Misingi Ya BIBLIA
Somo La 7: Mwanzo wa Yesu
Unabii unaomhusu Yesu kwenye Agano la Kale | Kuzaliwa na Bikira | Nafasi ya Kristo katika mpango wa Mungu | "Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno" (Yohana 1:1-3) | Tumeacha Kitambo sehemu ya (Yesu wa Historia, Nimeshuka kutoka Mbinguni, Je? Yesu aliumba Dunia, "Kabla ya Ibrahimu, Nalikuwepo" (Yn. 8:58), Melkizedeki) | Maswali

7.2 Kuzaliwa na Bikira

Habari iliyoandikwa ya mtungo wa mimba na kuzaliwa hairuhusu shauri la kwamba aliishi kwa mwili kabla ya kuzaliwa. Hao wanaoshika mafundisho ya uongo ambayo ni'Utatu’ wanapelekwa kwenye dhana ya kwamba wakati fulani walikuwa watu watatu mbinguni, kisha mmoja wao alitoweka na kwa njia nyingine alibadilika kuwa kitoto kidogo katika tumbo la Mariamu, akawaacha wawili tu mbinguni. Tumeona katika Maandiko kwamba kuwako yote - yakijumuishwa haya ya Mungu - anaishi kwa kuonekana, kwa umbo la mwili. Kwa hiyo tumeachwa tuone toka imani ya'kuishi kabla ya kuja’ Kristo ya kwamba kwa njia isiyoeleweka akiwa na mwili wa kuonekana alishuka toka mbinguni akaingia ndani ya tumbo la Mariamu. Elimu yote hii ya dini inayotatiza kuielewa ipo nje kabisa ya mafundisho ya Maandiko. Taarifa ya mwanzo wa Kristo haitoi sababu yoyote ya kufikiri kwamba akiwa na mwili wa kuonekana aliondoka mbinguni na halafu akaingia kwa Mariamu. Kwa hili ni kukosa shabaha kubwa ya ungano katika mafunzo ya utatu.

Malaika Gabrieli akamtokea Mariamu na ujumbe kuwa"tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyu atakuwa Mkuu, ataitwa mwana wa Aliye juu ……. Mariamu akamwambia Malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijuimume ? (Yaani, alikuwa bikira). Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu"(Luk. 1: 31 -35)

Mara mbili mkazo umetiwa kwamba Yesu atakuwa Mwana wa Mungu kwa kuzaliwa kwake; ni dhahiri Mwana wa Mungu hakuwahi kuishi kabla ya kuzaliwa. Tena, viarifa vingi vya wakati ujao vyahitajika kuangaliwa - k.m."atakuwa Mkuu". Ikiwa Yesu alikuwako na mwili kama Malaika alivyosema maneno na Mariamu, tayari angekuwa Mkuu. Yesu alikuwa ni"Shina na mzao wa Daudi"(Uf. 22: 16), neno la Kigriki'genos’ linadokeza kwamba Yesu'alizaliwa toka’ kwa Daudi.

MTUNGO WA MIMBA YA YESU

Kwa njia ya Roho Mtakatifu (Pumzi ya Mungu /uweza) akitenda kazi juu yake, Mariamu aliweza kupata mimba ya Yesu pasipo kukutana na mwanamume. Hivyo Yusufu hakuwa Baba wa kweli wa Yesu. Inabidi ieleweke ya kwamba Roho Mtakatifu si mtu (tazama somo la 2); Yesu ni mwana wa Mungu, siye Roho Mtakatifu. Mungu kwa kutumia Roho yake juu ya Mariamu,"kwa sababu hiyo hicho kitakatifu"kilichozaliwa naye,"ameitwa mwana wa Mungu"(Luk. 1:35). Kutumia neno"kwa sababu hiyo"linatoa shauri kwamba pasipo Roho Mtakatifu kutenda kazi katika tumbo la Mariamu, Yesu, mwana wa Mungu asingekuja kuishi.

Ikiwa Yesu alikuwa'mimba’ ndani ya tumbo la Mariamu (Lk. 1:31) ni ushahidi kwamba hakuwahi kuishi kimwili kabla ya wakati huu. Kama'tunafikiria’ wazo, linaanza ndani yetu. Vivyo hivyo Yesu alichukuliwa mimba ndani ya tumbo la Mariamu - alianza humo akiwa yai, kadri kama binadamu yeyote mwingine. Yohana 3:16 mstari maarufu sana wa Biblia, unatoa habari kwamba Yesu alikuwa"Mwana wa pekee wa Mungu".Mamilion ya watu wanaosimlia mstari huu wanashindwa kutafakari unachodokeza. Ikiwa Yesu alikuwa "mwanawe wa pekee", basi"alianza"kuzaliwa alipochukuliwa mimba ndani ya tumbo la Mariamu. Ikiwa Yesu alikuwa mwanwe Mungu na akiwa na Baba yake, huu ni ushahidi wazi kuwa Baba yake ni mkubwa kuliko yeye - Mungu hana mwanzo (Zab. 90: 2) na kwa sababu hiyo Yesu hawezi kuwa ni Mungu mwenyewe (somo la 8 linaeleza kwa upana maana hii).

Ni muhimu kuwa Yesu"alizaliwa"na Mungu kuliko kuwa aliumbwa, kama Adamu anavyofanywa awali. Jambo hili linaeleza ukaribu wa muungano wa Mungu na Yesu -"Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake"(2 Kor. 5:19) Kristo akiisha zaliwa na Mungu, kuliko kuumbwa toka mavumbi ya ardhi, inasaidia vile vile kueleza wepesi wake aliozaliwa nao kwa ajili ya njia za Mungu Baba yake.

Isa. 49: 5,6 ina unabii kumhusu Kristo kuwa ni nuru ya ulimwengu, ambao aliutimiza (Yn. 8: 12). Amesemwa kuwa anafanya upatanisho"kwa bwana aliyemuumba tangu tumboni ili awe mtumishi wake". Kwa hiyo Kristo"aliumbwa"na Mungu ndani ya tumbo la Mariamu, kwa uweza wa Roho yake Mtakatifu. Tumbo la Mariamu lilikuwa ni mahala palipokuwa dhahiri pa asili pa mwili wa Kristo.

Tumeanza katika somo la 7.1 kuwa zaburi 22 inatabiri mawazo ya Kristo pale msalabani. Aliwaza kwamba Mungu"ndiwe uliyenitoa tumboni …….. nalitupwa tangu tumboni: toka tumboni mwa mama yangu ndiwe Mungu wangu"(Zab. 22: 9,10). Wakati wake wa kufa, Kristo alitazama nyuma kwenye asili yake - katika tumbo la Mariamu mama yake, alipoumbwa kwa nguvu ya Mungu. Maelezo kabisa ya Mariamu katika Injili kuwa ni"Mama"yake Kristo yenyewe yanaondoa wazo la kuwa aliishi kabla ya kuzaliwa na Mariamu.

Mariamu alikuwa binadamu wa kawaida, mwenye desturi ya wazazi wanadamu. Imethibitishwa na ukweli kwamba alikuwa na binamu aliyemzaa Yohana mbatizaji, mtu wa kawaida (Lk. 1:36). Wazo la kanisa Katoliki la Roma la kuwa Mariamu hakuwa mwanadamu wenye mwili wa kawaida maana yake ni kwamba Kristo kwa pande mbili hakuwa ni"mwana wa Adamu" na"mwana wa Mungu". Haya ni majina yake mara kwa mara katika Agano Jipya lote. Alikuwa"mwana wa Adamu"kwa sababu ya kuwa na mama mwanadamu kabisa, na"mwana wa Mungu"kwa kuwa tendo la Mungu juu ya Mariamu lilifanya kazi kwa roho Mtakatifu (Lk. 1:35), inamaanisha kwamba Mungu alikuwa Baba yake. Mpangilio huu mzuri unafuatwa ikiwa Mariamu hakuwa mwanamke mwenye desturi ya kawaida.

"Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu ? Hapana awezaye. Mwnadamu ni kitu gani hata akawa safi ? huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata akawa na haki ? ……… au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke ?"(Ay. 14:4; 15:14; 25:4). Hii imekomesha ili pasiwepo na utata kwa jambo lolote la kuweza kutungwa mimba pasipo mawaa, aidha kwa Mariamu au Yesu.

Mariamu akiwa "amezaliwa na mwanamke", mwenye wazazi wanadamu wa kawaida, ilibidi alikuwa na uchafu wetu, Mwili wa mwanadamu, ambao naye Yesu akazaliwa nao,"amezaliwa na mwanamke"(Gal 4:4). Lugha ya kusema"amezaliwa"kwa njia ya Mariamu ni ushahidi tena kuwa hakuwahi kuishi kimwili bila yeye kuzaliwa.

Mara nyingi taarifa ya Injili inaonyesha Mariamu asili yake ya binadamu. Kristo ilimbidi amkaripie mara tatu kwa kukosa kuona kiroho (Luk. 2:49; Yohana 2:4); alishindwa kuelewa misemo yake yote (Luk. 2:50). Hivi ndivyo hasa tungetegemea mwanamke mwenye mwili wa mwanadamu, mwanawe alikuwa mwana wa Mungu, na kwa sababu hiyo mwenye kuona kwa kiroho zaidi kuliko yeye - Mariamu, ingawa Kristo, naye, alishiriki damu na mwili. Yusufu alishiriki na Mariamu baada ya kuzaliwa Kristo (Math. 1:25), hakuna sababu ya kufikiri kwamba hawakuwa na uhusiano wa ndoa ya kawaida tangu hapo na kuendelea.

Kutajwa"mama na ndugu zake"Kristo katika Math. 12:46,47 kwa sababu hiyo kulidokeza ya kwamba Mariamu alikuwa na watoto wengine baada ya Yesu. Yesu alikuwa wa pekee"Mzaliwa wake wa kwanza". Mafunzo ya katoliki ya kuwa Mariamu alibakia kuwa Bikira na kisha alipazaliwa mbinguni basi Biblia haisemi lolote kabisa. Kama binadamu mwenye mwili unaopatwa na mauti, Mariamu alizeeka na hatimae kufa; mbali na hivi tunasoma katika Yohana 3:13 "hakuna mtu aliyepaa mbinguni"ukweli kwamba Kristo alikuwa na mwili wa mwanadamu (ona Ebra. 2: 14 -18; Rum 8:3) maana yake ni kwamba mama yake nae alikuwa nao, tunaona Baba yake hakuwa nao.


  Back
Home
Next