Misingi Ya BIBLIA
Somo La 7: Mwanzo wa Yesu
Unabii unaomhusu Yesu kwenye Agano la Kale | Kuzaliwa na Bikira | Nafasi ya Kristo katika mpango wa Mungu | "Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno" (Yohana 1:1-3) | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Yesu wa Historia, Nimeshuka kutoka Mbinguni, Je? Yesu aliumba Dunia, "Kabla ya Ibrahimu, Nalikuwepo" (Yn. 8:58), Melkizedeki) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 24: Je? Yesu aliumba Dunia

"Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote: kwa kuwa katika yeye (Yesu) vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi,vinavyoonekana na visivyoonekana ikiwa ni viti vya enzi, au Usultani, au enzi,au mamlaka; vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikamana katika yeye. Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani cha Kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu ………"(Kol. 1: 15 -18). Maneno hayo ni mfano huu mmoja unaoweza kutoa fikira za kwamba Yesu hasa aliumba nchi.

  1. Ikiwa huu mfano ulikuwa kweli, basi maneno mengine mengi yamepingana yanayofundisha kwamba Yesu hakuwahi kuwepo kabla ya kuzaliwa. Ni wazi taarifa iliyo katika kitabu cha Mwanzo inafundisha kuwa Mungu aliumba. Aidha Yesu au Mungu walikuwa waumbaji; kama tukisema kwamba Yesu alikuwa muumba ambapo Mwanzo inasema ni Mungu, moja kwa moja tunasema kwamba muumba Yesu alikuwa sawa na Mungu. Katika Suala hili haiwezekani kuielezea mistari mingi inayoonyesha tofauti zilizopo kati ya Mungu na Yesu (Ona Somo la 8.2 kwa mifano hii).

  2. Yesu alikuwa"Mzaliwa wa kwanza"ambaye anadokezwa kuanza. Hakuna ushahidi wa kwamba Yesu alikuwa ni"Mzaliwa wa kwanza"kabla ya uumbaji wa dunia yenyewe. Mafungu ya Maneno kama yaliyo kwa 2 Sam. 7: 14 na Zab. 89: 27 yalitabiri kwamba mtoto halisi wa Daudi atakuwa mzaliwa wa kwanza wa Mungu. Ni wazi hakuwahi kuwapo wakati maneno haya yakiandikwa, na kwa sababu hiyo sio wakati wa uumbaji wa mwanzo. Yesu alidhihirishwa"kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu", kwa ufufuo wa wafu (Rum. 1: 4) Mungu kwa kutimiza ahadi iliyomfufua Yesu kama ilivyoandikwa katika zaburi ya pili; Yesu akawa mzaliwa wa kwanza kwa kufufuliwa kwake. Ujue vilevile kuwa mwana aliyesimama mkono wa kuume wa Baba yake ameungwa pamoja na kuwa mzaliwa wa kwanza (Mwa. 48: 13 -16), naye Kristo aliinuliwa mkono wa kuume wa Mungu baada ya kufufuliwa kwake (Matendo.2: 33; Ebra. 1:3).

  3. Ni kwa maana hii ambayo Yesu amesemwa ya kuwa ni mzaliwa wa kwamza kutoka wafu (Kol. 1: 18), msemo uliosambamba na"mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote (Kol. 1: 15). Kwa hiyo anajisema mwenyewe kuwa ni"mzaliwa wa kwanza wa waliokufa …. Mwanzo wa kuumba kwa Mungu"(Uf. 1: 5, 3: 14). Yesu alikuwa ni wa kwanza kwa uumbaji mpya wa watu wasiokufa wanaume na wanawake,ambao ufufuo wao na kuzaliwa kabisa wakiwa ni wana wa Mungu wasiokufa umewezeshwa na kifo chake Yesu na ufufuo wake (Efe.2:10; 4:23,24; 2 Kor.5:17)"Katika Kristo wote (waamini wa kweli) watahuishwa. Lakini kila mmoja mahala pake; limbuko - wa kwanza ni Kristo, baadaye walio wake Kristo, atakapokuja"(1 Kor. 15: 22, 23). Hili ni jambo moja na Kol. 1: Yesu alikuwa ni mtu wa kwanza kufufuka kutoka wafu na kupewa kutokufa, alikuwa wa kwanza kwa uumbaji mpya, nao waamini wa kweli watafuata mfano wake mzuri akirudi.

  4. Basi uuumbaji uliosemwa katika Kol.1 unatajwa uumbaji mpya, sio huo ulio kwenye kitabu cha mwanzo. Kwa njia ya kazi ya Yesu"Vitu vyote viliumbwa …… ikiwa ni viti vya enzi …au mamlaka"n.k. Paulo hasemi kwamba Yesu aliumba vitu vyote na kisha akatoa mifano ya mito, milima, ndege n.k. Vitu vya huu uumbaji mpya zinatajwa hizo thawabu ambazo tutazipata kwenye Ufalme wa Mungu."Viti vya enzi ….. Mamlaka n.k. wanatajwa waamini watakao fufuliwa jinsi watakavyokuwa"Wafalme na Makuhani, nasi tutakuwa na mamlaka juu ya nchi"(Uf. 5: 10) Vitu hivi viliwezeshwa kwa kazi ya Yesu."Katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni ……"(Kol. 1: 16). Katika Efe. 2: 6 tunawasomo waamini walio katika Kristo wamekaa katika ulimwengu wa roho - yaani "wameketi sehemu za kimbingu". Hivyo mistari hii inafundisha kwamba nafasi ya kupandishwa kiroho ambayo sasa tunaweza kuwa nayo, sawa na ile tutakayo kuwa nayo wakati ujao, yote imewezeshwa na Kristo."Mbingu na nchi"zina "Mambo yote ambayo yalihitajika kuyafanyia upatanisho kwa damu ya Kristo msalabani"(Kol. 1: 16, 20), yanaonyesha kwamba"Vitu vyote …. Vilivyo mbinguni"wanatajwa waaminio ambao sasa wanaketi katika ulimwengu wa roho -"nafasi za kimbingu katika yeye Kristo Yesu"Sio vitu vyote vya kimaumbile vinavyotuzunguka.


  Back
Home
Next