Misingi Ya BIBLIA
Somo La 7: Mwanzo wa Yesu
Unabii unaomhusu Yesu kwenye Agano la Kale | Kuzaliwa na Bikira | Nafasi ya Kristo katika mpango wa Mungu | "Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno" (Yohana 1:1-3) | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Yesu wa Historia, Nimeshuka kutoka Mbinguni, Je? Yesu aliumba Dunia, "Kabla ya Ibrahimu, Nalikuwepo" (Yn. 8:58), Melkizedeki) | Maswali

7.3 Nafasi ya Kristo katika mpango wa Mungu

Mungu hafanyi Uamuzi wa mipango yake bila kufikiri, akivumbua sehemu za ziada kwa kusudi lake kama historia ya mwanadamu inavyofunua. Mungu alikuwa na mpanngo kamili ulioelezwa kwa taratibu tangu mwanzo wa uumbaji (Yn. 1:1). Nia yake kuwa na mwana katika mpango wake basi ulikuwa toka mwanzo. Agano la Kale linadhihirisha maelekeo tofauti - tofauti ya Mungu kwenye mpango wake wa wokovu katika Kristo.

Mara nyingi tumeonyesha kwa kueleza kuwa katika ahadi, unabii wa utabiri, na mifano ya torati ya Musa, Agano la Kale daima linafunua kusudi la Mungu kwa Kristo. Ilikuwa ni kwa sababu ya maarifa ya Mungu hata akawa na mwana, ndipo uumbaji Mungu akaufanya uwepo (Ebra. 1: 1, 2, neno dogo la kiyunani;"kwa"katika U.V. ni bora ingetafsiriwa"sababu ya"). Ilikuwa sababu Kristo hata enzi za historia ya mwanadamu ziliruhusiwa na Mungu (Ebra.1: 2 (kiyunani). Kinachofuata ni kwamba ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu kushuka chini katika miaka, kama taarifa ilivyoandikwa katika Agano la Kale, ina ushahidi tele wa Kristo.

Ubora wa Kristo na ukubwa wake mno na umuhimu wa asili kwa Mungu ni vigumu kwetu kufahamu kabisa. Basi ni kweli kusema kwamba Kristo alikuwamo ndani ya fikira za Mungu na kusudi tangu mwanzo, ingawa alikuja kuishi tu kimwili alipozaliwa na Mariamu. Waebrania 1: 4, 7, 13,14 inasisitiza kwamba Kristo hakuwa Malaika wakati akiwa na mwili unaopatikana na mauti alikuwa mdogo punde kuliko Malaika (Ebra. 2:7), alikuja inuliwa kuwa na heshima kubwa kuliko wao sababu alikuwa ni"Mwana wa pekee wa Mungu"(Yn. 3: 16). Awali tumeonyesha ya kwamba namna pekee ya kuwako ambako Maandiko yamefundisha ni kuishi kwa umbo la mwili, kwa hiyo Kristo hakuishi akiwa'Roho’ kabla ya kuzaliwa. 1 Pet. 1: 20 unaisema nafasi kwa machache; Kristo"alijulikana tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia, lakini alifunuliwa mwisho wa zamani hizi". Yesu alikuwa kiini kikuu cha Injili, ambacho Mungu'aliahidi kabla kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko Matakatifu, yaani, habari za mwanawe, …….. Yesu Kristo Bwana wetu, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili; na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya Utakatifu, kwa ufufuo wa wafu’ (Rum. 1:1 -4).

Hivi unaeleza Muhutasari wa historia ya Kristo: -

  1. Aliahidiwa katika Agano la Kale - yaani, katika mpango wa Mungu

  2. Aliumbwa akiwa mtu aliye na mwili kwa kuzaliwa na bikira, akiwa ni mzao wa Daudi;

  3. Kwa ajili ya tabia timilifu ("roho ya Utakatifu"), iliyoonekana wakati wa maisha ya mwili unaopatikana na mauti.

  4. Alifufuliwa, na tena hadharani alielezewa kuwa ni Mwana wa Mungu na mitume waliopewa kipawa cha roho ya kuhubiri.

MAARIFA YA MUNGU

Tutakuwa tumesaidiwa mno kufahamu jinsi gani Kristo alikuwa ndani ya Moyo wa Mungu hapo mwanzo, ambapo kwa mwili hakuwapo, kama tukiukubali ukweli kwamba Mungu anajua mambo yote ambayo yatatokea'wakati ujao’; Ana maarifa ya kujua jambo kabla halijatokea. Kwa sababu hiyo Mungu anaweza kusema na kufikiri kuhusu mambo ambayo hayapo, kana kwamba yapo. Haya ndiyo maarifa yake kabisa ya wakati unaokuja. Mungu'anataja mambo yasiyokuwepo kana vile yapo’ (Rum. 4:17). Kwa sababu hiyo anaweza kueleza"Mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote"(Isa. 46: 10).Kwa sababu hii, Mungu anaweza kutangaza wafu kama kwamba wapo hai, na anaweza kuwasema watu kama wapo hai kabla ya kuzaliwa.

"Shauri", au neno la Mungu, lilimtabiri Kristo tangu mwanzo; alikuwa siku zote katika kusudi la Mungu au"mapenzi". Basi ilikuwa yakini kwmba wakati fulani Kristo kwa mwili atazaliwa; Mungu atatimiza kusudi lake alilolisema katika Kristo. Uhakiki wa maarifa ya Mungu kujua mambo kabla, umeletwa ndani ya neno lake lililo la kweli. Biblia ya kiebrania ina kiarifa cha'utimilifu wa unabii’, (1 Nyak. 22: 1), wakati bado hekalu lilikuwa limeahidiwa tu na Mungu. Hiyo ilikuwa imani yake kwa neno hilo la ahadi ambayo Daudi alitumia wakati aliokuwapo kutangaza mambo ya wakati ujao. Maandiko yana mifano tele ya Maarifa ya Mungu kujua mambo kabla. Mungu alikuwa na hakika mno kwamba atatimiza ahadi kwa Ibrahimu, ambayo alimwambia:"Uzao wako nimewapa nchi hii …."(Mwa. 15:18) wakati Ibrahimu hata mtoto hakuwa naye. Wakati wa kipindi kile kile kabla ya uzao (Isaka / Krsito) haujazaliwa, tena Mungu akamwahidi:"Nimekuweka uwe Baba wa mataifa mengi"(Mwa. 17: 5). Kweli,Mungu"hutaja hayo mambo yasiyokuwapo kana kwamba yapo"

Kristo alisema hivyo wakati wa utumishi wake jinsi Mungu'amempa vyote mikononi mwake (Kristo)"(Yn. 3:35), ingawa suala hili wakati ule halikuwa hivyo."umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake (Kristo) ….. lakini sasa hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake"(Ebra. 2: 8).

Mungu alitangaza mpango wake wa wokovu kupitia kwa Kristo"kama alivyosema tangu mwanzo kwa kinywa cha manabii wake watakatifu"(Luk. 1: 70). Kwa sababu walijumuika kwa karibu sana na mpango wa Mungu, watu hawa wamesemwa kana kwamba wenyewe waliishi mwanzo, ingawa suala si hivyo. Badala yake, tunaweza kusema manabii walikuwa katika mpango wa Mungu tangu mwanzo. Yeremia ni mfano mkuu. Mungu alimwambia:"Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua; na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa"(Yer. 1:5). Hivyo Mungu alijua kila kitu kumhusu Yeremia hata kabla ya uumbaji. Kwa namna hiyo Mungu aliweza kusema kuhusu mfalme wa Uajemi, Koreshi, kabla ya kuzaliwa kwake, akitumia msemo unaodokeza wakati ule alikuwako (Isa. 45: 1 -5). Waebrania 7: 9-10 ni mfano mwingine wa msemo huu wa kuwako kiumbe umetumika kumhusu mtu ambaye wakati ule alikuwa hajazaliwa.

Kwa njia iyo hiyo kama Yeremia na manabii wamesemwa kama wanaishi hata kabla ya uumbaji, kwa ajili ya wao kushiriki katika mpango wa Mungu, hivyo waamini wa kweli wamesemwa kuwa wanaishi wakati ule. Ni dhairi kwamba kimwili hatukuishi wakati ule isipokuwa katika fikira za Mungu. Mungu"alituokoa akatuita kwa wito mtakatifu ……… bali kwa makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele"(2 Tim.1:9). Mungu"alivyotuchagua katika yeye (Kristo) kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu …. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua …. Sawa sawa na uradhi wa mapenzi yake"(Efe. 1: 4,5). Wazo zima kwa kila mmoja kutangulia kujulikana na Mungu tangu mwanzo, na kwisha kuchaguliwa kwa wokovu, inaonyesha kwamba walikuwemo katika fikira za Mungu hapo mwanzo (Rum. 8: 27; 9:23).

Kwa mwangaza wa yote haya, Sio ajabu kwamba Kristo, kama kujumlisha kusudi la Mungu, anaweza kusemwa kama amekuwapo tangu mwanzo katika mawazo ya Mungu na mpango, ingawa kwa mwili hakufanya hivyo. Alikuwa ni"Mwana-kondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu"(Uf. 13: 8). Yesu mwenyewe hakufa wakati ule; alikuwa ni"Mwana-kondoo wa Mungu"aliyetolewa kuwa sadaka karibu miaka 4,000 baadaye Msalabani (Yn. 1:29; 1 Kor. 5:7). Kwa njia hiyo hiyo kama Yesu alivyochaguliwa tangu mwanzo (1 Pet 1:20), hivyo na waaminio (Efe. 1: 4; kwa Kiyunani ni neno moja"kuchaguliwa"limetumika katika mistari hii). Shida yetu kwa kufahamu yote haya ni kwa sababu hatuwezi kwa urahisi kufikiri jinsi Mungu anavyoshughulika nje ya wazo la wakati.'Imani’ ndio uwezo wa kutazama mambo toka mtazamo wa maana ya Mungu, pasipo sharti la muda.


  Back
Home
Next