Misingi Ya BIBLIA
Study 9: Ushindi Wa Yesu
Ushindi Wa Yesu | Damu Ya Yesu | Kutoa Dhabihu Kwa Ajili Yetu Na Kwa Ajili YaNafsi Yake Mwenyewe | Yesu Ni Mwakilishi Wetu. | Yesu Na Torati Ya Musa | Sabato | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Sanamu ndogo ya Yesu Msalabani, Je? Yesu alizaliwa December 25?) | Maswali

9.5 Yesu Na Torati Ya Musa

Yesu akiwa ni dhabihu timilifu kwa dhambi na Kuhani Mkuu asiye na kasoro yoyote ambaye kweli anaweza kutupati msamaha, utaratibu wa zamani wa kutoa dhabihu za wanyama na makuhani wakuu uliondolewa baada ya kifo chake (Ebra 10:5-14). "Maana ukuhani ule ukibadilika, (toka kwa walawi kwenda kwa Kristo), hapana budi sheria nayo ibadilike" (Ebra 7:12). Yeye hakufanywa Kuhani kwa sheria na maagizo ya kibinadamu (yaani kwa sababu ya mtu lazima atoke kwa kabla la Lawi ndipo awe kuhani), bali kwa nguvu ya uhai ambao hauna mwisho", ambao alipewa kwa sababu ya dhabihu yake timilifu (Ebra 7:16 B.H.N). basi ile amri ya zamani yaani torati ya Musa ilifutwa kwa sababu ilikuwa hafifu na isiyo kitu. Maana sheria ya Musa haikuweza kukamilisha jambo lolote. Lakini sasa mahali peke pamewekwa tumaini lilo bora zaidi (kwa njia ya Kristo) ambalo kwalo tunaweza kumkaribia Mungu. (Ebra 7"18.19 B.H.N).

Ni dhahiri kutokana na jambo hili ya kwamba sheria ya Musa ilifikia mwisho kwa dhabihu ya Kristo. Kuuamini ukuhani wa kibinadamu au kuendelea katoa dhabihu za wanyama maana yake hatukubali utimilifu wa ushindi wa Kristo. Kuwa na imani hizi ni kwamba sisi hatufahamu kuwa sadaka ya Kristo ni yenye ushindi uliokamilifu, na ya kuwa tunaona kufanya kazi hii ni ya lazima kutuletea kuhesabiwa haki, kuliko kumwamini Kristo pekee. "Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu mwenye (kuhesabiwa) haki ataishi kwa imani" (Gal 3:11 ml Hab 2:4).

Juhudi ya mapenzi yetu wenyewe kuwa imara kutii andiko la sheria ya Mungu haitatuletea kuhesabiwa haki; kwa kweli kila msomaji wa maneno haya tayari ameziasi sheria hizo.

Kama tunashika Torati ya Musa, yatupasa kujaribu kuyashika yote. Kutotii moja tu ya sehemu yake maana yake ni kwamba wote walio chini yake wamehukumiwa; "Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yalioandikwa katika kitabu cha torati;ayafanye" (Gal 3:10).

Kutokana na udhaifu wa mwili wetu wanadmu hatuwezi kutunza kwa ukamilifu torati ya Musa, lakini kwa kuwa Kristo alitii yote kabisa, tumeachwa huru toka sharti lolota la kuishika. Wokovu wetu ni kipawa cha Mungu kwa ajili ya Kristo, kuliko,matendo yote ya kutii. "Maana yake yasiowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu kwa kumtuma mwanae mwenyewe katika mfano wa mwili ulio na dhambi, na kwa sababu ya dhambi (Yaani, kutoa dhabihu ya dhambi. Kama unayo Biblia iitwayo Biblia Habari Njema aya hii inaeleweka vizuru zaidi), aliihukumu dhambi katika mwili" (Rum 8:3). Hivyo basi. Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu" (Gal 3:13).

Kwa hiyo hatutakiwi tena kutunza sehemu yoyote ya torati ya Musa. Tuliona katika somo la 3.4 kuwa Agano Jipya kwa Kristo liliingia mahali pa Agano la Kale la torati ya Musa (Ebra 8:13). Kwa kufa kwake Kristo aliifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake (kwa kutoweza sisi kushika vizuri torati)….. akaiondoa isiwepo tena, akaipigilia misumari msalabani……. Basi, mtu asiwahukumu nyinyi katika chakula au vinywaji (kutoa dhabihu), au kwa sababu ya sikukuu ya mwandamo wa mwezi; au sabato mambo haya ni kivuli cha mambo yajayo; Ukweli wenyewe ndiye Kristo" (Kolos 2:14-17 U.V na B.H.N). Hapa ni wazi kabisa - kwa sababu ya Kristo kufa msalabani, Torati "aliiondoa" ili kwamba tusishindane na mkazo wowote uliowekwa yetu kwa kushika sehemu yake k.m sikukuu za sabato. Kama shera yote, lengo la mambo haya lilikuwa laonyesha mbele kuja kwa Kristo ile mara ya kwanza. Baada ya kufa kwake maana ya mifano yake ilitimia, hapakuwa na haja zaidi kuendelea kuifuata.

Kanisa la awali la Kristo kwenye karne ya kwanza daima lilikuwa chini ya mkazo uliotoka kwa wayahudi wenye msimamo mkali kufuata sehemu ya sheria. Katika Agano hilo lipo onyo lililorudiwa la kuzuia haya mashauri. Usoni pa yote haya, ni ajabu ya kwamba yapo madhehebu baadhi yanayoshauri kutii sheria. Awali tumeonyeshwa ya kwamba jaribio lolote la kupata wokovu kutokana na kutii torati inabidi shabaha iwe kutunza Torati yote, upande mwingine sisi wenyewe tunakuwa tumehukumiwa kwa kuiasi hiyo Torati (Gal 3:10)

Kuna jambo ndani ya mwili wa mwanadamu linaloelekea kwenye wazo la kuhesabiwa haki kwa matendo; tunapenda kuona kwamba tunafanya jambo fulani la kuuelekea wokovu wetu. Kwa sababu hii, kutoa sehemu ya kumi (fungu la kumi) kwa lazima, kuvaa msalaba, kusemasema orodha ya sala, kusali kwa mkao fulani n.k. yote haya ni sehemu wafanyayo watu wengi wa dini, za Kikristo na wengineo.Wokovu kwa kumuamini Kristo peke yake ni mafundisho karibu ya kipekee kwa Ukiristo wa kweli msingi ukiwa ni Biblia.

Maonyo juu ya kushika sehemu iwayo yote ya Torati ya Musa ili kuupata wokovu, yametapakaa katika Agano Jipya. Wengine walifundisha ya kuwa wakristo watahiriwe kulingana na sheria za Musa, na "kuitunza Torati". Yakobo alilaumu wazo hili kwa niaba ya waamini wa kweli: "sisi hatukuwaagiza" (Mdo 15:24). Petro aliwasema wale waliofundisha ni lazima kutii Torati ya kuwa ni kuweka " kongwa juu ya shingo za wanafunzi ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua. Bali tunaamini kwamba tunaokoka kwa neema(ni kinyume na matendo yao ya kutii sheria) ya Bwana Yesu vile vile kama wao" (Mdo 15 10:11) Akivuviwa, Paulo akisema ilivyo sawa mambo yalivyo, anasisitiza jambo lilo hilo mara kwa mara: " Mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria bali kwa imani ya Kristo Yesu …. Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria……. Na kwa yeye (Kristo) kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiiyoweza kuhesabiwa haki toka kwa torati ya Musa" Gal 2:16; 3:11; Mdo 13:36).

Ni ishara ya hakika jinsi Ukristo wa wengi ulivyogeuka hata mengi ya mazoea yao yapo juu ya mambo ya Torati ya Musa - mbali ya mafunzo yaliyo wazi na kutendewa kazi yaliyopimwa hapo juu ya kuwa Wakristo wasiishike sheria, kwa kuwa katika Kristo imeondolewa. Sasa tutaona njia zilizowazi ambazo ndani yake Torati ya Musa ndio msingi wa mazoea ya ‘Ukristo’ uliopo.

Makuhani

Makanisa ya Katoliki na Anglikani yanatumia utaratibu ulio wazi mno wa ukuhani wa mwanadamu. Wakatoliki wa Roma wanamuona Papa wao kuwa yupo sawa na Kuhani wa Wayahudi. Yupo "Mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, Mwanadamu Kristo Yesu" (Tim 2:5) Basi. Haiwezekani kwamba Papa au makuhani wengine kuwa wapatanishi wetu kama Makuhani walivyokuwa chini ya Agano la Kale. Sasa Kristo ni Kuhani wetu pekee aliyekwenda mbiguni, akitoa maombi yetu kwa Mungu.

Haupo ushahidi kabisa wa Biblia wa kwamba mamlaka waliyokuwa nayo wazee waliopewa kipawa cha Roho karne ya kwanza - k.m Petro - waliwapa vizazi vilivyofuata au hasa kwa Papa. Hata kama uwezekano huu uliingizwa, hakuna njia iliyothibitisha kwamba Papa na Makuhani wenyewe ndio hao juu yao ambao vazi la kiroho la wazee wa kwanza liliwaungikia.

Vipawa vya Roho viliondolewa, Wote wanaoamini wana ruhusa iliyo sawa ya kutumia Roho- Neno lilo ndani ya Biblia (tazama masomo ya 2.2 na 2.4) Kwa sababu hii wote ni ndugu, hakuna awaye yote aliye na nafasi ya juu kiroho kuliko mwingine. Kweli, waaminio wote wa kweli ni washiriki wa ukuhani mpya kwa sababu ya wao kubatizwa katika Kristo, kwa maana ya kwamba wanaionyesha nje nuru ya Mungu katika ulimwengu wenye giza (1Petro 2:9). Kwa hiyo watakuwa wafalme - Makuhani wa Ufalme, utakapo wekwa duniani Kristo akirudi tena (ufunuo 5:10).

Mazoea ya Katholiki kuwaita makuhani wao ‘Baba’ (vile vile ‘Papa’ maana yake ni ‘baba.) yanapingana kabisa na maneno bayana ya Kristo" "Msimwite mtu baba duniani maana baba yenu ni mmoja. Aliye wa mbinguni"(Math 23:9). Kweli, Yesu alionya kumpa mtu - ndugu awaye yote heshima ya kiroho inayotakiwa na makuhani wa siku hizi: Ninyi msiitwe Rabi (mwalimu): maana mwalimu wenu ni mmoja, ndiye Kristo; nanyi nyote ni ndugu" (Math 23:8).

Mavazi yanayovaliwa na makuhani yenye mapambo sana, maaskofu na mapadri yana msingi wake katika vazi maalum lililovaliwa na makuhani katika kipindi cha Musa na Kuhani Mkuu. Uvaaji huu ulionyesha mbele kwenye tabia kamilifu ya Kristo, na kama pamoja na sheria yote, kusudi lake sasa limetimilika. Hakika ni ya Kuvunja Moyo, ya kuwa uvaaji ulilenga kuutukuza sana utukufu wa Kristo, na siku hizi uvaaji umesogeza utukufu wa wanadamu wanaovaa- wengine wanakiri ya kwamba hawakubali kuwa Kristo alifufuka hata uwepo wa Mungu.

Wazo la katholiki kwamba Mariamu ni kuhani ni kosa kubwa. Maombi yetu ni katika jina la KRISTO, sio Mariamu (Yon. 14:14,14; 15:16; 16:23-26). Kristo pekee ndiye kuhani wetu mkuu, sio Mariamu. Yesu aliwahi kumkemea Mariamu alipomjaribu awafanyie mambo wengine (Yn 2:2-4). Mungu sio Mariamu, huwaleta watu kwa Kristo (Yn 6:44).

FUNGU LA KUMI

Hii nayo ilikuwa sehemu ya Torati ya Musa(Hesabu 18:21), ambapo Wayahudi walitoa Fungu la kumi katika vitu vyao na kuwapa kabila ya Lawi ya ukuhani. Kwa kuwa sasa hakuna ukuhani wa kibinadamu, shurutisho haliwezi kuwapo tena la kutoa fungu la kumi kwa mzee awaye yote wa kanisa. Wazo potofu tena (katika suala hili la kuhusu makuhani) limewaongoza kwenye lingine (yaani, la kutoa fungu la kumi). Mungu mwenyewe hana haja ya matoleo yetu ya sadaka, kwa kuwa vitu vyote ni vyake (Zab. 50:8-13). Tunamrudishia Mungu tu kile ambacho ametupatia sisi (1 Nyak 29:14). Hatuwezi kupata wokovu kama tokeo la kutoa vitu vyetu viwe sadaka, kama katika masharti ya fedha. Katika kushukuru zawadi kubwa ya Mungu aliyotupatia, hatutoi tu sehemu ya fungu la kumi bali tunato maisha yetu yote. Katika haya , Paulo ameweka mfano, kweli akitendea kazi kile alichokihubiri: "Iitoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana" (Rum 12:1).

CHAKULA

Sheri ya wayahudi iliweka sheria fulani ya vyakula kuwa ni najisi- tabia iliyochukuliwa na madhehebu mengine, hasa ya nguruwe. Kwa sababu ya Kristo kuiondoa sheria juu ya msalaba, "Basi mtu asiwahukumu nyinyi katika vyakula, au vinywaji" (Kolos 2:14-16). Hivyo maagizo ya Musa kuhusu mambo haya yameondolewa na Kristo, kwa kuwa sasa amekuja. Alikuwa ni yeye ambaye ‘vyakula safi’ vilitabiri kuja kwake.

Ni wazi alieleza ya kuwa hakuna kitu anachokula mtu halafu kikamtia unajisi kiroho; ni kile kimtokacho ndani ya moyo ndicho hufanya hivi (Marko 7:15-23). " Kwa kusema hivi, Yesu alieleza kuwa vyakula vyote ni ‘safi’" (Marko 7:19). Petro alifundisha somo lile lile (Mdo 10:14,15), kama alivyofanya Paulo: "Najua tena nimehakikisha sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake" (Rum 14:14). Awali Paulo alitoa hoja ya kwamba kukataa vyakula fulani ilikuwa ishara ya udhahifu wa kiroho (Rum 14:2). Msimamo wetu wa vyakula "hakituhudhulishi mbele ya Mungu" (1Kor 8:8). Kwa yote yanayotia hatia zaidi ni onyo ambalo Wakristo wenye kuacha imani watafundisha watu, "kujiepusha na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokelewe kwa shukurani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli" (1 Tim 4:3).