Misingi Ya BIBLIA
Somo La 6: Mungu Na Ubaya
Mungu Na Ubaya | Ibilisi Na Shetani | Mapepo - Mashetani | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Uchawi, Edeni palitokea nini?, Lusifa, Majaribu ya Yesu, Vita Mbinguni) | Maswali

6.2 Ibilisi Na Shetani

Mara nyingi maneno ya asili ya aya za Biblia yameachwa bila tafsiri. Neno'Shetani’ ni neno la Lugha ya Kiebrania ambalo halijabadilishwa, nalo lina maana'adui’ wakati 'Ibilisi’ - devil ni badiliko la lugha ya Kiyunani - Kigriki 'diabolos’, maana yake mwongo, adui au mshitaki. Kama tunaamini ya kwamba shetani na Ibilisi ni kiumbe mwingine aliye nje yetu mwenye kuhusika na dhambi, basi popote atakapotoka upande mmoja hadi mwingine wa maneno haya katika Biblia, yatupasa tuyafanye kumtaja mtu huyu mbaya. Matumizi ya Biblia kwa maneno haya yanaonyesha kuwa yaweza kutumika kama neno linalotaja sifa za kawaida, za kusimulia watu wa kawaida. Ukweli huu unafanya isiwezekane kudhani kwamba Ibilisi na shetani kama yalivyotumika ndani ya Biblia yafanya yenyewe kumtaja mtu mkuu mbaya au kiumbe kilicho nje yetu.

NENO 'SHETANI’ KATIKA BIBLIA

1 Wafalme 11: 14 imetolewa taarifa ya kwamba "Bwana akamwondokeshea - yaani, aliamsha adui wa Suleimani (neno lile lile la Kiebrania kila mahali limetafsiriwa"Shetani"), Hadadi Mwedomi"."Tena, Mungu akamwondokeshea adui mwingine (Shetani mwingine), Rezoni ….. naye akawa adui (shetani) wa Israeli" (1 Wafal. 11: 23, 25). Hapa haina maana kwamba Mungu aliamsha mtu asiye wa kawaida au Malaika ili awe shetani / adui wa Suleimani; aliwaamsha watu wa kawaida. Math. 16: 22,23 inatoa mfano mwingine. Petro alikuwa anajaribu kumzuia Yesu toka kwenda Yerusalemu kufa msalabani. Yesu aligeuka na kumwambia Petro"Nenda nyuma yangu, shetani ….. huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu". Hivyo Petro aliitwa shetani. Habari ipo wazi kwa kuonekana ya kwamba Kristo alikuwa haongelei Malaika au mtu mbaya sana alipotamka maneno hayo; alikuwa akimsema Petro.

Kwa sababu neno 'Shetani’ lina maana tu adui, mtu mwema, hata Mungu mwenyewe, anawezakuitwa 'shetani’. katika maana hakuna lazima kuwa na dhambi kuhusiana na neno lenyewe. ukubwa wa maana ya dhambi ambalo neno'shetani’ linao kwa sehemu ni kwa ajili ya ukweli kwamba mwili wetu wenyewe ulio na dhambi ni 'shetani’ wetu mkubwa au adui, na kwa sababu pia ya matumizi ya neno katika semi za ulimwengu hutajwa kitu kingine kinachokuwa pamoja na dhambi. Mungu mwenyewe aweza kuwa shetani kwetu kwa njia ya kuleta mitihani katika maisha yetu, au kwa kuchukua hatua kutokana na mwendo mbaya wa matendo tunayoweza kuingia.Lakini ukweli ni kuwa Mungu anaweza kuitwa 'shetani’ haina maana ya kuwa yeye mwenyewe ni mtenda dhambi.

Kitabu cha Samweli na mambo ya Nyakati vina maelezo sambamba yenye matukio aina moja, kama taarifa za Injili zina matukio yale yale lakini zinatumia misemo tofauti. 2 Sam. 24: 1 pameandikwa:"Tena …. Bwana akamtia nia Daudi juu yao - Israeli" ili afanye sensa ya Israeli. Maelezo yaliyo sambamba katika 1 M / Nyakati 21: 1 unasema kwamba"Tena shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli" Katika fungu moja la maneno Mungu anashawishi, lingine shetani anafanya hivyo. Neno la mwisho ni kwamba Mungu alisimama akiwa 'Shetani’ adui wa Daudi. Alifanya hivyo hivyo kwa Ayubu kwa kumletea majaribu katika maisha yake, hivyo basi Ayubu alisema kuhusu Mungu:'Umegeuka kuwa mkatili kwangu yaani 'shetani’, wanitesa kwa mkono wako wenye nguvu"kimsingi ndivyo asemavyo Ayubu (Ayubu. 30: 21 B. H. N).

NENO 'IBILISI’ KATIKA BIBLIA

Hivyo hata neno 'Ibilisi’ vile vile. Yesu akasema, "Sikuwachagueni ninyi kumi na mbili (wanafunzi), na mmoja wenu siye ibilisi ?" Alisema Yuda Iskarioti aliyekuwa mtu wa kawaida. Hakuwa anazungumzia kiumbe binafsi aliye na pembe, au aitwaye 'roho’. Neno 'Ibilisi’ hapa anatajwa tu binadamu muovu. 1 Tim. 3: 11 tumepewa mfano mwingine. Wake wa wazee (Mashemasi) wa kanisa hawatakiwi kuwa 'wasingiziaji’; neno la asili la Kigriki hapa ni 'diabolos’ ambalo lina maana moja na 'Ibilisi’ kila mahali katika Biblia. Paulo alimuasa Tito ya kuwa wanawake wazee katika eklezia wasiwe "wachongezi" au'mashetani’ (Tito. 2:3 - B.H.N). Na hivyo hivyo alimwambia Timotheo (2 Tim. 3: 1,3) kuwa "Siku za mwisho …. Watu watakuwa …. Wasingiziaji (Mashetani)". Hii haina maana kuwa watu hawatakuwa watu wa kawaida, bali wataongezeka na kuwa waovu mno. Inabidi yawe wazi kabisa tokana na haya maneno 'Ibilisi’ na 'shetani’ kutotaja Malaika aliyeanguka toka juu au kiumbe mwenye dhambi nje yetu.

DHAMBI, SHETANI NA IBILISI

Maneno 'Shetani’ na'Ibilisi’ hutumika kwa mfano kusimlia maelekeo ya asili yenye dhambi yaliyo ndani yetu tuliyo yasoma katika somo la 6.1. Haya ndiyo 'shetani’ wetu mkuu au adui. Pia yamesemwa kana kwamba ni mtu, na kama hivi, yaweza kusemwa kama'Ibilisi’ - au adui yetu, msingiziaji kweli. Hivi ndivyo ulivyo 'utu’ wetu wa asili - Ibilisi kabisa. Muungano kati ya Ibilisi na nia zetu mbaya - dhambi ndani yetu - vimewekwa wazi kwenye mafungu kadhaa ya maneno: "Basi, kwa kuwa watoto (sisi wenyewe) wameshiriki mwili na damu, yeye (Yesu) naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo; ili kwa njia ya mauti (yake) amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, 'Ibilisi’ (Ebra. 2: 14). Hapa Ibilisi amesemwa ndiye anayehusika na mauti. Lakini "mshahara wa dhambi ni mauti (Rum. 6:23). Basi, dhambi na Ibilisi inabidi wawe sawa. Yakobo 1: 14 kama hivi anasema kwamba nia zetu mbaya hutujaribu, na kutuongoza kutenda dhambi na hivyo kupata kifo. Mstari huo huo unasema kuwa Yesu alikuwa na mwili wetu ili amharibu Ibilisi. Kutofautiana na, Rum. 8: 3; "Mungu kwa kumtuma mwanae mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi (mwili wetu wanadamu), na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili. Hii inaonyesha kuwa Ibilisi na maelekeo mabaya ya dhambi ambayo kwa kawaida yamo ndani ya mwili wa mwanadamu kwa maana ni mamoja. Ni lazima na muhimu kufahamu kwamba Yesu alijaribiwa kama sisi.

Kutokufahamu vema mafunzo ya Ibilisi maana yake ni kwamba kwa usahihi hatuwezi kuelewa mwili na kazi ya Yesu. Ilikuwa ni kwa sababu tu Yesu alikuwa na mwili wa mwanadamu - Ibilisi ndani yake - hata tumeweza kuwa na tumaini la wokovu (Ebra. 2: 14 -18; 4: 15). Kwa kuzishinda nia za mwili wake mwenyewe, Ibilisi wa Biblia, Yesu aliweza kumharibu Ibilisi juu ya msalaba Ebra. 9:26 unasema kuwa Kristo alifunuliwa "azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake" Ebra. 2:14 unalingana na taarifa ya kuwa Kristo kwa kifo chake amemharibu Ibilisi ndani yake mwenyewe. Kwa kufa kwake Yesu kwa matazamio aliuharibu "mwili ulio wa dhambi"(Rum. 6:6), yaani, mwili wa mwanadamu, dhambi ilifunuliwa katika (umbo la) miili yetu kabisa.

"Atendaye dhambi ni wa Ibilisi" (1 Yoh. 3:8), Kwa sababu dhambi hutoa ruhusa kwa mawazo yetu ya asili (Yak. 1: 14, 15), kile ambacho Biblia inaita' Ibilisi’."Kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za Ibilisi ni nia zetu, (1 Yoh. 3:8). Kama tupo sahihi kwa kusema kwamba ibilisi ni nia zetu, basi kazi za nia zetu mbaya, yaani, zinazoleta dhambi, tunazo wenyewe. Hizi zimethibitishwa na 1 Yoh. 3:5."Yeye (Yesu) alidhihirishwa ili aziondoe dhambi zetu" Huu unathibitisha kwamba "dhambi zetu" na "kazi za Ibilisi"ni moja. Matendo. 5: 3 huu unatupatia mfano mwingine wa muungano huu kati ya Ibilisi na dhambi zetu. Petro akamwambia Anania:"Kwa nini shetani amekujaza moyo wako ?". Kuwaza jambo fulani baya mioyoni mwetu ni sawa sawa na shetani amejaa mioyoni mwetu. Kama sisi wenyewe tuna jambo baya, k.m. mpango wa dhambi, basi unaanza ndani yetu. Ikiwa mwanamke anazaa watoto, hakai nje yake; mtoto anatoka ndani ya tumbo. Yakobo. 1: 14, 15 anatumia mfano huu kwa kuelezea jinsi tamaa inavyozaa dhambi, ambayo inaleta mauti. Zab. 109: 6 unasawazisha mtu mwenye dhambi na'shetani’; "Uweke mtu mbaya (mkorofi) juu yake: Shetani asimame mkono wake wa kuume"yaani kwa nguvu juu yake (Zab. 110: 1).

KUTAJA KITU KANA KWAMBA NI MTU

Ingawa hivyo, kwa haki unaweza kujibu: 'Lakini anasema ibilisi kama mtu !’. Ni kweli kabisa; Ebra. 2: 14 amesemwa "Yeye aliye na nguvu za mauti, yaani, ibilisi". Hata kiasi kidogo cha usomaji wa Biblia chaonyesha kuwa mara nyingi kutaja kitu kama mtu Biblia inatumia sana - kuzungumzia jambo la kuwazika tu kana kwamba ni mtu. Hivyo Mithali 9: 1 hekima anaonekana kama vile ni mtu ameijenga nyumba, na Rum. 6:23 dhambi imelinganisha na Bwana mwenye malipo atoaye mshahara wa mauti. Jambo hili limejadiliwa tena katika kuacha kitambo kilichokuwa kimeandikwa sehemu ya 5. Ibilisi wetu, 'diabolos’ mara kwa mara maana yake ni mawazo yetu mabaya.

Hata hivyo huwezi kuwa na Ibilisi wa kuwazika tu; mawazo mabaya ambayo yamo ndani ya moyo wa mtu hayawezi kuwepo kwa kujitenga na mtu; kwa hiyo 'Ibilisi’ ametajwa kama vile ni mtu. Mara nyingi dhambi imetajwa kama mtu ambaye ni Bwana (k.m. Rum. 5:21; 6:6, 17; 7:3). Kwa hiyo inaeleweka kuwa'Ibilisi’ pia ametajwa kama kiumbe, kwa kuwa vile vile'Ibilisi’ inatajwa dhambi. Kwa njia h iyo hiyo, Paulo anasema sisi tuna watu wawili, kama alivyokuwa ndani ya mwili wetu (Rum. 7:5 -12): Utu na mwili,'Ibilisi’ anapingana na utu wa Rohoni. Lakini ni wazi hawapo viumbe binafsi wawili wanaopingana ndani yetu. Hii sehemu ya mwili wetu ulio na dhambi imeitwa kama ni mtu "yule mwovu"(Math. 6:13) - Ibilisi wa Biblia. Fungu hilo hilo la maneno katika sentensi ya Kiyunani limetafsiriwa "yule mwovu"kwa usemi wetu limetafsiriwa "yule mbaya"katika 1 Kor. 5:13, yaonyesha kwamba mtu anaporuhusu dhambi, 'yule mwovu’ wake yeye mwenyewe - anakuwa ni 'yule mwovu"au 'Ibilisi’.

‘IBILISI’ NA 'SHETANI KATIKA MANENO YA - TAWALA

Maneno haya 'ibilisi’ na 'shetani’ vile vile yametumika kuelezea uovu, mpangilio wa ulimwengu wenye dhambi tunamoishi. Kijamii, Kisiasa na muungano wa daraja za mamlaka toka chini hadi juu kwa walimwengu wenye dini za uwongo zaweza kuitwa'Ibilisi’ kwa maneno. Ibilisi na shetani katika Agano Jipya mara nyingi zinatajwa tawala na nguvu za jamii ya Wayahudi au utaratibu wa Waroma. Tunasoma hivi Ibilisi akiwatupa baadhi ya waaminio gerezani (Uf. 2:10), yatajwa mamlaka ya Waroma ikiwafunga waaminio. Katika maneno haya haya tunasoma habari ya kanisa lililokuwa Pergamo ni kwenye kiti cha shetani, au kiti cha enzi, kilikuwa - yaani mahali pa utawala wa koloni katika Pergamo, Kundi la waaminio. Hatuwezi kusoma shetani mwenyewe, kama yupo anaishi, binafsi alikuwa na kiti cha enzi Pergamo.

Dhambi ya mtu mmoja mmoja imefafanuliwa kuwa ni kuvunja amri za Mungu (1 Yoh. 3:4). Bali dhambi ikielezwa kwa pamoja kama kisiasa na nguvu ya jamii vikipingana na Mungu ni nguvu yenye uwezo mkubwa kuliko mtu mmoja - mmoja; ni hii nguvu ya pamoja inayoitwa mara nyingine kama vile ni mtu mwenye uwezo mkubwa anayeitwa Ibilisi. Kwa maana hii Irani na mamlaka zingine za Kiislamu zimeita Amerika ni "Shetani mkubwa"- yaani, adui mkubwa kwa lengo lao, Kisiasa na maneno ya dini. Hivi ndivyo maneno 'Ibilisi’ na'Shetani’ mara nyingi yalivyotumika katika Biblia.

Kwa kumalizia, labda ni kweli kusema kuwa katika jambo hili tunalosema zaidi ya lingine lolote, ni muhimu kuweka fahamu zetu juu ya mtazamo uliowiana wa Biblia nzima, kuliko kujenga mafundisho makubwa kwa mistari michache iliyo na maneno yaliyovuma yanaonekana kutaja imani ya kawaida kuhusu Ibilisi.Somo la 6.1 na sehemu hii kwa makini yanalipa, kwa kuomba kusoma tena. Nafasi ya mafunzo iliyowekwa imeelezea njia pekee ya kuweza kufahamu vema mafungu yote ya maneno yanayotaja vema ibilisi na shetani. Maneno hayo yaweza kutumika kama ni yenye sifa za kawaida, au katika maneno mengine yanataja dhambi ambayo inapatikana ndani ya mwili wake mwanadamu. Baadhi ya mafungu ya maneno ambayo kwa upana zaidi hayaeleweki yaliyonukuliwa kwa kusaidia mawazo ya watu wengi yamepimwa katika sehemu tunayoacha kilichokuwa kinaandikwa inayofuatana na somo hili.

Walio na matatizo ya kukubali maneno yetu wanatakiwa wajiulize wenyewe: (1) Je ! dhambi imeitwa kama vile mtu ?. Ni wazi. (2) Je ! ni kweli kwamba 'shetani’ aweza kutumika kama maneno ya sifa ? Ndiyo. Ni tatizo gani basi, laweza kukubalika kwamba dhambi imeitwa kama mtu kama adui yetu / shetani ?. Ulimwengu mara nyingi umeitwa kama mtu katika nyaraka za Yohana na Injili; ni jina gani bora litumiwe kuliko 'shetani’ au'Ibilisi’ kwa mtindo huu wa kuita kama mtu ?.


  Back
Home
Next