Misingi Ya BIBLIA
Somo La 11: Maisha Katika Kristo
Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali

11.2.1 Matumizi Ya Nguvu

Tunaishi katika ulimwengu wenye kutawaliwa na dhambi. Tuliona katika sehemu 6.1 ya kwamba serikali ya wanadamu zinaweza kuitwa ‘Ibilisi’ kwa kuwa zimetengezwa kuzunguka pande zote matakwa ya mwili, ‘Ibilisi’ wa Biblia.

Ujumbe wa Biblia uliorudiwa ni kwamba, kwa kifupi, dhambi na uzao wa Nyoka utaonekana kuwa na Ushindi, ambapo baada ya mateso ya kitambo kidogo kwa namna mbalimbali, uzao wa mwanamke hatima yake utahesabiwa kuwa na haki. Kwa sababu hii mwamini ameamriwa daima "Kutoshindana na uovu" (Math 5:39; Rum 12!&; 1Thes 5:15; 1 Petro 3:9).

Tumeona kwamba ubaya mwishoni umeruhusiwa na kuletwa na Mungu (Isaya 45:7; Amosi 3:6 linganisha Somo la 6.1). Kwa kutumika ili kushindana na uovu basi ni kupingana na Mungu. Kwa sababu hii Yesu aliamuru ya kuwa sisi kimwili tusishindane na nguvu ya uovu: "lakini akupigayeshavu la kuume mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki, na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia" (Mathayo 5:39,40). Kwa jambo hili Kristo ni mfano "Naliwatolea wapigao mgongo wangu…." (Isaya 50:6).

Maneno ya Kristo yanaunga pamoja atakaye kukushitaki na shughuli za ulimwengu zinapopingana na aaminiye. Kufanya hivi ni mfano mkubwa wa kupinga uovu, nao hautafanywa na awaye yote aliye na imani thabiti katika ahadi ya Mungu ya kwamba "Kisasi ni juu yangu; mimi nitalipa anena Bwana" (Rum 12:19). "Usiseme, mimi nitalipa mabaya; Mngojee Bwana, naye atakuokoa" (Mithali 20:22 linganisha Kum 32:35). Kwa sababu hii Paulo aliwakaripia wazi Wakoritho kwa kuwapeleka wengine kwenye sheria (1 Kor 6:1-7).

Kwa mtazamo wa ukuu wa tumaini letu, hatutajihusisha sana na maisha ya sasa yasiyo na haki: "Je! mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio na haki …… Au hamjui ya kwamba watakatifu watahukumu ulimwengu?" (1 Kor 6:1,2). Kuwapeleka wengine kuwashitaki, ikiwa ni kugombea kiwanja au mambo ya talaka, basi liwe ni tendo lisilokuja akilini kwa mwamini wa kweli.

Ili kukomesha nguvu za ubaya, sawa sawa (katika masuala mengine) kwa kuweka watu wabaya katika uweza, jeshi na nguvu za polisi zinatumika na serikali za wanadamu. Hizi ni desturi zilizowekwa kupinga uovu, kwa hiyo mwamini wa kweli asizishiriki hizo. "Wote washikao upanga, wataangamia kwa huo upanga (Math 26:52). Hili ni jambo la Mungu la awali kabisa linalorudia "Atakayemwaga damu ya mwanadamu (kwa kusudi), damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu: maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu" (Mwanzo 9:6). Jeuri yoyote ya makusudi juu ya ndugu yetu mwanadamu ni kumfanyia jeuri Mungu, ila akiruhusu.

Chini ya utumishi wa Kristo, tumeambiwa, "Wapendeni adui zenu, waoombeeni wanaowaudhi, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi" (Math 5:44; Lk 6:27). Nguvu za kijeshi na Polisi zinashughulika na kupingana moja kwa moja na mambo haya na kwa hiyo mwamini wa kweli atajiepusha yote kujiunga nao. Hata kama si moja kwa moja kuhusika katika kutenda jeuri, kufanya kazi katika Taasisi hizi au kujihusisha katika ajira zilizoungana nazo, ni dhahiri haushauriwi; hakika, ajira yeyote inayofuatana na kutoa kiapo cha kutii mamlaka hizi, hutuondolea uhuru wa dhamiri ya kutii amri za mwenyezi Mungu. Waamini wa kweli basi siku zote ni wenye bidii kufanya vyema yote yapasayo kukataa shughuli za jeshi na kutumikia Polisi kwa namna yeyote , ingawa siku zote wanapenda kutumia ajira ya hiari katika nyakati shida za taifa ambazo zitawafaidisha kupata vitu ndugu zao wanadamu.


  Back
Home
Next