Misingi Ya BIBLIA
Somo La 6: Mungu Na Ubaya
Mungu Na Ubaya | Ibilisi Na Shetani | Mapepo - Mashetani | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Uchawi, Edeni palitokea nini?, Lusifa, Majaribu ya Yesu, Vita Mbinguni) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 20: Majaribu ya Yesu

Mathayo 4: 1 -11:"Kisha Yesu akapandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwishowe akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia; Ukiwa ndiwe mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Kiisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia; Ukiwa ndiwe mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia Malaika zake; na mikononi watakuchukua usije ukavunjika mguu wako katika jiwe. Yesu akawaambia, tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha miliki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. Ndipo Yesu alipomwambia, nenda zako, shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, Umwabudu yeye peke yake. Kisha Ibilisi akamwambia na tazama, wakaja Malaika wakamtumikia".

TAFSIRI YA WATU WALIO WENGI

Maneno haya yanasomwa kuwa na maana ya kuwa kiumbe aitwaye"Ibilisi alimjaribu Yesu kutenda dhambi kwa kutoa shauri la mambo fulani kwake na kumwongoza katika sehemu za kumjaribu.

UFAFANUZI

 1. Yesu "alijaribiwa sawa sawa na sisi kwa mambo yote, bila kufanya dhambi" (Ebra. 4:15), na "kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa"(Yak. 1: 14). Tunajaribiwa na"Ibilisi"wa tamaa yetu wenyewe au nia mbaya, ndivyo hata Yesu. Hatujaribiwi na kiumbe mbaya asimamaye ghafla karibu yetu akitushurutisha kutenda dhambi - dhambi na majaribu huja"toka ndani"ya moyo wa mtu"(Marko. 7:21).

 2. Ni wazi majaribu hayawezi kuchukuliwa kwa jinsi ya maana hasa ya maneno: -

  • Mathayo 4: 8 anadokeza ya kwamba Yesu alichukuliwa mpaka mlima mrefu ili kuona miliki zote za ulimwengu na fahari ijayo"kwa dakika moja"(Luk. 4:5). Haupo mlima mrefu wa kutosha kuuona ulimwengu wote. Ni kwa sababu gani urefu wa mlima ulimwezesha Yesu kuona ulimwengu utakavyokuwa baadae ?. Dunia ikiwa duara, hakuna maana toka uso wake mtu akaweza kuona pande za ulimwengu kwa dakika moja.

  • Mlinganisho wa Math. 4 na Luk. 4 unaonyesha kwamba majaribu yameelezwa kwa mpangilio unaohitilafiana. Marko 1: 13 anasema Yesu alikuwa"Jangwani siku arobaini, akijaribiwa na shetani", Wakati Math. 4: 2-3 anasema ya kuwa 'alipofunga siku arobaini …... mjaribu (shetani) akamjia ……".Kwa sababu maandiko hayawezi kujipinga yenyewe, tunaweza kusema kwamba majaribu yale yale yalikaa yakirudiwa -rudiwa yenyewe. Jaribu la kubadili mawe kuwa mkate ni mfano bayana. Kwa uzuri huu utafaa ikiwa haya majaribu yalitokea ndani ya moyo wa Yesu. Akiwa na mwili wetu, kukosa chakula kulimdhuru kiakili na kimwili, na hivyo moyo wake kwa urahisi ulianza kuwaza mambo. Kukaa siku chache bila kula kwa wengine wanaweza kuweweseka au kuzimia (1 Sam. 30: 12). Hali iliyo sawa kati ya mkate na mawe umetajwa na Yesu kwa Mathayo 7:9, hapana shaka mifano hiyo mara nyingi iliungana na mawazo yake yaliyoumia vibaya - ingawa siku zote upesi uliyatawala kwa kuamuru yarudi nyuma kwa Neno.

  • Inaweza kuwa Yesu aliwaambia waandishi wa Injili habari ya majaribu yake, na kukiri kwa maneno yaliyokuwa ya nguvu aliyoyapata, inawezekana alitumia mfano ulioufikia ulionekana kwa Math. 4 na Luk. 4.

Anaonekana namna tofauti ibilisi aliyemwongoza Yesu kupita jangwani na mitaa ya Yerusalemu kisha walipanda kinara cha hekalu pamoja, wote kwa mtazamo wa udadisi wa Wayahudi. Josephus hatoi taarifa yoyote ya kutokea hii - kwa kuthubutu kungesababisha vurugu kubwa. Kwa hali moja, ikiwa haya majaribu yalitokea mara kadhaa ndani ya siku arobaini sawa na mwisho wa kipindi hicho (ambacho yalifanya karibu mara mbili, kwa kuwa Mathayo na Luka wanayo kwa mpangilio unaotofautiana), ni jinsi gani Yesu alikuwa na muda wa kutembea (n.b ibilisi"akampandisha"pale) kwenye mlima mrefu ulio karibu (ambao wanaweza kuwa ulikuwa Hermoni upande wa mbali Kaskazini mwa Israeli), kupanda hata kileleni na kushuka chini tena, kurudi jangwani na kisha kurudia zoezi ? Majaribu yake yote yalitokea jangwani - alikuwepo kule kwa siku arobaini, akajaribiwa muda wote na ibilisi (ambaye alimwacha mwishowe - Math. 4: 11). Ikiwa Yesu alijaribiwa na ibilisi kila siku, na majaribu yalitokea jangwani tu, basi ni kwamba Yesu hakuondoka jangwani kwenda Yerusalemu au kusafiri ili kupanda mlima mrefu. Kwa hiyo mambo haya hayakuweza kutukia kwa jinsi ya maana ya maneno yalivyo.

 • Kama ibilisi ni mtu aliye na mwili ambaye haheshimu Neno la Mungu naye anapenda kuwakosesha watu, basi ni kwa nini Yesu alinukuu Maandiko ili kushinda ? Kulingana na mtazamo wa walio wengi, hii isingemwondoa Ibilisi. Fahamu kuwa Yesu alinukuu fungu la maneno ya Biblia kwa kila wakati. Ikiwa ibilisi yalikuwa ni mawazo mabaya ndani ya moyo wa Yesu, basi inaeleweka kwamba kwa tendo la kuwa na Neno la Mungu ndani ya moyo wake na kujikumbusha mwenyewe, aliweza kuyashinda mawazo haya mabaya. Zab. 119: 11 ni ya muhimu ambapo labda ni bayana alikuwa anatoa unabii wa yaliyompata Kristo jangwani:"Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi".

 • Math. 4: 1 unasema kwamba Yesu "alipandishwa na roho jangwani (ukipenda nyikani), ili ajaribiwe na ibilisi". Huyu alikuwa ni Roho kustaajabisha Roho wa Mungu kumpeleka Yesu jangwani ili akajaribiwe na kiumbe anayemzidi mwanadamu kwa maarifa aishiye kwa kupingana na Mungu.

MAELEZO YAMEDOKEZWA: -

 1. Yesu alipobatizwa mto Yordani na Yohana, alipokea nguvu za Roho Mtakatifu (Math. 3: 16). Mara alipotoka majini, alipelekwa kwenda nyikani kujaribiwa. Akiisha kuwa na uweza wa roho kugeuza mawe kuwa mkate, kuruka jengo bila kudhurika n.k, majaribu haya ilibidi yatamani vitu moyoni mwake. Ikiwa ni mtu alikuwa adokeza mambo haya kwa Yesu naye akijua mtu huyo ni mtenda dhambi, basi majaribu yalikuwa magumu kidogo kuliko kama yaliyotoka ndani ya moyo wa Yesu.

 2. Jaribu la kuutwaa ufalme wake lilikuwa na nguvu mno ikiwa lilitoka ndani ya Kristo. Moyo wa Yesu ulikuwa umejaa Maandiko, na kwa hali ya kuumia moyo, Kulikosababishwa na aumu, ilimjaribu atumie vibaya maneno ili kumwezesha kujihesabia haki ya kuchukua njia rahisi ya kujiepusha na mazingira aliyokuwemo. Kusimama juu ya mlima mrefu kunakumbusha Ezekieli akiisha kuonyeshwa ufalme utakavyokuwa toka mlima mrefu (Ezek. 40: 2), na Yohana akiuangalia"Mji mtakatifu wa Yerusalemu"toka "mlima mrefu mkubwa"(Uf. 21: 10). Yesu aliuona ufalme wa ulimwengu kama utakavyokuwa wakati ujao (Luk. 4: 5), yaani, akiwa katika ufalme, hapo "Falme za ulimwengu huu unakuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake"(uf. 11:15).

 3. Inawezekana aliwaza Musa mwishoni mwa miaka 40 ya kuzunguka jangwani (siku zake 40) akitazama nchi ya Ahadi (Ufalme) toka mlima Nebo. Mkazo umewekwa kwa (Dan. 4:17, 25, 32; 5: 21) kwamba "aliye juu hutawala katika falme za wanadamu, naye humpa amtakaye" Yesu aliishajua kuwa, ni Mungu pekee, sio mtu mwingine, atampa ufalme. Kwa hiyo lisingekuwa jaribu sana kama ni mtu mbaya ndiye aliyedai kuweza kumpatia Yesu ufalme, lingebidi litolewe shauri na 'iblisi’ ndani ya Yesu kwamba ataweza kuuchukua huo ufalme mara moja. Isitoshe, aliweza kujihoji, Mungu amenipa Mamlaka kwa matazamio (Yoh. 5: 26, 27), kwa upana ambao pande mbili zote alikuwa na uwezo kutoa uhai wake na kuutwaa tena (Yoh. 10: 18), ingawa hatimaye uweza wote alipewa baada ya kifo na kufufuka kwake tu (Math. 28: 18).

 4. Kwa uzoefu wake wa Maandiko, Kristo aliona hali moja kati yake mwenyewe na Eliya, moyo wake ulikata tamaa baada ya siku 40 jangwani (1 Fal. 19: 8) na Musa, ambaye alipoteza urithi wake haraka wa nchi mwishoni mwa miaka 40 ya kuzunguka jangwani. Yesu, mwishoni wa siku 40, alikuwa na hali ya nafasi moja nao - akikabiliwa na uwezekano wa ukweli wa kushindwa Eliya na Musa walishindwa kwa sababu ya udhaifu wa mwanadamu - sio kwa sababu ya mtu aitwaye "Ibilisi". Ulikuwa ni huu udhaifu wa mwanadamu,"shetani" au adui, ndiyo ulikuwa unamjaribu Yesu.

"Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe mwana wa Mungu, ……."(Luk. 4: 3). ilibidi majaribu yawe yakidumu bila kubadilika ndani ya nia ya Yesu kuhoji ikiwa kwa kweli alikuwa Mwana wa Mungu, kwa kuwa kila mmoja aliwaza ni mtoto wa Yusufu (Math. 1: 1, 6; Luk. 3: 23, palipo na neno"akidhaniwa"maana yake'alihesabiwa kwa sheria’). Alikuwa ni mtu wa pekee kutokuwa na Baba mwanadamu. Wafilipi 2: 8 unashauri la kwamba Yesu alikubali kuwa ni kweli alikuwa binadamu kama sisi, kwa kujua sababu yake alikuwa akijaribiwa kutoamini alikuwa ni Mwana wa Mungu, au kutouelewa mwili wake mwenyewe.

Majaribu yalitawaliwa na Mungu kwa elimu ya kiroho ya Kristo. Maneno aliyonukuu Yesu kujipa moyo mwenyewe dhidi ya mawazo yake mabaya ("Ibilisi") yote yapo sehemu ile ile kumbukumbu la Torati, kuhusu yaliyowapata Israeli Jangwani. ni wazi Yesu aliuona usawa kati ya yaliyomsibu yeye na wao:-

KUM. 8

Math. 4 /Luka 4

mst. 2

"Bwana Mungu wako alikuongoza miaka arobaini katika jangwa, ili akutweze, Kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo"

 

"Yesu alipandishwa na roho""siku arobaini""Jangwani"Yesu alitwezwa kwa majaribu. Yesu aliyashinda kwa kunukuu Maandiko yaliyo kuwa moyoni mwake. (Zab. 119: 11).

mst.3.

"Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana…apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu imetafsiriwa na haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana

 

"Mwisho akaona njaa"Katika Yohana 6 mana Yesu kuwa ni Neno la Mungu ambalo Yesu aliishi kwa hilo jangwani. Yesu alijifunza kwamba kiroho alikuwa akiishi"Akawaambia ……. Imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila neno la Mungu"

mst. 5.

"Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile Baba amrudiavyo mwanaye, ndivyo Bwana, Mungu wako, akurudivyo"

 

Bila shaka Yesu aliwaza kwa yaliyompata.Mungu alimrudi mwanawe, Yesu 2 Sam.7: 14; Zab. 89:32.

Hivyo Yesu ametuonyesha jinsi ya kusoma na kujifunza neno - aliwaza yeye mwenyewe nafasi ya Israeli walipokuwa jangwani, kwa hiyo alichukua masomo ya kujifunza toka yaliyowapata mwenyewe kwa majaribu yake katika jangwa.


  Back
Home
Next