtawasha moto katika nyumba zenu kwa siku ya Sabato", na kwa sababu hiyo walikatazwa kuadaa chakula siku hiyo (Kut 35:2,3: 16:23). Mtu aliyekusanya kuni kwenye sabato, labda ili kuwasha moto, adhabu yake ilikuwa kifo kwa kufanya hivyo (Hesabu 15:32-36).

Hayo madhehebu yanayofundisha kwamba kuitunza Sabato kunahitajika kwa washirika wao basi hao washirika wanapoivunja waadhibiwe kifo. Usiwepo upishi wa chakula au matumizi ya moto kwa namna yoyote- kama kuendesha magari, kutumia mfumo wa kuchoma au kupasha joto n.k. Wayahudi wenye msimamo mkali wa siku hizi wameweka mfano wa aina ya mwenendo unaotakiwa na Sabato: wanabaki ndani ya Nyumba siku nzima isipokuwa kwa sababu ya dini, wao hawajihusishi na upishi, kusafiri n.k. Wengi wa ‘Wakristo’ hao wanaodai kuitunza Sabato wanashindwa mno kwenye jambo hili.

Imesisitizwa ya kwamba kuitunza Sabato ilikuwa moja ya amri kumi alizopewa Musa, na ya kuwa, Sheria iliyobaki ya Musa iliondolewa, ulazima umesalia wa kushika amri zote kumi. Seventh Day Adventists (S.D.A) wanatofautisha kati ya ‘sheria ya uadilifu’ ya amri kumi na iitwayo ‘Sheria ya mambo ya ibada kulingana na mwili’, ambayo wanaamini iliondolewa na Kristo. Huku kutofautisha hakujafundishwa na maandiko. Tangu awali tumeeleza kwa kuandika kwamba Agano la Kale linataja mambo ya Torati ya Musa, iliyobadilishwa msalabani na Agano Jipya. Inaonyesha kwamba amri kumi, ukijumlisha ile inayohusu Sabato, yote ilikuwa ni sehemu ya Agano la kale ambayo iliondolewa na Kristo:-

  • Mungu "akawahubiri ninyi (Israel) agano lake, aliwamuru (Israel) kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbao mbili za mawe" (Km 4:13).

  • Tena ilielekea ya kwamba agano hili, msingi wake ulikuwa juu ya amri kumi, lilifanywa kati ya Mungu na Israel, sio watu wa mataifa walikuwepo siku hiyo.

  • Musa alikwea Mlima Horebu kupokea mbao za mawe ambazo Mungu aliandika juu yake Amri kumi. Kuhusu hii Musa alifafanua baadae."BWANA, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu"(Km 5:2) yaani, kwa amri hizo kumi.

  • Kwa wakati huu Mungu "aliandaka maneno ya agano juu ya mbao, amri kumi (Kut 34:28). Agano lili hili lilikuwa na hiyo inayoitwa ‘ sheria ya ibada kulingana na mwili’ (Kut. 34:27). Kama tukitia mkazo kushika ibada kama ilivyofanywa katika amri kumi ni lazima, yatupasa vile vile kufuata kila kipengele cha sheria nzima, kwa kuwa yote haya ni sehemu ya agano moja. Kwa kuweka wazi ni vigumu kufanya hivi.

  • Ebra 9:4 yazungumzia ‘mbao za agano’. Amri kumi ziliandikwa juu ya mbao za mawe, ambazo zilikuwa za "agano la kale".

  • Paulo analitaja agano hili kuwa "liliandikwa na kuchorwa katika mawe", yaani, juu ya mbao za mawe. Analiita "huduma ya mauti….. huduma ya adhabu…….. iliyobatilika (iliyoondolewa)" 2 Kor 3:7-11. Agano lilokuwa pamoja na amri kumi ni dhahiri haliwezi kutoa tumaini lolote la wokovu.

  • Kristo aliifuta " hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu" (Kol. 2:14) msalabani. Hii inatajwa hati ya Mungu ya amri kumi juu ya mbao za mawe. Vivyo hivyo Paulo anaisema ‘torati’….katika hali ya zamani, ya andiko" (Rum. 7:6) hali inayodhihirisha kutaja maandiko ya amri kumi yalioandikwa juu ya mbao za mawe.

  • Ni moja tu ya amri kumi inayoitwa "amri" katika Rumi 7:8: "Amri…. ilisema, usitamani". Aya zinazotangulia katika Rum 7:1-7 zinasisitiza jinsi "torati" ilivyobatilishwa kwa kufa Kristo; kwa hiyo ‘torati’ ina amri kumi.

Yote haya yanaweka wazi ya kwamba Agano la kale na ‘torati’ ndani yake ilikuwa na amri kumi. Kama zilivyobatilishwa na Agano Jipya, kwa sababu hiyo amri kumi ziliondolewa. Ingawa hivyo, tisa kati ya amri kumi zimethibitishwa tena, iwayo yote katika roho, kwenye Agano Jipya. Kitabu cha hesabu 3,5,6,7,8,na 9 zaweza kupatikana kwa 1Tim.1 peke yake, na Hesabu 1,2 na 10 kwa 1 Kor. 5. Bali amri ya nne inayohusu Sabato kurudiwa katika Agano Jipya haijawa lazima kwetu kushika.

Orodha ya maneno ya hati zifuatazo zinakuza jinsi gani nyingine tisa zimethibitishwa tena Agano Jipya:-

Ya 1-Efe 4:6; 1 Yoh 5:21; Math 4:10

Ya 2- 1Kor 10:!4; Rum 1:25

Ya 2 -1 Kor 10:14; Rum 1:25

Ya3- Yak 5:12; Math 5 :34,35

Ya 5-Efe 6:1,2; Kol 3:20

Ya 6- 1 Yoh 3:15; Math 5:21

Ya 7- Ebra 13:4; Math 5:27,28

Ya 8- Rum 2:21; Efe 4:28

Ya 9- Kol 3:9; Efe 4:25; 2 Tim 3:3

Ya 10- Efe 5:3; Kol 3:5