Misingi Ya BIBLIA
Somo La 6: Mungu Na Ubaya
Mungu Na Ubaya | Ibilisi Na Shetani | Mapepo - Mashetani | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Uchawi, Edeni palitokea nini?, Lusifa, Majaribu ya Yesu, Vita Mbinguni) | Maswali

Tumeacha Kitambo sehemu ya 17: Uchawi

Sehemu hii imeandikwa kwa upana kwa kuwapatia hao wahitaji walio Afrika na pande zingine za ulimwengu ambako uchawi ni jambo lililoenea kwa maisha ya kila siku. Imejulikana na wasomaji wengi wa Biblia kwamba wanawaendea wachawi, Waganga wa Kiafrika na wengineo hawapatani na kushika kweli. Walakini, nafahamu kuwa waganga wa kienyeji wakiwa rahisi na mara nyingi wanasifika kuliko matabibu wa dawa za kisasa, wameunganisha kufaulu kwao kunakoonekana, kunawafanya wavutiwe. Tunataka kujua tatizo hili, kwa akili timamu, kwa njia ya Biblia. Hii ndiyo njia pekee utapata nguvu ya kupinga majaribu ya kuwatumia watu hawa .

MADAI YA UCHAWI

Ya kwanza, madai ya uchawi huu hufanya kufanikiwa haja ya kuchambua. Tunaweza kuwa na hakika ya kuwa sifa nyingi zinakwenda katika madai yaliyofanywa kwa mafanikio yao. Tiba zao hazifanywi kwa kuonekana wazi, ili wote waone. Ikiwa kweli zimekuwa na mafanikio basi labda walikuwa wakifanya kazi katika mahospitali, na wangepatikana ulimwenguni pote. Hali hasa ya hao wanaodai kuwaponya pia haieleweki - kiasi gani kweli wanapona haipo wazi.

Ninyi kati yenu mnaokabiliana na majaribu haya mnatakiwa mjiulize wenyewe ikiwa mnaushahidi bayana wa uweza wao - k.m. umewahi kuona (hujawai kusikia kuhusu) mtu aliyekatwa mkono na msumeno amekwenda kwa mchawi na kurudi na mkono mwingine unaofanya kazi sawa sawa ?. Huu ni aina ya ushahidi tunaouhitaji kabla ya kuwapa lolote la kuwasadikisha kabisa. K/Torati 13: 1-3 ni lenye nguvu sana: Israeli waliambiwa kwamba kama mchawi akitoa ishara au ajabu ambayo inaonekana kuwa muujiza, hawakutakiwa bado kumwamini mtu huyo isipokuwa wakinena mafundisho ya kweli kama yaliyodhihirika ndani ya Biblia. Ni bayana kwamba mchawi au mganga wa kienyeji haamini kweli katika neno la Mungu - kwa hiyo tusijaribu kuwasadiki kuwa wana uwezo wa kweli, kwa kuwa uwezo wote watoka kwa Mungu (Rum. 13: 1; 1 Kor. 8: 4-6).

Pili, aina ya magonjwa wanayoshughulikia ni ya maana, imegundulika sasa ya kuwa tunatumia karibu 1% tu ya nguvu ya ubongo wetu. zinazobaki zinaonekana kuwa nje ya nguvu zetu kwa fahamu kutoa nguvu (bila shaka tutafanya hivyo kwenye ufalme). Pasipo kuelewa, fikira zetu zinaweza kuwa karibu na matokeo ya viungo vya miili yetu. Hivyo watafiti wa akili ya binadamu wamejulikana kwa kuponya magonjwa ya damu za watu kwa mkazo wa kupima damu zao vema na jumla ya viungo vya mtu na kufanya kazi kawaida. Madaktari wanakiri kwamba pengine tiba hii inayofanyika ambayo haitegemei juu ya dawa za imani. Vivyo, kuwa na mawazo mengi yaweza kusababisha vidonda vya tumbo na maumivu ya kichwa. Kuipumzisha akili au kufanya mazoezi kwa namna fulani yaweza maumivu kuondoka. Lakini kama, kwa mfano, mkono wetu umekatwa na msumeno, hakuna kiasi cha mazoezi ya akili kinachoweza kurudisha tena. Ni fikira zetu pekee zinazotawala magonjwa ambayo wachawi waonekana kuweza kuyageuza. Kwa sababu hatujui vya kutosha namna fikira zetu zinavyofanya kazi, hii inaonekana kuwa kwa ajili ya nguvu nyingine za mwili ambazo hawa waganga wa kienyeji wanazo. Lakini hivi sivyo; ni kwa ushawishi wao juu ya fikira za watu unaoleta matokeo haya..

CHANZO CHA UWEZO

Kwa kadri yeyote, uweza wote ni wa Mungu, Mambo ya pande mbili mazuri na mabya kama haya magonjwa yaletwa na yeye - sio wachawi. Haya ni mambo yanayosemwa sana katika maandiko: - Isa. 45: 5 -7; Mika. 1: 12; Amosi. 3: 6; Kutoka. 4: 11; K/torat. 32: 39; Ayubu. 5: 18. Yote haya yatoa faida kwa kusoma vema. Kinachofuata ni kwamba ni yeye ambaye tumgeukie kwa maombi kama tukiwa wagonjwa, tukifanya yote ambayo ni ya jinsi ya mwanadamu inapowezekana kwa kutumia dawa zinazokubalika na nchi ili kurekebisha tatizo lakini sio kwenda kwa waganga wa kichawi. Kama tukifuata waganga wa kienyeji, tujue twafuata watu ambao wanadai wana 'nguvu za giza’ ambazo zinawawezesha kutufanya tupone. Lakini tunajua ya kwamba hizo nguvu wanaamini kuzitenda hazipo. Mungu ndiye muasisi wa nguvu. Kuwaendea wachawi ni kuamini kwamba Mungu hana nguvu zote, na kwamba siye Mungu anayeleta magonjwa yetu bali nguvu ambazo wachawi hudai wanazivuta.

Kufikiri kama hivyo ni kutompendeza Mungu kabisa, kwa kuwa anajua ya kuwa ameuleta ugonjwa, na ni mwenye uweza wote. Israeli walichagua kumwamini Mungu lakini pia waliamini kwamba zipo nguvu zingine zinzotenda kazi katika maisha yao, ambazo iliwabidi washughulike nazo kwa kuzitumikia na sanamu zilizoundwa na nguvu hizo. Jambo hili lilimkasirisha sana Mungu hata akawaacha kuwa watu wake (K/Torati. 32:16 - 24) kwa Mungu tusipomwamini kikamilifu, kwa kweli tujue hatumwamini kabisa. Kadhia ya kusadiki kwa Mungu wa kweli wa Israeli na wakati huo huo kuwa na wazo la kuwepo kwa nguvu zilizojitenga na Mungu, na kuruhusu mganga wa kienyeji ajaribu kuvuta hizo nguvu zituache kutenda kosa kabisa kama Israeli walivyofanya zamani. Historia ya muda mrefu ya kuhuzunisha ya Israeli ya kuzitumikia sanamu "imeandikwa ili tujifunze"(Rum. 15: 4). Tusishirikiane kabisa na hao waaminio nguvu hizi.

"Pana shirika gani kati ya nuru na giza ?. Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu ?. Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliyehai …. Kwa hiyo tokeni kati yao mkatengwe nao , asema Bwana …….nitakuwa Baba kwenu nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike"(2 Kor 6:14 -17).

Kama kweli tunafanya bidii na kujitoa kwa kujitenga toka mambo haya, basi tuna amana yenye utukufu na ya kuwa tu wana wa Mungu mwenyewe. Mzazi wa mwili kwa moyo anamtunza mtoto wake anapoumwa. Je ! ni shida kweli kukusanya imani yetu kwa kumwamini kwamba Baba yetu aliye mbinguni atafanya hivyo hata zaidi ?.

Ukweli ni kwamba uchawi una mvuto tu juu yao wanaoamini. Kwa jinsi hii mtu aliyempoteza mpenzi wake anaweza kwenda kwa mtu anaye dhaniwa kuongea na wafu na kwa mchawi na kutaka kumwona mtu aliye kufa. Huyo mtu atawaambia wafumbe macho yao na wakumbuke sura ya mtu wazi wazi kabisa. Mtu atakaye shauri anaweza kukaza nia yake juu ya picha ya mtu anaweza kumkumbuka bayana. Huyu mwenye kudhaniwa kuongea na roho za watu basi anaweza kusoma nia ya mwenye shida, na kwa kupiga chuku kidogo ananena kuhusu mtu kwa maneno anavyoonekana,Hivyo basi mtu anayetaka shauri anaamini kwamba mlozi amemuona mtu aliyekufa angali hai. ujue kwamba hakuna ushahidi kamili umewahi kutolewa wa kuwa mtu yu hai. Lakini mtaka shauri au mpigiwa ramri akikataa kuamini au kumtii huyu mwaguzi basi hakuna kinachotokea kabisa.

‘Wachawi ambao kwa kawaida walimwambia Farao na Nebukadneza ndoto zao wangefanikiwa na nafasi zao za madaraka ila wangefaulu kwa haki. Bila shaka walitumia ujanja huu wa kusoma akili kwa wingi. Lakini Mungu anajihusisha katika maisha ya mtu aliyejishughulisha naye, kama alivyoingilia katika maisha ya Farao na Nebukadneza, walipoteza nguvu zao wakati ule. Vivyo hivyo Baraki aliamini uwezo wa Balaamu wa kuwalaani watu - alipamatia zawadi kubwa ya fedha kwa huduma yake, huku akisema najua tangu zamani alivyopata kukuona "yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa"(Hesabu. 22: 6). Lakini Balaamu ambaye alikuwa kwa namna nyingine ni sawa na mganga wa kuagua, alikuta kwamba uwezo wake wa kawaida ulitoka alipokuwa anajishughulisha na watu wa Israeli. Ni bayana, watu hawa hawana nguvu kabisa wanapojishughulisha na watu ambao wameungana na Mungu wa kweli, Wowote umashuhuri unaweza kujipatia kwa kufanikiwa unapojihusisha na watu wengine.

UCHAWI KATIKA BIBLIA

Maana ya kufaa ni kwamba kama tunajaribu kwenda kwa mganga wa kienyeji, basi tumwamini kabisa. Hakuna maana ya kuaguliwa na mchawi kama tunatumainia mema; na huenda wao wenyewe watafanya hayo hayo. Kuamini kabisa watu hawa na kuwepo kwa nguvu wanazodai wanamiliki, maana yake hatumwamini Mungu mwenye nguvu zote wa kweli. Kama kweli tunaamini taarifa za Farao, Nebukadneza na Balaki waliotajwa, ndipo na sisi tutakwenda kwa mpiga ramli na imani kwamba watakuwa na matokeo yoyote juu yetu . Mifano tuliyoiona yaonyesha kwamba uchawi hauna nguvu juu ya watu wa Mungu - tunajua ndivyo tulivyo, kwa sababu ya kuitwa kwetu na kubatizwa.

Uchawi ni bayana umeelezewa na Paulo kuwa ni "Matendo ya mwili", na kwa jinsi hiyo hata'uzushi’ (mafundisho ya uongo), Uzinzi / uasherati na uchafu (Gal. 5: 19 -21). Anafafanua: "Nawaambia mapema kama nilivyokwisha kuwaambia (yaani haya yalitiliwa msisitizo katika mafundisho ya Paulo), Ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo, yakufanana na hayo hawataurithi ufalme wa Mungu"Uwiano wa hili chini ya sheri ya Musa, amri ilikuwa kwamba wachawi wote, wote wanaoagua au kupiga ramli (jina lingine la Uchawi) na hao waliopitisha watoto wao chini ya moto waliuliwa mara moja (K/torati. 18: 10,11; Kut. 22: 18). Waliopitisha watoto wao motoni hawakuwa ni wachawi hasa - Wachawi na viongozi wa Ibada ya sanamu walifundisha kwamba ili kujilinda dhidi ya nguvu za uovu, watotot wa hao waliotaka ulinzi waliwapitisha katika moto. Basi tunaona kwamba wote wachawi na hao walioutumia waliuwawa; na kwenye Agano Jipya adhabu kwa wafanyayo hayo ni kutoingia ufalme wa Mungu.

Kutumia uchawi kuwa ndio njia yako nzuri kuboresha maisha ni jambo lingine ambalo Mungu hapendi sisi kufanya kwa kila uamuzi tunakabiliwa na maisha yetu kwa Kristo, inatubidi kwa kusema kweli tujiulize 'Je ! kweli Mungu anataka mimi nifanye hivi ?. Je ! nifanye hivi huku Yesu akiwa karibu yangu ? kwa mtazamo wa hukumu ya Mungu bayana kwa uchawi, nadhani jawabu liwe dhahiri ipasavyo - hapana, Mungu hataki tutumie uchawi umebainishwa na Samweli ni kuhusika na 'uasi’ (Kiebrania kinadokeza'kukasirisha’) juu ya neno la Mungu (1 Sam. 15: 23). Kumkasirisha mwenyezi kama Israeli walivyofanya kuamini sanamu na uchawai (K/Torati 32: 16 -19), ni hakika hakuwazika. Mungu ana maana kwa kuwaamuru Israeli kwa kuwafukuza Wakanaani watoke kwa sababu ya kuamini uchawi ambao ulikuwa chukizo mno kwake, lakini badala yake, walijiunga kutenda hayo (K/Torati 18: 9-14).Basi kwa Israeli wapya, waamini waliobatizwa, haitupasi kutenda mambo haya ya ulimwengu mbaya uliotuzunguka, au la sivyo hatutaweza kurithi milele nchi ya ufalme tuliyoahidiwa. Kutoa sababu kwamba ni uchawi pekee unaotumika, sio sisi, sio jambo lenyewe, kama tunatumaini kwamba matokeo ya uchawi yataonekana kwetu, basi kwa kushitusha tuna utumia.

Mungu atubariki sote tunapotembea kwa kufunga siku za giza, ulimwengu wa watu na mataifa kuelekea ufalme wake wenye nuru ya kweli na utukufu.

"Kwa sababu hawakubali kuipenda hiyo kweli, wapate kuokolewa kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, Wauaminio uongo; …… Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana ……Basi ndugu simameni imara mkashike mapokeo mliofundishwa ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu. Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema" (2 Thes. 2: 10 -17).


  Back
Home
Next