Misingi Ya BIBLIA
Somo La 11: Maisha Katika Kristo
Dibaji | Utakatifu | Matumizi Ya Nguvu | Siasa | Anasa Za Ulimwengu | Maisha ya kikristo yenye Matendo | Kujifunza Biblia | Sala | Kuhubiri | Uhai Wa Iklezia | Kumega Mkate | Ndoa | Maswali

11.3.2 Kujifunza Biblia

Mazoezi mengine muhimu kukuza ni hayo ya sala. Tukiisha kumbushwa ya kwamba yupo "mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, mwanadamu Kristo Yesu; aliyejitoa mwenyewe kuwa fidia kwa wote" Paulo anaagiza sana kwa kina kufahamu kazi ya Kristo: "Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali…… pasipo hasira wala majadiliano" (1 Tim 2:5-8). "Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuliana nasi katika mambo yetu ya udhaifu, bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi natukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji" (Ebr 4:15,16).

Tukifahamu ukweli wa kwamba Kristo ni kuhani mkuu wetu wenyewe wa kutoa maombi yetu yenye nguvu mbele za Mungu, huu unatuvuvia kwa desturi kuomba kwa imani. Ingawa hivyo, ombi lisiwe tu na ‘orodha ya mahitaji’ ya kumpa Mungu; kutoa shukrani kwa ajili ya chakula kabla ya milo, kwa ajili ya kulindwa safarini n.k haya yatafanywa kuwa sehemu muhimu ya maombi yetu.

Kuweka shida zetu mbele za Bwana katika sala iwe ndani yake yenyewe, inatoa maana kubwa ya amani: "Katika kila neno (hakuna lilo dogo mno kuombea) kwa kusali…. na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu" (Wafilip 4:6,7).

Ikiwa maombi yetu yanakuwa sawa na mapenzi ya Mungu, hakika kweli yatajibiwa (1 Yoh 5:14). Tunaweza kujua nia ya Mungu tunapojifunza kwa kusoma Neno lake, linalofunua Roho/nia yake kwetu. Kwa hiyo somo letu la Biblia litufundishe sehemu mbili, jinsi ya kuomba na jambo gani liombewe, yafanywe hivi maombi yetu ya nguvu. Basi "…. Maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa" (Yoh 15:7). Kuna mifano mingi ya kuomba sawa sawa katika maandiko (Zab 119:164; Dan 6:10). Asubuhi na jioni, kwa maombi machache mafupi ya kutoa shukrani wakati wa mchana yataonekana kama yanafunua kidogo sana.


  Back
Home
Next