Misingi Ya BIBLIA
Study 9: Ushindi Wa Yesu
Ushindi Wa Yesu | Damu Ya Yesu | Kutoa Dhabihu Kwa Ajili Yetu Na Kwa Ajili YaNafsi Yake Mwenyewe | Yesu Ni Mwakilishi Wetu. | Yesu Na Torati Ya Musa | Sabato | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Sanamu ndogo ya Yesu Msalabani, Je? Yesu alizaliwa December 25?) | Maswali

9.4 Yesu Ni Mwakilishi Wetu.

Tumeona kwamba dhabihu za wanyama hazikuwawakilisha kikamilifu watu wenye dhambi. Yesu alikuwa mjumbe wetu, kwa mambo yote "akafananishwa na ndugu zake" (Ebr 2:17). "Alionja mauti kwa ajili ya kila mtu" (Ebra 2:9). Tunapofanya kosa kama - tukiwa na hasira - Mungu aweza kutusamehe sisi "katika Kristo" (Efe 4:32). Hivi ni kwa sababu Mungu aweza kutulinganisha na Kristo mwanadamu aliyekuwa kama sisi alipojaribiwa kufanya dhambi - kama kukasirika - bali alishinda kila jaribu. Kwa hiyo Mungu aweza kutusamehe dhambi yetu- ya hasira kwa kule kuwa ndani ya Kristo, tukiwa tumefunikwa na haki yake. Kristo akiwa mwakilishi wetu, basi amekuwa na njia ambayo Mungu anaweza kutuonyesha neema yake, wakati tukithibitisha mambo ya haki yake mwenyewe.

Ikiwa Yesu alikuwa ni Mungu na siye mtu aliye na mwili wa Adamu tu, asingekuwa mwakilishi wetu. Huu ni mfano mwingine wa wazo moja potofu linalokwenda kwenye lingine. Kwa sababu hii, watu wa dini wameendeleza njia nyingi zilizo ngumu kufahamika kueleza mauti ya Kristo. Mtazamo wa madhehebu mengi ya Kikristo yaliyo kengeuka ni kwamba dhambi za mwanadamu zimemfanya awe na deni kwa Mungu ambalo yeye mwenyewe hakuweza kulipa. Ndipo Kristo akalipa deni la kila mwamini kwa damu yake, iliyomwagika msalabani. Wahubiri wengi wa kwenye baraza la Injili wameeleza namna hii; "Ilikuwa kana kwamba tulikuwa tumepangwa kwenye ukuta, karibu kupigwa risasi na ibilisi. Wakati huo Yesu akakimbilia ndani kwa haraka; badala yetu ibilisi akampiga, sisi tupo huru".

Maelezo ya mawazo haya hayana uthibitisho wowote imara wa Biblia. Yameachana wazi ikiwa kama Kristo alikufa badala yetu, wakati huo tusife. Kama bado tuna mwili wa Adamu, bado yatupasa kufa; wokovu toka dhambi na mauti mwishoni utafunuliwa kwenye hukumu (tutakapopewa kutoharibika). Huu hatukupokea wakati wa kufa Kristo. Mauti ya Kristo yalimharibu ibilisi (Ebr 2:14) na sio Ibilisi alimwangamiza yeye.

Biblia inafundisha ya kwamba wokovu umepatikana kwa njia ya mauti ya Kristo NA ufufuo, na sio kwa mauti yake. Kristo "alikufa kwa ajili yetu" mara moja. Wazo la kuwa badala ya mwingine lina maana ya kwamba yeye mwenyewe ilimpasa kufa kwa ajili ya kila mmoja wetu.

Ikiwa Kristo alilipa deni kwa damu yake, wokovu wetu unakuwa ni jambo lingine ambalo tunaweza tegemea kama ni haki. Ukweli ni kwamba wokovu ni zawadi (kipawa), kimeletwa kwa neema na msamaha wa Mungu, unapotea machoni ikiwa tunaelewa dhabihu ya Kristo kuwa ni malipo ya deni. Vile vile inadaiwa kwamba hasira ya Mungu ilitulizwa mara alipoiona damu yake Yesu. Lakini kile ambacho Mungu anaona tunapotubu ni mwanae kama ni mwakilishi wetu, ambaye tunajaribu kuiga mwenendo wake, sio tunajiunga na damu ya Kristo kama kitu cha kutupa bahati njema. Utenzi na nyimbo nyingi za ‘Kikristo’ zina kiasi cha kushangaza mafundisho potofu katika eneo hili. Mafunzo potofu zaidi yameingia mioyoni mwa watu kwa njia ya miziki, kuliko kwa busara, mafundisho ya Biblia. Siku zote yatupasa kujihadhari na aina hii ya msukumo wa kukataa mafundisho ya kweli kwa kupokea yaliyo ya upotoshaji.

Kwa huzuni sana, maneno rahisi "Kristo alikufa kwa ajili yetu" (Rum 5:8) yameelekwa vibaya sana kwa maana ya kuwa Kristo alikufa badala yetu. Kama idadi ya miunganiko kati ya Warumi 5 na 1 Wakorintho 15 (k.m mst 12=1Kor 15:21 mst 17= Kor 15:22). "Kristo alikufa kwa ajili yetu" (Rum 5:8) umelingana na "Kristo alikufa kwa sababu ya dhambi zetu" (1Kor 15:3). Kifo chake kilikuwa kikifanya njia ya kutuwezesha tupate msamaha wa dhambi zetu, ilikuwa namna hii ya kusema ya kwamba "Kristo alikufa kwa ajili yetu". Neno ‘kwa’ halina sharti la maana ya ‘badala ya’; Kristo alikufa "kwa ajili ya dhambi zetu", sio badala yao. Kwa sababu hii, Kristo anaweza "kutuombea" tukimjia Mungu (Ebra 7:25), sio ‘badala yetu’. Wala "kwa" halina maana ya ‘badala ya’ katika Ebra 10:12 na Gal 1:4.