Misingi Ya BIBLIA
Somo La 11: Maisha Katika Kristo
Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali

11.3.5 Uhai Wa Iklezia

Pamoja na kusali, kusoma Biblia, desturi ya kutii amri ya Kristo ya kumega mkate na kunywa divai kwa kukumbuka dhabihu yake ni muhimu. " Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu" Yesu aliagiza (Luka 22:19). Ilikuwa ni nia yake kuwa wafuasi wake watafanya hivi mara kwa mara hata ajapo mara ya pili, Yesu atakaposhiriki mkate na kunywa divai pamoja nao (1 kor. 11:26; Luka 22:16-18).

Mkate ni mfano wa mwili wa Kristo uliotolewa msalabani, na divai ni damu yake (1 Kor 11:23-27). Waumini wa kwanza wanaonekana walishika ibada hii mara nyingi (Mdo. 2:42,46), mara moja kwa wiki (Mdo. 20:7). Kama kweli tunampenda Kristo, tutatii maagizo yake (Yoh.15:11-14). Ikiwa tuna uhusiano wa kweli naye, itakuwapo haja ya kukumbuka dhabihu yake kama alivyotaka, na kwa sababu hiyo tutajitia nguvu wenyewe sisi kwenye wokovu aliotimiza kwa ajili yetu. Kipindi cha kutulia wakati wa kuwaza juu ya mateso yake msalabani kitafanya majaribu yetu wenyewe yafifie na kuwa hayana maana yanapolinganishwa na hayo ya Bwana wetu.

Kimsingi kumega mkate ni ibada ya ukumbusho, hakuna muujiza unaotokea kwa matokeo ya kuifanya hii ibada. Ni sawa sawa na Pasaka iliyofanywa chini ya Torati ya Musa (Lk 22:15; 1 Kor 5:7,8). Hii ilikuwa ni njia ya kukumbuka wokovu mkuu wa kutoka Misri ambao Mungu aliutenda kwa mkono wa Musa penye Bahari ya Shamu. Ibada ya kumega mkate inatukumbusha wokovu kutoka katika dhambi kwa njia ya Kristo, ambao umefanikishwa msalabani na uliotuunganisha na Ubatizo. Basi kushika amri hii kwa kawaida iwe ni desturi kufanya ukumbusho.

Kutwaa mkate na divai, kimwili kunafanya upendo wa Kristo kwetu na kwa kweli mambo yote yanayohusu wokovu wetu, huja vivi hivi kuwa ya kweli mara nyingine tena. Kumega mkate kwa karibu mara moja kwa juma basi ni dalili ya kuwa na hali ya afya kiroho. Ikiwa mtu hawezi kuhudhuria ibada hii na waumini ndugu wa Kweli, ifanywe hata akiwa pekee yake. Hakuna udhuru unaoruhusiwa kutuzuia kutunza/ kutimiza amri hii. Tufanye kila jitihada kuwa na mkate na divai kwa ajili ya ibada, ingawa katika mambo mbalimbali hata vikikosekana vitu hivi hatutazuiwa toka kumkumbuka Kristo kwa njia iliyowekwa kwa kadri tuwezavyo. Yesu alitumia "tunda la mzabibu" (Luka 22:18), basi nasi tutumie divai ya zabibu nyekundu.

Kuchukua vitu ambavyo ni mfano wa mateso ya Kristo na dhabihu ni heshima ya juu zaidi ambayo mwanamme au mwanamke aweza kuwa nayo. Kuvishiriki isivyostahili kwa namna inavyoonyesha ni sawa na kukufuru, kwa "maana kila mlapo mkate huu na kukinywea kikombe mwaitangaza mauti ya Bwana….. kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana" (! Kor 11:26,27). Ibada ya kumega mkate kwa sababu hii itafanywa wakati na mahali ambapo hapata kuwapo na kuvutwa mawazo kwenda pengine na kudakizwa na mtiririko wa mawazo ya mtu. Hii yaweza kufanywa mapema asubuhi au mchana ukishapita, ndani chumbani au mahali pengine panapofaa. Tunashauriwa zaidi,

" Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo (katika hiyo roho ya unyenyekevu ya kujipima nafsi) aule mkate, na kukinywea kikombe", (1 Kor 11:28). Kwa hiyo tutaweka mioyo yetu juu ya dhabihu ya Kristo, labda kwa kutazama taarifa za Injili kuhusu kusulubiwa kwake, kabla ya kutwaa mifano. Kwa kufanya hivyo vema, bila kuepuka tutajihoji dhamiri zetu wenyewe kumweleke Kristo, zaidi.

Kanuni inayofaa kwa ibada ya kumega mkate ni kama ifuatavyo:-

  1. Sala - ya kumuomba Mungu abariki mkutano: Afumbue macho yetu kuelekea Neno lake; kukumbuka mahitaji ya waumini wengune; kumtukuza kwa upendo wake, hasa ulioonyeshwa kwa Kristo, na kuomba kwa habari za matokeo mengine dhahiri.
  2. Kusoma masomo ya Biblia kwa siku kama yalivyotajwa katika "Mwenzi wa Biblia"
  3. Kutafakari juu ya masomo ya kufundisha, kusoma ‘Maonyo’- kujifunza Biblia juu ya sura hizo zinazotuongoza kuelekea kwenye lengo la ibada yetu - ukumbusho wa Kristo.
  4. Somo 1 Kor 11:23-29
  5. Kipindi cha kukaa kimya cha kujihoji mwenyewe
  6. Sala kwa ajili ya mkate
  7. Mega mkate, kula kipande chake kidogo.
  8. Sala kwa ajili ya divai
  9. Kunywa tone la divai
  10. Sala ya kumalizia

Ibada nzima ichukue saa moja tu.


  Back
Home
Next